My Authors
Read all threads
KWANINI UHAMIE WINDOWS 10 KUTOKA WINDOWS 7?

Inawezekana unaipenda sana windows7. Inawezekana pia computer yako ina taarifu nyingi ambazo usingependa uzipoteze. Lakini mifumo ya uendeshaji (OS) ya Microsoft hukamilisha muda wake kila baada ya miaka 10.

T H R E A D 👇👇
Kufikia January 14 mwaka huu, kampuni ya Microsoft iliacha kutoa matoleo (updates) mbalimbali kuhusu windows7. Hivyo, matoleo ya kiusalama, speed n.k yalikomea hapo na kufanya kama unatumia Windows7 baada ya tarehe hio, basi computer yako ipo hatarini kushambuliwa kimtandao
.,kwa kuwa hakuna uimara wa kiusalama tena katika mifumo ya uendeshaji (OS) ya computer yako.

JE, COMPUTER ITAZIMA BAADA YA UKOMO HUO?
Hapana, computer yako yenye windows7 itaendelea kufanya kazi kama kawaida isipokuwa, Microsoft hawatakupa updates za kuisalama wala marekebisho
yoyote ya kiautomatiki yaliyokua yakitolewa hapo kabla. Hii itaifanya computer yako kuwa katila hatari kubwa ya kuvamiwa na virusi au mashambulio ya kimtandao yatakayoelekezwa kwako muda wowote upenyo ukipatikana.
KWANI LAZIMA KUWEKA WINDOWS 10?
Sio lazima, wala hakuna mtu atakulazimisha kuanza kutumia windows10. Lakini ni jambo muhimu na la busara zaidi kuimarisha mifumo tendaji (OS) ya computer yako kwa kuwa windows10 imetengenezwa kwa uimara zaidi katika matoleo ya kiusalama, antivirus
iliyojishikiza (built-in antivirus) na Windows defender ambazo hukulinda zaidi dhidi ya shambulio lolote la kimtandao.

KWANINI MICROSOFT WAMEIACHA WINDOWS 7?
Microsoft wana utaratibu wao wa kisera (Fixed Lifestyle Policy) ambao unazipa muda wa kuhudumu bidhaa zao mbalimbali.
Mfano, Windows 7 ilitoka kwa mara ya kwanza October 2009, hivyo miaka yake 10 ya kuhudumu imehitimishwa January 14 mwaka huu (japo imechelewa kidogo kufikia ukomo wake). Hii windows 10 inayopigiwa chapuo ilizinduliwa mwaka 2015 na inatarajiwa kuhudumu kwa miaka 10 mpaka 2025.
Sasa windows 10 ilikus ni bure kabisa kuinstall mpaka kufikia majira ya kiangazi cha mwaka 2016. Lakini, ofa hio iliishia hapo ambapo kwa sasa itakulazimu kulipia gharama za kufanya installation kama unatumia matoleo ya zamani ya mifumo tendaji. Windows10 ya kawaida (Home edition
hugharimu dola za kimarekani $ 139.99 na ile ya kiuweledi (Pro edition) itakugharimu dola za kimarekani $ 199.99 kuipata katika majukwaa ya kimtandao ya Microsoft.
Sasa Leo tukiacha yote hayo, nataka nikupe faida 10 za kutumia windows10 kama mfumo tendaji katika computer yako:
1. USALAMA
Windows10 imerithi mifumo ya kiusalama kutokes kwenye toleo ls nyuma yake la windows8, hivyo kuifanya windows10 kuwa salama zaidi. Hii ni kwa kuws code yoyote ambayo huanza kufanya kazi pale computer inapowaka, basi code hio ni lazima ipewe kibali na Microsoft au
watengenezaji wa Hardware (Dell, hp n.k). Lakini zaidi ya windows8, windows10 imetengenezwa kuhakikisha codes zake haziwezi kuvukwa (kuwa bypassed). Kuboresha huduma, hivi karibuni Microsoft wameongeza features katika usalama zaidi za Ransomware Protection na Threat Protection.
2. SPEED
Kuanzia pale unapowasha computer yako pengine ni spidi kuliko computer zenye MacOS japokuwa mifumo tendaji ys Mac imeonekana muda mrefu kuwa ipo fasta zaidi. Safari hii imekula kwao😂. Injini ya 3D iitwayo DirectX 12, ambayo watengenezaji wa michezo ya video(video games)
huitumia kurahisisha matengenezo na viwango vya michezo hio, hufanya kazi vizuri zaidi katika windows10 kuliko katika matoleo mengine.
3. CORTANA
Ebwana eeh, nna uhakika hata wewe huwa unafurahi sana pale unapoweza kuzungumza/kukiamuru kifaa chako kufanya jambo unalolitaka kwa sauti tu. Hapa watumiaji wa iPhone na yule "Siri" wao watakuwa wananipata vizuri sana.
Sasa kwenye Windows10 kuna feature inaitwa "Cortana" ambayo ni teknolojia ya Sauti ambayo unaweza kuiamuru ifanye shughuli mbalimbali zilizopo kwenye computer yako kama "Hey Cortana, Cheza muvi ya Ray Kigosi, Imba wimbo wa Ray C, Onyesha picha ya Mr. Blue, zima computer." n.k
Hivyo vyote vinaweza kufanyika kwa sauti yako tu kupitia Kipengele hicho ndani ya computer yako yenye Windows10. Kumbe mambo ni murua bwana..😀
4. START MENU
Kama ulikua hufahamu basi Windows95 ambayo ilitoka mwaka 1995 ilikua na kipengele cha menu ambayo inafanana na menu ya windows8. Lakini watu waliilalamikia sana kuwa menu ile ilikua na mambo mengi hivyo kulazimisha Microsoft kuiondoa katika matoleo yake yaliyofuata.
Lakini ajabu ni kwamba baada ya kubuni start menu ambayo ilitumika kwenye matoleo ya windows98 mpaka windows7 bado watu wengi walikua wakilalamika kuwa menu haijakaa vizuri mpaka ilipotoka windows8 na start screen yake.
Hivyo toleo la Windows10 limeboreshwa zaidi na kuipa
muonekano bora Start Menu yake na kuifanya yenye kuvutia na rahisi kutumia. Mudhui yake yameifanya iwe bora zaidi kwa kufanya Apps muhimu zaidi ziweze kuongezeka ukubwa na zile zenye umuhimu kidogo zinaweza kufanywa ndogo ili iwe rahisi hata kuchagua kwa kutumia kipanya (mouse).
5. TOUCH
Kama kila kifaa unachotumia kimetengenezwa kuruhusu teknolojia ya "Touch screen" kuanzia simu janja, redio za gari, tablet mpaka mifumo ya ramani elekezi (navigation systems). Sasa kwanini isiwezekane katika computer yako pia? Kuna watu watasema "oh kioo cha Pc
ukiwa unakigusa gusa kinachafuka na kuharibika" Sasa hilo linakuaje tatizo kwenye Pc na lisiwe kwenye simu yako ambayo kioo chake ni kidogo zaidi. Basi kama ulikua hujui, computer zilizotengenezwa kupokea teknolijia ya "Touch screen" hufanya kazi kwa ufanisi zaidi pale zinapokuwa
na Windows10 kuliko zile zinazokua na mifumo tendaji mingine. Pc kama Lenovo IdeaCenter Yoga A940, The Surface Pro7, Convertible Tablet na Acer T232HL ambazo zimewezeshwa na Touch screen hufanya kazi kwa ufanisi zikiwa na Windows10 kuliko hata Tablet za iOS katika mambo mengi.
6. KIVINJARI BORA
Hakuna tena mambo ya Internet Explorer. Sasa hivi ni mwendo wa Microsoft Edge ambayo ni balaa..🔥🔥 Hii Microsoft Edge imefanywa kuwa bora sana katika speed, vipengele (features) kama web page markup na reading mode. Vile vile hii Edge inatajwa
kuwa inatumia kiasi kidogo cha umeme (Power use) kuliko kiasi kinachohitajika katika kivinjari chs Google Chrome. Inategemewa katika maboresho yajayo kutakuwa na matafuto ya mtandaoni kupitia "Cortana" katika hii Microsoft Edge. Watu wamejipanga bwana.
7. KUCHAPA(TYPING) KWA SAUTI
Kirahisi kabisa, bonyeza alama ya Windows na kitufe H (Ili kuiamuru computer yako ianze kukusikiliza). Halafu anza kuongea kila unachotaka kichapishwe kwenye nyaraka yako. Hakuna haja ya kutatanisha mambo hapa. Wale wavivu wa kuchapa hapa ndo kwenyewe
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Faustine

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!