Kwenye interviews nyingi maswali huwa yanatafuta kujua ujuzi wako na uzoefu wako. Badala ya kukariri majibu ya maswali ambayo huulizwa mara kwa mara, jaribu kuelewa mbinu inayotumika mara nyingi kujibu maswali haya ambayo pia hujulikana kama "behavioral questions"
Maswali haya hutaka kujua namna ambavyo umewahi kukabiliana na changamoto na namna ambavyo unaweza kutatua changamoto nyinginezo huko mbeleni. Mbali na kudadisi ujuzi, huangalia kama una uzoefu. Njia hii kwa kifupi huitwa STAR - kifupi cha Situation, Tasks, Action & Results!
Situation/Hali - Fikiria hali inayofanana na swali, eleza namna ulivyofanya, weka taarifa mahsusi za tukio kama mahala, lini, nini n.k
Task/Jukumu - Ongelea jukumu ulilopewa kutatua changamoto hiyo. Eleza kwa kifupi na nyoosha maelezo. Elezea changamoto yoyote uliyokutana nayo
Action/Hatua - Elezea namna ulivyotatua tatizo/changamoto. Pia onesha stadi ambazo mwajiri angependa kuziona, uongozi, kujituma, ari na ushirikiano.
Results/Matokeo - Elezea matokeo na mchango wako katika kupata matokeo hayo. Ulijifunza nini? Nini matokeo ya hatua ulizochukua?
Maswali hutofautiana, lakini mara nyingi huangukia katika kutaka kujua namna unavyoshirikiana na wengine, uongozi, kutatua changamoto, uvumilivu. Kabla ya usahili, angalia kazi unayoomba na jiandae kwa kutumia njia ya STAR kwa kutazama stadi zinazotafutwa na kutoa mifano sahihi.
Zingatia - jiandae kwa kufanya utafiti wa kazi uliyoomba na kuandaa mifano 3-5 utakayotumia wakati wa usaili inayoonesha ujuzi na uzoefu wako, kuwa mkweli, usitunge stori, eleza stori yenye mafanikio/mafunzo. Unaweza kusoma zaidi hapa online.hbs.edu/blog/post/comm…
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh