Zahoro Muhaji Profile picture
Ordinary person. Among the founders and CEO for @TanzaniaSA. My mantra “There is a World out there”
Oct 9, 2021 31 tweets 8 min read
Karibuni kwenye #ElimikaWikiendi na leo nitakielezea kwa ufupi kitabu cha A knight in Africa, ambacho kimeandikwa na Sir Andy Chande akielezea historia ya maisha yake kutokea kuzaliwa mpaka uzee wake. Kitabu hiki kina chapters 13 na utangulizi wake, uliandikwa na Rais Mkapa. Image Chapeter 1: BUKENE HOMETOWN AND CHILDHOOD.

Sir Andy Chande alizaliwa Mombasa Tarehe 7, May, 1928, ila wazazi wake walikua wakiishi Bukene, Tabora. Licha ya kuzaliwa tarehe 7-5-1928, cheti chake kinaonyesha kazaliwa tarehe 17-8-1929. Hivyo ana birthday 2, kama Malkia Elizabeth!