My Authors
Read all threads
Mambo muhimu Maishani ambayo mara nyingi huwa hayafundishwi shuleni.

cc. @SwahiliBible
@MariaSTsehai
U hali gani mpenzi msomaji wa Nyuzi mbalimbali? Naamini unaendelea vema na unapambana kuhakikisha unatimiza yaliyo majukumu yako ya kila siku. Kutimiza ndoto zako yahitaji muda na malengo muhimu na thabiti. Japo vikwazo havikosi, Usife moyo siku zote mambo mazuri yanahitaji muda.
Niendelee kukusihi kuchukua tahadhari madhubuti juu ya Ugonjwa mbaya wa Corona. Fuatilia Taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu na matabibu.
Leo nitagusia kwa uchache juu ya mambo muhimu ambayo hawakufundishi shuleni ila yenye umuhimu mkubwa sana maishani. Kila mwaka tumekua tukishuhudia sherehe nyingi za wahitimu wa elimu katika Nyanja mbalimbali.
Nyuso zenye furaha sana na matumaini katika maisha yao wakitimiza kile ambacho wamekua wakipambania kwa muda mrefu. Ukweli ni kwamba wengi wamekua na matumaini makubwa ya kupata ajira katika vitengo mbali mbali serikalini na katika mashirika makubwa.
Wakiwaza juu ya mshahara mnono na marupurupu kadha wa kadha. Ukweli usiopingika Duniani ni kwamba kwa wale wanaohitimu shule kwa sasa Asilimia 35 tu ndio pekee waweza kua na ujuzi wa kupambana na soko la ajira duniani.
Si hivyo tu elimu na ujuzi vinavyotolewa vyuoni na mashuleni havikidhi vigezo vya mhitimu kupata ajira.
Sipingi elimu inayotolewa mashuleni ila ukweli ni kwamba asilimia ndogo sana ya yale unayojifunza hua unayatumia maishani,
Mfumo Rasmi wa Elimu una mambo mengi sana amabayo mengine kutokana na mazingira yetu hayana sehemu ya kutumika. Mwanafunzi anaweza soma mambo mengi katika safari ya Taaluma yake na mwisho akaja kufanya kazi tofauti kabisa ambayo hajaisomea.
Tusonge pamoja tujionee mambo kadhaa Muhimu ambayo Mfumo Rasmi haukufundishi ila lazima ujitahidi kuchukua muda wako kujifunza zaidi.
1.Namna ya kua na Hekima na Adabu ya Fedha. Tutakubaliana kwamba katika mifumo ya elimu ambayo ulishawahi kupitia bado hakuna mfumo hata mmoja ambao ulikufundisha namna ya kua makini katika matumizi na fedha zako.
Katika mazingira ya kila siku kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anajifunza namna ya kua na heshima ya fedha. Katika nchi za ulimwengu wa tatu huenda kisiwe kipaumbele sana maana unaweza omba omba kwa ndugu na jamaa hata ukiwa mtu mzima na familia yako.
Lakini kwa nchi za KIbepari ni ngumu sana kuona senti ya mtu Aliyomwaga jasho kuitafuta ikikufikia kilaini na kizembe, hiyo sahau. Kwa umri mtu anapohitimu yapaswa ajue hata namna ya kutengeneza bajeti yake binafsi ajue anatupata kiasi gani,
anatumia kiasi gani na Anaweka akiba kiasi gani ili kujikimu na siku za usoni. Adabu na hekima ya fedha itakupunguzia madeni yasiyo ya lazima maishani.
2.Kujitambua. Unaweza kujiuliza hivyi kweli msomi wa chuo kikuu anaweza asijitambue? Ila ukweli ni kwamba sio kila aliyeenda shule anajitambua wengine ni sehemu tu ya ukuaji. Kutokana na mazingira yao na Umri wao akili zao bado zimefungwa katika Makaratasi tu.
Msomi anakua hana hata malengo ya muda mfupi wala muda mrefu. Hana namna ya kutekeleza malengo yake zaidi sana anaishi kimiujiza tu. Anaenda tu kwa namna maisha yanavyobadilika na mwisho wa siku msomi anahitimu na kua na maisha magumu sana kuliko ya mtu ambae hajawahi kuhitimu.
Kujitambua kwa msomi ni pamoja na Kujua namna ya kutatua matatizo yake binafsi yanayomsibu. Kujifunza kufikiri kwa umakini nakufanya maamuzi ya msingi.
3.Namna ya kufanya mazungumzo na kusimamia ukweli. Wahitimu wengi hata hawajui namna ya kujieleza na kutengeneza hoja. Msomi safi lakini hana maarifa juu ya kuongea na wengine. Ifahamike tu kwamba baada ya kuhitimu huendi kuishi katika ulimwengu wako binafsi unaishi na watu.
Elimu uliyoipata yaweza kua haijielekezi moja kwa moja juu ya kuishi na watu ila kuna elimu ya mtaa na muhimu ambayo ni lazima uwe nayo. Je kama unafanya biashara ni namna gani unavyoweza jenga mazingira mema ya kufanya mazungumzo katika biashara?
Ni kwa namna gani unaweza wasilisha wazo na likubalike kwa wale wanaohitaji kufanya biashara na wewe?. Wahitimu hawajui kujieleza kwamba wanahitaji walipwe kiasi gani, wananyonywa na ni waoga hawawezi kusimamia wanachokijua.
4.Namna ya kuwekeza. Ni dhahiri kwamba shule hawafundishi namna ya kuwa tajiri hivyo kama ni ndoto yako kuwa mwekezaji jitahidi kupata mawazo na namna ya kufanya uwekezaji kadri uwezavyo. Wengi wana mawazo mazuri lakini mawazo hayo na ndoto zao zinaishia njiani.
Mfumo hautoi elimu ya moja kwa moja juu ya yale wanayohitaji kufanya. Ni vema ukatenga muda wa kujifunza namna Masoko ya hisa yanavyofanya kazi duniani, uwekezaji na sharia zake zilivyo katika maeneo mengi duniani,
La sivyo utabaki kua mtumwa wa elimu yako mpaka unazeeka. Matajiri wengi wanawafundisha watoto wao juu ya mambo haya ila Daraja la kati wengi hawana ujuzi na uelewa wa mambo haya. Tumia muda wako kujifunza.
5.Kujifunza kutokana na makosa. Kukosea na kushindwa ni jambo la msingi sana katika kujifunza. Ni kawaida ya mwanadamu kukosea na kwa nyakati nyingi tumekua tukikosea. Elimu haikufundishi kwamba kukosea kunaweza kua sahihi maana ukikosea ni kwamba hujui.
Kwenye maisha mambo ni tofauti sana unaweza kua unajua unalolifanya nab ado ukafeli. Kwenye uwanja wa maisha jkufeli ni sehemu ya kwamba una jambo unalolifahamu hivyo unahitaji muda tena wa kuinuka.
6.Namna Bima zinavyofanya kazi. Katika ulimwengu ambao mambo mengi yamekua yakibadilika na kila siku mambo mapya yanatokea, je ulishawahi kujifunza aina za bima na namna unavyoweza nufaika kwazo?
Wasomi pia hawana uelewa binafsi namna bima zinzvyosaidia kurahisisha maisha pale ambapo wanakua wamekwama. Mfano, Bima muhimu ya Afya pia kwa walio wengi hukoma pale wanapohitimu maana hawana misingi maalumu .
ya kuendelea kulipia na hawana uelewa kwamba waweza kosa fedha taslimu ila kwa vile ni wanufaika Bima inaweza kuwaokoa kwa kiasi kukubwa na kuwapa huduma stahiki.
Zipo bima zingine pia muhimu kama zile za thamani kama nyumba, magari n.k ila pia zipo bima za maisha. Ni vema upate muda wako ujifunze juu ya haya.
7.Elimu ya mlipa kodi. Kama mwananchi kuna umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kuelewa mfumo mzima wa Kodi namna kodi zinavyokusanywa lakini pia wajue namna matumizi yalivyo. Ni ukweli usiopingika kwamba kuna wanafunzi
hawajui kwamba wanalipa kodi pale wanapofanya manunuzi, vile vile baada ya wao kuhitimu hawajui asilimia ya kodi inayokatwa katika mishahara yao inafanyia kazi gani. Mambo muhim u yenye manufaa kwa maisha yao na Taifa lao.
Mifumo hii muhimu ya kodi ni vema ikajulikana kwa kila mwanafunzi maana baadae anaweza kuwaajiri na kuajiriwa sehemu Fulani. Mambo haya yasiwe mageni kwake.
8.Haki za msingi za kikatiba. Katiba ni nini? Ina vipengele gani muhimu vinavyokuhusu kwenye katiba? Haki za kikatiba kama mwananchi ni zipi? Leo hii ni ngumu sana kwa namna mifumo ilivyo mwanafunzi kukuelezea hatua kwa hatua haki zake za msingi pale polisi anapokuja kumkamata.
Ni vitu gani vya msingi polisi anapaswa kua navyo? Kwa kiasi kidogo sana kwa wale waliosoma sharia wanaweza elewa ila wengi hawana uelewa, Haki za msingi za mtuhumiwa hawazifahamu? Haki ya kupata huduma Fulani ambayo ni muhimu,
namna ya kupeleka malalamiko yako kwa ngazi muhimu za kisheria ni mtihani kwa wanafunzi na wahitimu wengi. Wengi wameonewa na hawaelewi haki za msingi hata maeneo ya kazi baada ya wao kuajiriwa.
9.Kufanya kazi kwa pamoja kama Timu. (Team Work). Maeneo mengi ya kujifunza ni mara chache huwa watu hukaa pamoja na kufanya mambo kwenye timu. Wataalamu wanasema watu wenye malengo yanayoendana ni rahisi sana kufika mbali.
Zaidi ya kazi za kikundi Elimu haifundishi namna mnavyoweza badili kundi lile kubadilisha maisha yenu. Si kila jambo waweza likamilisha mwenyewe kwa nguvu zako. Ila unaweza ungana na watu baadhi wenye njozi kama zako na mnaweza fika mbali sana.
Zipo fursa za mfuko wa vijana katika kila halmashauri, hawawezi kukuamini wewe peke yako lakini mkijiunga kwenye kundi la watu kadhaaa mkaweka malengo ya mradi wenu ni rahisi sana kuaminiwa na kusaidiwa na mtabadilisha maisha yenu.
10.Thamani ya maisha yako haishikiliwi na vyeti ulivyovipata shuleni. Wapo wengi wamepoteza utu Heshima na adabu mara baada tu ya kuhitimu masomo yao. Kitu ambacho shule haikufundishi ni kwamba yapo mambo mengi sana unayoweza kuyafanya na yakabadili maisha yako nje ya
namna vyeti vyako vinavyoonesha. Si lazima ukomae kutafuta na kutegemea cheti chako tu yapo maarifa na mambo mengine mema na mazuri upande mwingine. Ni kweli umebobea lakini Thamani ya maisha yako ni kubwa kuliko cheti hicho.
Mambo ni mengi lakini kwa haya machache yakufanye wewe unayesoma (mwanafunzi) au Yule aliyehitimu kuendelea kukumbuka kwamba maisha yanaendelea baada ya kuhitimu hivyo ni lazima uwe mpole na mbunifu maana shule haikufundishi kila jambo. Shule inakufundisha ila haikupi kazi,
Thamini muda, Fanya maamuzi muhimu, Fikiria vema, Pata muda wa mapumziko ila pia jifunze zaidi, kua na mpango mbadala wa kufanya pale mpango maalumu unapokwama, Jithamini na vifahamu vipaumbele na vipaji vyako, Tafuta Mentor akufundishe na akuelekeze vema,
jiheshimu na waheshimu wengine na jifunze namna ya kuhimili hali halisi.Teknolojia inabadili mambo mengi mengine yaweza athiri kazi yako, Weka muda kuyafahamu, Soma nyakati. Yale ambayo hufundishwi kwenye mfumo rasmi ni mengi kuliko unayojifunza kua tayari kujifunza kila mara.
Elimu haina mwisho kwa yeye anayehitaji kujifunza ila ina ukomo kwa anayedhani ni lazima awe kwenye mfumo rasmi. Elimu ni Fursa tuitumie vema inaweza kubadilisha maisha yetu, jamii na Taifa kwa ujumla.
Kwa leo nakomea hapa. Tukutane wakati mwingine. Kama unahitaji kuwekeza Afrika kuna fursa nyingi sana karibu jci.co.tz tuwekeze pamoja. Ahsanteni sana.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with WIlly

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!