Faustine Profile picture
Website Designer | S.E.O Expert | Founder, Rednet Technologies | We help your business to grow online. Send TIP on LIPA NAMBA 5432715 (M-PESA)
Mar 12, 2022 25 tweets 8 min read
VITA VYA KIUCHUMI NA KIMTANDAO VYA NATO vs URUSI:

Zamani vikwazo vya kiuchumi vilikua ni kadhia kweli. Ilikua ni kama kufungiwa usitumie akaunti yako ya benki. Haiumi sana coz unaweza kufungua akaunti kwenye benki nyingine maisha yakaendelea.

Lakini leo mambo ni tofauti.

UZI👇 Sasa pata picha ufungiwe kwenye benki zote, yani usiweze kufungua akaunti, wala kutuma pesa, wala kutumiwa pesa.
Imagine utakuwa kwenye hali gani.

Sasa hiko ndo kinachoikuta Urusi. Marekani na washirika wake wa NATO wamedhamiria kuitoa Urusi kwenye mfumo wa fedha duniani.
Mar 30, 2021 25 tweets 7 min read
IFAHAMU AINA MPYA YA UDALALI WA MTANDAONI (DROPSHIPPING)

Dunia inakwenda kasi sana na Teknolojia inazidi kusambaa na kuteka sekta za kiuchumi. Mwandishi mmoja alinukuliwa akisema "In this modern world, prepare to change your career."

Umeshafikiria kuwa Dalali smart?

THREAD👇 Kwa Afrika yenye watumiaji wa huduma za internet wanaokadiriwa kuzidi milioni 400, tafiti zinaonyesha fursa za kuongezeka kwa biashara za mtandaoni (e-commerce) sasa ni kubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Shirika la Statista linakadiria sekta ya e-commerce kufikia thamani ya..
Sep 5, 2020 20 tweets 7 min read
BRANDING Vs MARKETING. KIPI NI KIPI?

Unapofanya biashara, moja kati ya malengo makubwa ni Kupata/kuendelea kupata wateja kila siku. Wateja ndio Roho ya biashara. Hakuna biashara kama hakuna wateja. Lakini unawapataje wateja hao? Unatumia vipi Marketing strategy/Branding?

UZI👇 Unapokuwa unaitengeneza biashara yako unatumia mbinu nyingi sana kujitangaza na kuvuta wateja wengi kwa kadiri inavyowezekana. Kuna wanaotumia ndugu, jamaa wa karibu, classmates, colleagues n.k. Ili mradi tu connections zinahusika kwa ukubwa wake. Kuna wengine wanatumia mitandao
Aug 29, 2020 25 tweets 8 min read
UFAHAMU MFUMO WA KODI NA MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA

Serikali za mitaa zikiwa ndani ya Halmashauri za miji/Majiji na Wilaya zina mamlaka ya kukusanya mapato na ushuru kutoka vyanzo mbalimbali vya kodi. Pia zina mamlaka ya kutumia mapato hayo kwa mujibu wa sheria.

T H R E A D👇 Kulingana na mipaka ya kisheria inayowekwa na Serikali Kuu, hizi Serikali za mitaa zina uwezo wa kutengeneza sera zake za mapato ili kuleta maendeleo katika shughuli zinazogusa kwa ukaribu maendeleo jamii nzima kama mashule, hospitali, mazingira ya mitaa na ulinzi shirikishi.
Jul 9, 2020 25 tweets 5 min read
KWANINI UHAMIE WINDOWS 10 KUTOKA WINDOWS 7?

Inawezekana unaipenda sana windows7. Inawezekana pia computer yako ina taarifu nyingi ambazo usingependa uzipoteze. Lakini mifumo ya uendeshaji (OS) ya Microsoft hukamilisha muda wake kila baada ya miaka 10.

T H R E A D 👇👇 Kufikia January 14 mwaka huu, kampuni ya Microsoft iliacha kutoa matoleo (updates) mbalimbali kuhusu windows7. Hivyo, matoleo ya kiusalama, speed n.k yalikomea hapo na kufanya kama unatumia Windows7 baada ya tarehe hio, basi computer yako ipo hatarini kushambuliwa kimtandao