My Authors
Read all threads
Karibu kwenye simulizi za kweli za mapenzi za #Tommy'smission. Leo tunaanza na
PENZI LA ONLINE💕
Mitandao ya kijamii imesaidia sana watu kutoka mahala mbalimbali kufahamiana na wengine kupata wenza wa maisha yao. Nami nikiwa kama mmoja wao leo nashuka na UZI HUU 👇 👇 👇
Story inaanza kama miaka minne nyuma nilivyokuwa kidato cha tano pale Uboizin UMBWE. Kama unavyojua kuishi uboizini kipindi cha likizo magroup na shule za wasichana yanakuwa kibao😁 si unaelewa watu wenye ukame wakikutana😂
Ilikuwa ni likizo pale ambapo mwanangu bichwa akafanya kuniadd kwenye group kwa lengo la kwenda kulichangamsha maan mimi kwa fujo tu nipo njema😁. Nakumbuka ilikua usiku naadiwa kweny group nikakuta lipo kimya basi nikaanza kujichatisha pale mpaka saa saba 😂😂.. nina makusudi
Ile amsha amsha mwanangu akanifata inbox akanicheki baba kazi nzuri, enhee baba yenu nikisifiwa tu huwa naongeza dozi. Basi asubuhi na mapema nikaamka nao baba moto ule ule mpaka kuna mdada mmoja ndo mwenye story sasa akanifata inbox🤗 pata maji kwanza maan mbele patamu😋
Akaja na moto inbox nikampoza na mijibu yangu ya uswazi si munaelewa watoto wa mbagala😎 enheee mimi ni wa mbagala japo ni wakishua kidogo.Alijitambulisha anaitwa Maimuna. Mtoto akawa anaenjoy company yangu maana huwa sinaga maringo ukija inbox as long as unastories mbona sahf.👇
Ikapita kama wiki ivi mtoto nachat nae sana kama dozi yaan asubuhi mchana na usiku. Kuna iyo siku sasa nikakosa bando nikawa sipatikani Whatsapp kwa siku mbili mfululizo mtoto akaamua kunipigia kuuliza nini shida mpaka nipo kimya vile. Wazee sikutegemea 👇👇👇
Aliniuliza mbona haupo whatsapp nikamjibu tatizo vocha mama akaanza kulalamika kuwa siningesema mapema mambo madogo madogo hayo ayamalize basi baada ya michambo nikatumiwa vocha😋 siwafichi kuhusu bando nikawa siwazi kijana wenu maan vya wiki kwangu ikawa sahf tu👇👇
Utamu ulizidi pale alipoanza videoCalls wazee ndo iyo day naona mali sahf😋 mate yalinitoka kijana wenu maan mtoto alikuwa mzuri mpaka nashindwa wa kumfananisha nae au vuta picha wewe toto la kigita lenye shombe shombe za kiarabu mrefu kiasi,huko nyuma sungura Pale mungu kaumba😋
Ile mitego ya kwenye videocall kijana wenu nikaona nitupe wavu anhaaa sikukosea timing wazee mai akajaa basi kuanzia pale mazuri yakawa upande wangu maan niseme nini ninyimwe mimi. Ila tatizo lilikuwa kwenye kukutana nae yaan alikua anabanwa wanangu mpaka sio vizuri👇👇
Nilikuja kuonana na maimuna baada ya kumaliza kidato cha sita maan kipindi chote shule alikua anapelekwa na kufutwa kipindi cha likizo. Tulipomaliza kidogo ikawa nafuu. Iyo day nimechill tu mtaani sina habar inaingia text yake njoo mlimani city mida hii😲😲 nikicheki nipo mbagala
Nikasema sio kesi mwanaume nikajikoki chap kwa haraka nikaunga nauli kwa wanangu nikawahi namba mliman. Wazee sijui ilikua ni ushua wake au malezi mtoto anajali muda sana mpaka sio vizur yaan nilichelewa dk 5 tu na hakutaka kusubiri kasepa nafika pale hamna mtu😖.
Nilitaman nimtukane ila nikasema boss anuniwi 😁 nimfokee vocha na ela za viwalo nitatoa wapi?? Wee nikapoa nikarudi home kinyonge.
Kumbe ile ilikua ni lazima nikutane nae tu ikapita kama wiki nakumbuka @SimbaSCTanzania ilikuwa inacheza na @SevillaFC_ENG pale taifa
Mtoto akanipanga tuonane mbezi mida ya saa mbili usiku wanangu sikudelay chap tu nikaruka nikaaga naenda kucheki mpira taifa. Pata ndinga mpaka mbezi nikamkuta kabla hata ya salamu nikapokewa na romance zito hakujali watu wala nini.👇👇
Nakuja kukaa sawa akanifuta eneo tukachill stori zikaanza mambo kibao maan nilihis kama ndoto. Yalivyokuwa hot nikaanza kuwaza wapi napata guest😂 maan mtu mwenyew anapatikana kwa shida wakati nawaza ivyo ikapigwa simu kwake..👇👇👇
Alikua ni dada ake na aliongea nae ile sisi ndo tunarudi upo wapi?? Akajibu narudi sasa ivi😖 wanangu alikata simu chap alf kwa saut ya upole akaniita TOMMY im sorry i have to go na sijui ni lini tutaonana maan kesho kutwa naenda kwa baba yupo Sweden.😖
Wanangu nilipigwa ganzi kila kiungo nilikua kama gogo pale ikabidi nimwambie tu ebu nikuwahishe na mimi niwahi home mambo yasiwe mingi.
Uko moyoni hasira wanangu nimepoteza sana muda kumsubiri alf inakua ivi?? Sikuwa na namna nilimsindikiza hadi kituoni kwao pale korogwe
Mimi nikaendelea na safar maan sikutaka mengi nipo njiani anatuma voice notes analia mimi akili yangu haipo na yeye mda huo nishamaindi nikaona uchawi tu. Ukweli nilizama kwenye hili penzi ila sikuwa kua nae maan aliondoka na kwenda kuishi na mzee wake na mimi npo tu mbagala hapa
Naunga unga mwana nipate chochote siku ipite✊

Shukran kwa muda wako🙏
Simulizi powered by @travellers_tz
@_challah75 @fungojnr pamoja na @MpwaOG
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with T R A V E L L E R S 🇹🇿

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!