Adam Anthony Profile picture
Executive Director at @HakiRasilimali working towards accountability and transparency in the extractive sector #LSEAlumni at @LSEPublicPolicy #CheveningScholar
Sep 15, 2020 6 tweets 2 min read
Kwenye interviews nyingi maswali huwa yanatafuta kujua ujuzi wako na uzoefu wako. Badala ya kukariri majibu ya maswali ambayo huulizwa mara kwa mara, jaribu kuelewa mbinu inayotumika mara nyingi kujibu maswali haya ambayo pia hujulikana kama "behavioral questions" Maswali haya hutaka kujua namna ambavyo umewahi kukabiliana na changamoto na namna ambavyo unaweza kutatua changamoto nyinginezo huko mbeleni. Mbali na kudadisi ujuzi, huangalia kama una uzoefu. Njia hii kwa kifupi huitwa STAR - kifupi cha Situation, Tasks, Action & Results!