My Authors
Read all threads
Fuatana nami katika Uzi huu ili ufahamu,
Uswahiba wa Rais wa kwanza wa Uganda Kabaka Edward Muteesa II na Milton Obote na mvurugano wa Idd Amin Dada. ImageImage
Kipindi Uganda ipo katika harakati za kusaka Uhuru kulikuwa na mvutano mkubwa baina yao wenyewe kutokana na kwamba baadhi ya makabila makubwa kuchukua nafasi kubwa ya kupigania Uhuru wa Taifa hilo lakini baadae wanafunzi wa Makerere waliona ni bora kuanzisha chama ambacho...
kitawapa muongozo kuelekea Uhuru.
Kikaanzishwa Chama cha Uganda People Congress (UPC) kilichukua jukumu zito la kudai uhuru, lakini kutokana na Utashi na uelewa wa siasa za ukombozi Kabaka Edward Muteesa II mfalme wa kabila la Buganda aliona atapoteza sifa hiyo na kuamua....
nayeye kuanzisha chama chake alichokiita Kabaka Yekka na mwaka 1962 aliomba kuunganisha nguvu na UPC ya Obote.
Obote aliona ukubwa wa kabila la Baganda akaona ni bora wapiganie uhuru kwa kusaidia na Kabaka.
kabila la Buganda lilikuwa na serikali yake yenye makao makuu yake Kampala Mengo kwahiyo Obote aliona imejitoshereza kabisa kushirikiana nao.
Baada ya Chama cha Kabaka Yekka kuungana na UPC hapo nguvu iliongezeka maradufu kushinikiza serikali ya kikoloni kuwaachia waganda wajiitawale, ndipo tarehe 9 Okt 1962 Uganda ilipata uhuru wake Kabaka Muteesa II akiwa ndio Rais wa kwanza wa Taifa hilo na Obote Makamu wa Rais. ImageImage
Serikali yao ilipendwa sana kwa mwaka mmoja wakiwa pamoja lakini dosari ilianza kuingia pale Milton Obote alipotaka nafasi ya Urais baada ya kuona upendeleo wa kabaka kuegemea kwa watu wake wa Kabila la Buganda na sio taifa zima kama ajenda ya muungano ya vyama vyao ulivyotaka.
Ilifika wakati mpaka Kabaka Muteesa ananunua silaha kwaajili yake binafsi na sio kwaajili ya Uganda jambo hili lilimkasirisha sana Obote na kumtazama Boss wake kama msaliti ,mchoyo na kiongozi asiyestahili kuwaongoza.
Kwakua bado makabila yalikuwa yanaruhusiwa kuongoza baadhi ya maeneo kwa kushirikiana na serikali ya taifa hilo, Milton Obote alianza kufanya visa kwa Kabaka ambapo aliamua kuchukua maeneo mawili ya Buganda ambayo ni Buyaga na Bugangayizi na kuyagawa kwa adui zao ...
kabila la Bunyoro jambo ili lilimfanya kabaka afanye vikao vya siri kujiondoa Uganda ili Buganda liwe taifa Huru😂.
Lakini mambo haya hayakuwezekana kwani Obote alikuwa amejenga uswahiba na Kamanda Fieldmarshel Idd Amin Dada na mipango yao ya kumuondoa kabaka ilikuwa imekamilika. Image
Walivamia Ikulu ya Kabaka iliyopo Mengo wanajeshi 1000 inadaiwa waliuwawa lakini Kabaka alifanikiwa kutoroka kwa mlango wa uwani, ilibainika baadae kuwa alipita nchini Rwanda na huko ndipo alipobahatika kwenda uhamishoni nchini Uingereza.
Picha ya ikulu ya Mengo ilivyoharibiwa. Image
Ushindi wa kumuondoa Kabaka ulimpa nafasi Obote kuwa rais kamili wa taifa hilo mwaka 1966, hapo akaafuta utawala makabila kama uchifu na ufalme na kuwafukuza kabisa huku akisema kuwa walikuwa wanaligawanyisha taifa hilo. Image
Mwaka 1969 November 19 Kabaka akiwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa aliamua kuwaalika baadhi ya watu washerehekee nae kwa kutimiza miaka 45, hiyo picha hapo inamuonesha akiwa anawekewa mvinyo (Wine) wanasema kabaka alikuwa vizuri kwenye kupiga vyombo . ImageImage
Siku hiyohiyo ilikuwa ndio mwisho wake pia kwenye ile wine aliokuwa anakunywa aliwekea sumu ambayo iligharimu maisha yake siku ya pili na kufariki.
BBC na Radio Uganda walikuwa wakwanza kuripoti taarifa hiyo lakini radio ya Uganda waliambiwa wasitangaze na kuwaomba msamaha raia kwa kuwapa habari wasioitaka inadaiwa amri ilitoka kwa Obote.
Obote aliamuru pia mwili wa Muteesa usirudishwe uzikwe huko huko Uingereza, Waganda walimchukia sana Obote kwani sio utamaduni wa kumzika mfalme wao na hata hivyo Rais wa kwanza wa taifa hilo kuzikwa uhamishoni lakini aliendelea kushikilia msimamo wake.
January 25, 1971 Obote akiwa katika kikao cha Commonwealth nchini Singapore General Idd Amin alimtumia Salamu kuwa abaki huko huko na yeye ndio rais, Amin akaapishwa siku hiyo hiyo ya mapinduzi. Image
Idd Amin alivyoingia madarakani akataka kufuta vidonda vya raia wake wa kabila la Buganda na kuandika barua ya kurudishwa kwa mwili wa Kabaka Muteesa ili uzikwe kwa heshima na jambo hilo likafanyika ImageImageImage
Picha 1: Idd Amin akiwa na mtoto wa Kabaka Muteesa ambaye ni mfalme wa Buganda kwasasa Kabaka Mwenda Muteebi.
Picha 2: Idd Amin akitoa heshima za mwisho kwa kabaka muteesa
Picha 3: Jeneza lenye mwili wa Kabaka likiwa mbele ya makaburi ya wafalme wa Buganda (Kasuubi Tombs) ImageImageImage
@threadreaderapp unroll this please
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with MSAFIRI

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!