FAHAMU JUU YA SIFA NA TARATIBU ZA KUWA URUBANI
-THREAD HOW TO BE PILOT-
Leo nitapenda tuongelee mambo machache juu ya Urubani watu wengi tumekua hatuna uelewa juu ya urubani kuhofia gharama....
🔁 Retweet iwafikie wengii #ElimikaWikiendi
Shuka nao👇👇👇
Watanzania wengi hatuna uelewa tosha juu ya fani ya Urubani hii ni kutokana na kuogopa gharama kubwaa za Urubani pia na kupotoshana kwamba hatuna vigezo
Urubani ni kazi zilivyo kama kazi nyingine na inaingiza kipato kikubwa mno ikiwa ipo miongoni mwa kazi zenye kulipa vizuri na hulipa kuanzia $20,000-$40,000 per year hii inaongezeka kulingana na shirika husika
Nifanye nini niwe Rubani.....Wengi nchini kwetu tunaambizana kusoma urubani ni lazima umalize PGM high school tukizani urubani ni kama degree wakati si kweli Hakuna ulazima wa kuwa PGM ndio uwe Rubani lakini itakusaidia kuwa vizuri maana Geography itakuasaidia katika location
Kwenye urubani husomi kama Degree yaani miaka mitatu unamaliza hapana hapa tunafanya mafunzo kwa grade....
Kuna mafunzo ya awali ambapo ukihitimu unakua umepata Private Pilot Licence (PPL)
Then unapata Commercial Pilot License (CPL) hii ndio tunaowaona wanaoendesha bombardier
Key requirements to Join Flight School
➡️Uwe na miaka walau 16yrs
➡️Uwe umemaliza Ordinary secondary education level na uwe na ufaulu mzuri walau C 4 kwenye somo la kiingereza na physics itakusaidia
➡️ English language lazima uijue fluent maana ndiyo lugha ya mawasiliano
➡️Uwe umepass vigezo vya aviation health examination
➡️Uwe unaweza kulipa Ada katika flight school...
➡️Mengineyo kama urefu weight baadhi ya vyuo wanaconsider kama ethiopia
hivyo vigezo ni kulingana na Tanzania Piloting Center 👇👇
1: Private Pilot Licence (PPL);
hii ni leseni ya chini katika urubani. Ili upate leseni hii lazima uwe na masaa ya kuwa angani 40 (flying hours). Leseni hii inakuruhusu kuongoza ndege ambayo si abiria. Yaani ni wewe na familia yako na jamaa zako ndani ya ndege.
Kwa hapa Tanzania, pale airport kuna mzungu anafundisha leseni hii kwa zaidi ya mli. 35 Tsh. Nilisikia NIT walitaka kuanzisha course ya urubani sijui waliishia wapi....Kwa pale JK Nyerere Tanzania Piloting Center nilijaribu kufanya application mwaka 2018 wakanitumia hizi gharama
2:Commrcial Pilot Licence (CPL); Hii ni leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za kukodiwa lakini si abiri.Lakini pia ukiwa na leseni unaweza kuajiliwa kwenye kampuni ya ndege kama Co-pilot wakati ukifukuzia masaa.Chuo cha Soroti flying school kinatoa mafunzo ya leseni hii kwa $62k
Hii leseni ni lazima uwe na m careasaa ya angani 200. Kwa mfano yule mzungu pale airport JNIA anatoza saa moja 200 USD. Ukiipata leseni hii unaweza ajiriwa sasa kama rubani kamili....
Gharama kamilj za hii CPL pale Tanzania Piloting Center ni kama ifuatavyo
3: Airline Transport Pilot Licence (ATPL); Hii ndo leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za abiria. Na ili upate leseni lazima uwe na masaa yasiyopungua 1000.Lakini uzuri wa leseni utafikisha hayo masaa ukiwa ni Co-pilot ilimradi upate sehemu ya kujishikisha.
Baada ya kupata hizo lesseni unaweza kuwa rubani rasmi sasa kurusha ndege tofauti tofauti....
Kunakua na Instrumental rating sasa pale unapotaka kusoma kurusha ndege aina tofauti japo basics mnakua mmefanya huko mwanzoni
Moja ya marubani wachanga katika tasnia hii ni David Matoya....Nenda istagram utampata kwa Pilot pears...Amemaliza mafunzo yake ya urubani yaani CPL nchini Africa kusini ukiwa na maswali waweza kwenda kumuulizaa
Leo Tumjue Mnyama Nyegere
RT iwafikie wengi
Ongezea unalojua zaidi
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani.
Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula.
Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea.
Ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake,hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike,hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike
FURSA YA KILIMO CHA NYOKA
Achana connection za ifm njoo connection hii...
Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo chenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.
Sumu ya nyoka inatumik kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake
Gram moja ya "snake venom" kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25K
Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka
1.Zingatia hali ya joto na hewa.
Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29°C nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku
MASKINI & TAJIRI:-
1.Maskini hudhani utajiri ni bahati,tajiri hudhani umaskini hutokana na uvivu na uzembe. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake,tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.
2.Tajiri bila masikini ni maskini lakini maskini bila tajiri ni tajiri.Umaskini ni matokeo ya fursa zote ambazo hazikutumika kwa usahihi,utajiri ni jumla ya fursa zote zilizotumika kwa usahihi
3.Maskini huwaza kulima mchicha,tajiri huwaza kulima miti ya mbao.Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa,tajiri huamini atapata pesa kupitia pesa za wengine.Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa,tajiri hudhani maskini ana tabia ya kuombaomba.
MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE NI BABA WA TAIFA LA TANZANIA.
Kuelekea Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa .Tujue machache kumhusu
1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama na kufariki tarehe 14/10/1999 kule London. Ni Raisi wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
2.Ni Raisi wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo akiwa bado Raisi. 3.Ni kati ya Raisi aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani na pia raisi aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
4. Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Uingereza na Muafrika wa pili kupata Degree nje ya Afrika, akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.
Mambo Ya Msingi Unayopaswa Kufahamu Kuhusu Nidhamu Ya Pesa.
Ni bora tuwe wakweli katika somo linalohusu pesa kwani ndilo somo ambalo watu wengi hufeli sana hasa pale wanapozipata,wapo baadhi ya watu wakizipata pesa hujikuta hawana kitu au zimeisha pasipo kufanya mambo ya msingi
Wengi wao wamesahau ya kwamba pesa zina kanuni na misingi yake ambapo kila mwenye kuzihitaji ni lazima aweze kuzielewa kanuni hizo, na pia kanuni hizo ni lazima aendane na misingi pamoja na nidhamu ili ziweze kujizalisha.
Hivyo ili uweze kumiliki pesa unatakiwa kufahamu mambo haya ya msingi yahusuyo pesa kama ifuatavyo:-
1. Ongeza kiwango cha uzalishaji.
Ukitaka kuishi katika kiwango kizuri cha umiliki wa pesa unatakiwa kuzingatia misingi itayokusaidia wewe kuweza kuwa hivyo, na miongoni mwa