Yung Forevér Profile picture
just wanna stay young forever | @arsenal & @SimbaSCTanzania | i witnessed Leo Mess winning world cup & 8TH ballon d'or ☝🏾|

Oct 8, 2022, 18 tweets

- Ni moja ya washkaji wanaojua ile kitu tunaita "Hardcore hip hop"

- Licha ya kua media zimemfumbia macho lakini hii haijafanya aache kuifanyia kazi talanta yake

- Leo nimekuandalia story ya maisha yake ya kimuziki, RT kisha shuka Nayo

#KiddyMusicBrief

- #Uzi 👇🏾

- Kwa majina kamili anaitwa Daniel Nwosu Jr., Maarufu kama "DAX"

- Ni msanii, muandishi na mtunzi wa nyimbo (song writer) ambapo alishtua industry ya hip hop kwa track yake ya "Dear God" na kujizolea Kijiji

- Alizaliwa March 22, 1994 Nigeria na kisha kulelewa huko sehemu moja inaitwa Ottawana, Canada

- Baadae akahamia Wichita, Marekani kuhudhuria masomo ya chuo kikuu, baadaye akahamia Los Angeles, California.

- Alihudhuria chuo kikuu cha Newman, ambako aliwahi kuchezea timu

ya vikapu ya Newman jets.

- Hapo awali alikua muandishi wa mashairi na motivational speaker kabla ajaanza rasmi career yake ya kurap

- Rasmi mnamo 2016 Dax alianza career yake ya kurap, ambapo inaelezwa aliandika shairi akiwa kwenye Bus na timu yake.

- Baada ya kumvutia moja ya wachezaji wenzake shairi hilo, Dax akagundua ana ustadi wa kuandika na kuandaa nyimbo

- Alianza rasmi kutangaza na kuachilia muziki wake kupitia account yake ya SoundCloud akidondosha mixtape kama 2pac Reincarnation Vol: 2 na As I told

- Mnamo mwaka 2017, Dax alipata umaarufu kwa video yake rasmi ya wimbo wake wa " Cash Me Outside" akimshirikisha Danielle Bregoli.

- Baada ya hapo ikawa ni Back to back, kufikia August 2018 akaachia EP yake ya kwanza kabisa ambayo inaenda kwa jina la "It's Different Now"

- "It's Different Now" ilifanya vizuri kwa kiasi chake na "Did it first" ulikua moja ya mikwaju bora ya hii EP

- Mnamo mwaka 2020 Dax alidondosha EP yake ya pili iliyoitwa "I'II Say It For You" ambapo hii ndio ilileta impact kubwa kubwa kwenye game yake na kupata

positive comments nyingi zaidi.

- EP ilikua na mikwaju 7 na single track ya kuitwa "Dear God" ambapo Dax anaumuuliza Mungu juu ya uwepo wake ulimwenguni ndio ulikua wimbo bora wa EP.

- Track hii ilisifiwa sana na wadau wa muziki kwa mada na maneno yake yaliyo jaa hisia kali

- Video ya wimbo huo imetazamwa mara Million 50 huko mjini yuchubu mpaka sasa na imesikilizwa mara Million 50 huko Spotify

- Mwaka huo huo Dax hakutaka kupoa, akatoa Misumali miwili "Faster" na "I don't want another sorry" akimshirikisha Tech N9ne na Trippie Redd

- Baadaye kidogo akatoa wimbo wa "Corona virus (State of emergency)" ambapo aliandika kuhusu janga la Corona

- Mnamo July 2021 Dax alitoa muendelezo wa "Dear God" ambapo alidondosha msumali wa kuitwa "Child Of God" ambapo hapo Dax alikua akimshukuru Mungu kwa yote aliyomtendea

- Mnamo August 2021, Dax alitangaza ujio wa album yake ya kwanza kabisa na kudondosha msumali wa kuitwa "Propaganda" akimshirikisha Tom MacDonald ikiwa ni wimbo wa utangulizi wa Album

- Msumali huu ulifanya vizuri mpaka kufikia kushika namba 15 kwenye chart za

Billboard ya R&B/Hip-hop Digital Song sales chart na kushika namba 9 kwenye Rap Digital Song sales chart.

- Mapema October 2021, wimbo wa tatu wa album iyo uitwao "40 Days 40 Nights" aliomshirikisha Nasty C ukatolewa.

- Kisha mnamo October 15, 2021 album yake hiyo ya kwanza

iitwayo "Pain Paints Painting" ilitolewa rasmi ikiwa na mikwaju 16 takatifu.

- Mnamo March 11, 22, Alitoa wimbo wake unaoitwa "Dear Alcohol" ambapo Dax aliandika mashairi kuhusu ulevi (madhara ya pombe na vitu ka izoo)

- Msumali huu ndio ukawa wimbo wa kwanza kuingia kweye chart za Hot 100 Billboard ukitinga namba 9 na kushika namba 28 kati nyimbo zinazofanya vizuri zaidi Marekani

- Humo ndani Dax kaongea vitu vingi akiangazia nyakati zake yeye akiwa addicted na Pombe na kumpoteza

kwenye ramani ya maisha.

- Kupitia kurasa zake (IG, TI & YT) Dax alisema kua huu wimbo ni unahusu maisha yake kabisa "This one is very personal to me" - alisema Dax

- Huu ni mwisho wa simulizi ya Dax, ila kwanini nilisema Media zimemfumbia macho

👉🏽 Kazi na kipaji chake havifanani na tension anayopewa, hapati interviews, Shows, promotion kama wasanii wengine na sababu kubwa huenda labda kwakua sio mzawa

👉🏽 Imani yangu inanithibitishia kama angakuwa anapakuliwa minofu kama rappers wengine asingekua Dax huyu

- Asante kwa muda wako, ulikua na mimi POPKIDDY!😎 Chaooow👊🏽

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling