My Authors
Read all threads
Mwaka 1910 Akiwa na Miaka 23 Padre Pio wa Italia Alitokewa na Vidonda Mikononi na Miguuni Kama Aliyetobolewa na Misumali, Havikupona Kwa Miaka 58, Siku 3 Kabla ya Kifo. Alikuwa Anapigwa Mijeredi Kimaajabu. Alimtabiria Upapa John Paul II Miaka 31 Kabla. Alimuombea Kipofu #UZI👇👇
Padre Pio ni mmoja wa viongozi wa dini maarufu sana kuwahi kutokea duniani anayetajwa kuwa alikuwa na imani kali sana ya dini yake, alikuwa muumini wa kanisa katoliki raia wa Italia, alizaliwa Mei 25, 1887 na kufariki September 23, 1968. 👇👇
Dalili za kuijua dini ndani yake zilianza kuonekana tangu akiwa mdogo kwani mara kadhaa alikuwa anadai kuwa amezungumza na malaika, Yesu pamoja na Bikra Maria. September 21, 1910 akiwa na umri wa miaka 23 wakati ametawazwa kuwa mtawa alitokewa na vidonda katika mikono na 👇👇
miguu yake mfano wa vidonda alivyovipata Yesu kutokana na kusurubishwa msalabani, vidonda hivyo alikaa navyo kwa miaka 58 bila kupona. Ajabu ni kwamba siku tatu tuu kabla ya kifo chake vidonda vyote vilipona. Padre Pio anaelezwa kuwa alikuwa ana uwezo wa kuisoma nafsi 👇👇
a mtu na kujua mtu huyo anawaza vitu gani, na hata ilikuwa muumini ukienda kuungama dhambi kwake, baada ya kutaja madhambi yako anakwambia kabisa kuwa dhambi fulani na fulani umezisahau, tubu zote. March 21, 1912 Pio alimuandikia barua padre mwenzake Agostino akiandika mambo 👇👇
mengi ya kimiujiza ambayo Padre Agostino alikiri kutoelewa na ikaelezwa kuwa ni mambo yanayopatikana katika kitabu cha siri cha Maria Gemma aliyefariki mwaka 1903 akiwa na umri wa miaka 25. Kama ilivyo kwa Padre Pio, ndivyo alivyokuwa pia Maria, naye aliyapata makovu hayo 👇👇
hayo June 8, 1899 akiwa na umri wa miaka 21, alidai pia kuwa huongea na malaika mbalimbali, Yesu na hata Bikra Maria ambao walikuwa wanampa jumbe kadhaa kuhusu mambo yajayo. Baada ya barua hiyo Padre Pio alikataa kwamba hana kitabu hicho kilichowahi kuandikwa na Maria ambaye 👇👇
aliitwa pia bikira Maria. September 20, 1918 Pio alikiri wazi kuwa katika maombi yake hakuwahi kuomba apone madonda hayo yakiwemo ya miguuni na mikononi kama mtu aliyepigiliwa misumali, licha ya kuwa yalikuwa na maumivu makali na kutoa damu kila siku lakini alisema anapenda 👇👇
anavyoteseka. Alisema kuwa damu zilizokuwa zikitoka katika madonda hayo alikuwa anazisafisha na manukato maalumu au maua, hali hii ya kupata vidonda kama hivi inaitwa Stigmata, inahusiana na imani za dini hasa Ukristo. Pio Alimwambia Agostino kuwa alikuwa akipata uchungu 👇👇
wa taji la miiba na mara nyingine alikuwa anapigwa mijeredi kimiujiza. Hakufafanua zaidi kuhusu matukio haya lakini alisema kuwa amekuwa akisumbuliwa nayo angalau mara moja kwa wiki kwa miaka kadhaa. Kama ilivyo kawaida, wanasayansi ni lazima watie miguu katika kila jambo 👇👇
linaloonekana kuiteka dunia, walifanya uchunguzi wao katika hili pia na mwaka 1954 walisema kuwa inawezekana madonda hayo Pio aliyatengeneza mwenyewe kwa kujidondoshea asidi aina ya carbolic. Mwaka 1947 Padre Pio alimponya upofu msichana mdogo Gemma de Giorgi wa umri wa 👇👇
miaka 7 aliyesafiri na bibi yake kutoka Sacile hadi San Giovanni Rotondo kumuona Pio. Gemma alidaiwa kuzaliwa bila pupils za macho hivyo kuambiwa kuwa hataweza kuona katika maisha yake yote. Mwaka 1947 pia Padre Pio alikutana na Padre Karol Wojtyła wa Poland, mbali na 👇👇
mazungumzo mengine pia akamwambia ajiandae kuwa kiongozi mkubwa wa kanisa duniani, kweli mwaka 1978 Wojtyła akatangazwa kuwa ndiye Papa mpya wa kanisa katoliki duniani miaka 31 baada ya utabiri. Karol Wojtyła ndiye Papa John Paul II aliyekuwa kiongozi mkuu wa 👇👇
kanisa katoliki duniani, Papa kuanzia mwaka 1978 hadi anafariki mwaka 2005. Mwaka 1962 tena Padre Wojtyła alimuandikia barua Padre Pio akimuomba kumuombea rafiki yake Wanda Półtawska aliyekuwa anaugua kansa huku akiambiwa kuwa amebakiza miezi 18 pekee ya kuishi, baada ya Pio 👇👇
kupokea barua hiyo alimuombea, na kansa ikapotea. Wanda aliyezaliwa mwaka 1921 yuko hai mpaka sasa, yeye ni mwandishi na mwanafizikia kutoka Poland, aina hii ya kansa kupotea kimaajabu inaitwa Spontaneous Remission, hata madaktari walishindwa kuelezea imekuwaje Wanda kawa 👇👇
mzima hana kansa tena. September 21, 1968 akiwa anatimiza miaka 58 tangu apatwe na Stigmata, Pio hali yake ilianza kuwa mbaya, na hatimaye akafariki siku mbili baadaye September 23, 1968 akiwa na umri wa miaka 81. Ajabu ni kuwa ndani ya siku hizo tatu hali yake ianze kuwa 👇👇
mbaya vidonda vyake vilipona kabisa. March 3, 2008 ikiwa ni miaka 40 imepita tangu afariki kaburi lake lilianza kuumuka, kuvimba hali iliyopelekea mabaki ya mwili wake kuondolewa kaburini humo na sasa yapo katika sehemu maalumu ya makumbusho mjini San Giovanni Rotondo in Italy.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with FM facts

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!