Zahoro Muhaji Profile picture
Oct 9, 2021 31 tweets 8 min read Read on X
Karibuni kwenye #ElimikaWikiendi na leo nitakielezea kwa ufupi kitabu cha A knight in Africa, ambacho kimeandikwa na Sir Andy Chande akielezea historia ya maisha yake kutokea kuzaliwa mpaka uzee wake. Kitabu hiki kina chapters 13 na utangulizi wake, uliandikwa na Rais Mkapa. Image
Chapeter 1: BUKENE HOMETOWN AND CHILDHOOD.

Sir Andy Chande alizaliwa Mombasa Tarehe 7, May, 1928, ila wazazi wake walikua wakiishi Bukene, Tabora. Licha ya kuzaliwa tarehe 7-5-1928, cheti chake kinaonyesha kazaliwa tarehe 17-8-1929. Hivyo ana birthday 2, kama Malkia Elizabeth!
Baba yake Sir Chande, alitokea India Gujarat, na alipande meli mwaka 1919 kuja Tanzania kutafuta maisha. Akaenda mpaka Bukene ambapo ni kituo kikubwa cha treni kuanza biashara. Sir Chande alisoma elimu ya msingi huko Bukene, shule ya wahindi tupu. #ElimikaWikiendi
Chapter 2: SCHOOL DAYS:

Alipomaliza elimu ya msingi, wakahamia Tabora mjini na akaanza sekondari. Anasema Tabora alikuta wanaishi kwa matabaka. Wazungu ni watawala, wahindi ni watumishi wa serikali na biashara, waarabu biashara na weusi wakulima na vibarua.#ElimikaWikiendi
Mama yake Sir Chande akafariki ghafla, hivyo ikamlazimu yeye kupelekwa Mjini Dar, kuishi na mjomba wake. Alivyofika akajiunga na shule ya sekondari ya wahindi watupu, ambayo kwasasa inaitwa Tambaza. Anasema Dar ndio ushamba ukamtoka, akawajua 'mademu' na bia #ElimikaWikiendi
Baada ya masomo ya kidato cha nne, akapelekwa India kusoma high school. Huko anasema ilikua shule ya ghali na kimataifa na ndio iliyomjengea connection ya kupata marafiki dunia nzima. Baadae akajiunga na chuo kikuu, ila baba yake akamuambia aache chuo arudi kusimamia biashara.
Chapter 3: FAMILY BUSINESS.

Alivyorudi Sir Chande, alikuta biashara za baba yake zimetanuka sana na kwasasa wamehamia Dar, ambapo walikua na kiwanda kikubwa cha kusaga mahindi(kile cha Tazara kwa Bakheressa) na pia wao ndio walikua exporters wakubwa wa Kahawa. Pia waliuza pamba
Kinyume na matarajio yake, akaambiwa hawezi kuanza kua bosi hapa Dar, arudi kijijini akaanzie kujifunza kusimamia biashara chini kabisa. Baada ya miezi kadhaa ndio akarudishwa Dar kufanya biashara na baba yake. Hapo ndio alipokutana na Dossa Aziz na John Rupia #ElimikaWikiendi
Anasema aliiva kwenye biashara mapema na mpaka akafikia kuteuliwa kua mwenyekiti wa @CEOrtTZ ambae wa kwanza kua sio mzungu. Tofauti na baba yake aliyekua mtu wa dini, yeye alikua mtu wa starehe na kujichanganya, kitu kilichomfanya ajuane na kujulikana na watu . #ElimikaWikiendi
Baba yake aliugua kansa, na waliazimia kumpeleka marekani kwa matibabu lakini baba aligoma na kuishia Nairobi, ambapo alirudi Tz na kufariki hapa, mwaka 1959. Biashara rasmi zikabaki mikononi mwa Sir Andy Chande. Familia yake ikamshauri aoe, na akatafutiwa mchumba huko Uganda.
Chapter 4: MARRIAGE,my beautiful Jayli.

Anasema walipofika Uganda kumuona mchumba, alipata uoga maana familia ya mwanamke ilikua ya kitajiri sana wakimiliki kiwanda cha sukari na binti mwenyewe alikua na miaka 16 lakini tayari anaendesha gari. Ila familia ikamkomalia aoe.
Familia ya Sir Chande ikajikaza wakakodi ndege nzima, enzi hizo East African Airways, wakaenda kuoa Uganda. Wakarejea Tanganyika kuanza maisha na wakapata mtoto wao wa kwanza mwaka 1959. #ElimikaWikiendi
Chapter 5: TANGANYIKA SOVEREIGNTY.

Kufikia miaka ya 1950, vuguvugu la uchaguzi lilikua limepamba moto. Serikali ya kikoloni iliitisha uchaguzi, wakigawa viti 10 kwa weusi, 10 wahindi na 10 wazungu. TANU wakasema wagomee uchaguzi wakiona hata wakishinda vyote vyao 10, bado watazi
watazidiwa na wahindi na wazungu ambao jumla watakua na viti 20. TANU ilijaa wahafidhina ambao walichukia wahindi na wazungu, hivyo walibishana siku nne, mpaka kupeleka chama kugawanyika! Wale wenye msimamo mkali wakajitenga na kuunda chama chai ANC, wakiongozwa na Zuberi Mtemvu
Wenye msimamo wa wastani kama Julius Nyerere waliendelea na TANU na wakashiriki uchaguzi wakashinda viti vyao, lakini pia walisapoti baadhi ya wagombea wa kihindi na wazungu kushinda viti vyao hivyo bungeni wakawa na wingi. Hatimae serikali ya kikoloni ikakubali kuwapa TANU nchi
Chapter 6: NYERERE AND TANZANIA.

Sir Chande anasema baada ya Uhuru, liliendelea vuguvugu la kutaka wafanyakazi wazungu na wahindi wafukuzwe serikalini na kazi zao wapewe wazawa(weusi). Mwl Nyerere alipinga sana hilo wazo hata kufikia kijiuzulu Uwaziri Mkuu. #ElimikaWikiendi
Mwaka 1963, kulitokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi ya kutaka kumtoa mwalimu madarakani, lakini uasi huo wa jeshi ulizimwa na majeshi kutoka Uingereza na Nigeria. Mwl Nyerere alipenda kumtumia Sir Chande kwenye shughuli za maendeleo, akaanza kumteua uenyekiti wa bodi za umma.
Aliteuliwa kua Mwenyekiti wa shirika la Air Tanzania, Bandari pamoja na bodi ya maendeleo ya Elimu ya mkoa wa Dar, ambapo aliwezesha kujengwa shule ya viziwi pale Buguruni, pia shule ya Shaaban Robert na kusaidia ujenzi wa shule zingine. #ElimikaWikiendi
Sir Chande pia alikua mshauri wa ujenzi wa reli ya Tazara, pia alitumwa na serikali kwenda kuongea na Dr. Leakey arudishe fuvu la Zinjathropus, ambapo ilihitajika pesa nyingi, na alipowaambia serikali, ikamjibu azitafute anapojua wao hawana. Akaomba michango fuvu likarudi.
Chapter 7: THE CHALLENGE OF NATiONALISATION:

Mwaka 1967, February azimio la Arusha likachapishwa. Siku 4 baadae Sir Chande akaitwa Wizara ya Biashara. Alipofika, aliwakuta wafanyabiashara wengine wakubwa wenzie 8 wenye biashara ya viwanda vya usagaji nafaka. #ElimikaWikiendi
Wakakaribishwa na Waziri wa biashara, Mhe. Abdulrahman Babu. Mhe. Babu, akawasalimia na kuwapa ujumbe wao. "Kuanzia leo serikali imetaifisha viwanda vyenu na mtapewa fidia zenu" ilimchukua Babu chini ya dakika moja, mali ambazo wamezihangaikia kwa miaka 40, ziliondoka ghafla!
Anasema hawakuruhusiwa kuuliza maswali, tayari serikali ilishaamua kuchukua viwanda vyao. Sir Chande anasema aliporudi, ofisini kwake kiwandani Tazara, akakuta tayari kuna askari wenye silaha wamezingira kiwanda kuashiria rasmi ile ni milki ya umma.
Sir Chande hakua na mali binafsi kila kitu alichokua nacho aliwekeza kwenye kampuni, ikiwemo nyumba na gari lake. Navyo vigageuka mali ya serikali, akajikuta ghafla amekua masikini anayetegemea marafiki wamchangie fedha aweze kuishi. Anasema alisaidiwa zaidi na shemeji zake.
Aliomba kwenda kuongea na Mwalimu Nyerere kuhusu uamuzi huu na alipofika ikulu akamuambia "Nahisi umefanya kosa kubwa sana kwa uchumi wa Tanzania kwa uamuzi huu, historia itahukumu kati yangu na wewe nani yuko sahihi" mwl akamuambia achana na historia, sema kama unataka kazi.
Sir Chande akaomba kazi ya kuajiriwa serikalini kuendesha biashara zake zile zile ambazo serikali imezichukua, na Mwalimu akamkubalia. Rasmi akaajiriwa kama CEO wa shirika ambalo lilikua lake mwenyewe. #ElimikaWikiendi
Chapter 8: AND WINES AND BREAD AND BOXES.

Sir Chande akaendelea na kazi kwenye shirika sasa likiitwa NMC, lakini anasema wanasiasa walikua wakiingilia uendeshaji na kuvuruga biashara. Waziri wa kilimo wakati huo Bryson(mzungu alikua) aliamua kushusha bei ya mchele.
Bila ya kumtaarifu. Ikapelekea demand ya mchele kuongezeka na mchele kua hautoshi na shirika kupata hasara sababu walikua wanauza bei ya chini tofauti na gharama. Serikali ikaamua sasa inataka Tz itengeneze wine(mvinyo) kazi hiyo akapewa tena Sir Chande. #ElimikaWikiendi
Anasema akalazimika kwenda kumuomba msaada Balozi wa Ufaransa na wa Italy wakamsaidia utaalamu na mafunzo kwa Watanzania, na hatimae wakaanza kutengeneza wine. #ElimikaWikiendi
Chapter 9: AND NEWSPAPERS

Sir Chande aliteuliwa kua mwenyekiti wa bodi ya kampuni binafsi inaitwa the Standard Group, iliyokua ikichapisha magazeti kadhaa. Alipoteuliwa, akaamua kugawa kampuni hiyo kwenye kampuni 4 tofauti, moja ya kumiliki mitambo ya uchapaji, nyingine
Magazeti yenyewe, nyingine mali zingine etc. Anasema siku moja Waziri, Paul Bomani alimuita na kumuambia serikali imeamua kutaifisha kampuni hiyo, akamuambia lakini pale tunazo 4 tofauti, Bomani akamuambia kua watachukua zote! Ndio serikali wakazitaifisha na kumteua
Benjamin Mkapa kama mhariri mkuu, wa Daily News na Reginard Mengi akiteuliwa mwenyekiti wa Bodi. #ElimikaWikiendi

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Zahoro Muhaji

Zahoro Muhaji Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(