Habibu B. Anga Profile picture
Oct 14, 2021 β€’ 98 tweets β€’ 25 min read β€’ Read on X
π—•π—œπ—‘π—§π—œ π—π—”π—¦π—¨π—¦π—œ π—ͺ𝗔 π— π—œπ—”π—žπ—” 25 π—”π—‘π—”π—¬π—˜π—œπ—§π—œπ—žπ—œπ—¦π—” 𝗔𝗙π—₯π—œπ—žπ—” 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔π—₯π—œπ—žπ—œ

Thread..

Siku ya 30 May 2019, maafisa Usalama Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA, Nairobi walimuweka kizuizini abiria mmoja mwenye hati ya kusafiria ya kidiplomasia, mwanaume.. Image
wa asili ya kisomali. Japokuwa watu wenye diplomatic passport wapata exemptions kadhaa kwenye kaguzi za uwanja wa ndege, lakini ilikuwa ni lazima kwa maafisa hawa kumuhoji abiria huyu kutokana na utata wa mzigo ambao alikuwa nao.

Huyu somo alikuwa na briefcase ambalo ndani yake
alikuwa amebeba fedha cash dola za Kimarekani milioni moja na nusu.

Mtu huyu nyaraka zake zilikuwa zinaonyesha kwamba alikuwa safarini kuelekea nchini Ethiopia.

Maafisa hawa wa Usalama. Wakaanza kumuhoji abiria huyu sababu za kusafiri na kiwango kikubwa hivyo cha fedha na pia.. Image
dhumuni la safari yake ya Ethiopia.

Lakini badala ya abiria huyu kuwajibu, akawaeleza maafisa wa Usalama kwamba anahitaji kuzungumza na wakili wake anayeitwa Ahmed Adan.

Huyu Ahmed Adan ni wakili maarufu sana pale Kenya. Ni msomali ambaye amezaliwa pale pale Kenya
Licha ya kuwa
ni wakili, huyu Adan (maarufu kwa jina la "Dere") pia ni ndugu wa Rais wa sasa wa Somalia, Mohamed Abdullah.
Pia huyu Dere anasemekana yuko Kenya kusimamia mali ambazo Rais wa Somalia amezificha hapo Kenya.

Hivyo, huyu bwana Dere ni ndugu na pia msiri wa karibu sana wa Rais wa..
Somalia.

Sasa, baada ya kuitwa hapo uwanja wa ndege, Dere akawaeleza wale maafisa usalama, kuhusu yule abiria ambaye walikuwa wanamshikilia.

Yule bwana jina lake halisi anaitwa Abdulla Kulane (nchini Somalia wananchi wamembatiza jina la utani la "Jiis Marihan"). Huyu somo ni.. Image
Mkurugenzi wa Oparesheni wa Idara ya Kijasusi ya Somalia, NISA.

Hii ilikuwa inashitua zaidi. Kwamba kigogo wa Idara ya Ujasusi ya nchi jirani alikuwa anataka kuvuka mpaka kwenda Ethiopia akiwa na kiwango kikubwa hivyo cha fedha, kuna nini? Anapeleka wapi fedha? Kwa dhumuni gani? Image
Ili kuepuka mgogoro wa kidiplomasia, serikali ya Kenya ikamkatalia Jasusi "Jiis Marihan" kuvuka mpaka na badala yake wakamrudisha kwao Somalia.

Lakini katika duru za masuala ya intelijensia Afrika Mashariki, tukio hili lilizua maswali mengi sana.

Kuna jambo gani la siri baina..
ya Somalia na Ethiopia

Kama wafuatilia hali ya usalama kwenye huu ukanda wetu basi utaona kwamba kwenye miaka miwili mpaka mitatu iliyopita hali imekuwa ya hafadhali kiasi (kabla ya miezi sita iliyopita.. Kabla ya Tigray na hali ya sintofahamu ya Somalia miezi michache iliyopita
Kwa ujumla hali ya usalama imekuwa ya afadhali sana. Somalia kwenyewe kumetulia kwa kiasi kikubwa hata wameweza kufanya uchaguzi na transition ya serikali kwa utulivu. Vivyo hivyo Congo, DRC.
Pia Kundi la Al Shabab limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa na kupokwa udhibiti wa Mogadishu Image
Bado tuna changamoto za hapa na pale lakini kwa ujumla hali imekuwa ya afadhali sana kiusalama.

Lakini katika muda wa miezi sita hali hii yote ya utulivu kiusalama imekuja kubomoka kwa matukio kadhaa.. kwa mfano, vita inayoendelea Tigray pamoja na hali ya sintofahamu iliyoibuka
nchini Somali.

Na huyu binti Jasusi ninayetaka kumueleza hapa, ana nafasi kwenye matukio yote haya mawili.

Namna gani,

Moja ya Msomali mashuhuri sana anaitwa "Sanbalolshe" (Abdullahi Mohamed Ali). Huyu bwana mpaka kufikia mwaka 2018 ndiye alikuwa bosi wa Idara ya Ujasusi ya.. Image
Somalia, NISA.

Kipindi fulani mwaka 2017 akiwa bado ni Mkurugenzi wa NISA, Sanbalolshe alitembelea ofisi ya Meya wa jiji la Mogadishu.
Akiwa hapo kwenye ofisi ya Meya, Sanbalolshe akavutiwa sana na utendaji kazi wa Katibu Kiongozi wa Meya. Katibu huyo kiongozi alikuwa ni binti
mdogo tu wa miaka 20 kipindi hicho.

Alivutiwa zaidi na zaidi baada ya kusikia historia ya binti huyo

Kwamba familia ya binti huyo ni Wasomali waliolowea nchini Ubelgiji kwa miaka mingi. Kwa hivyo hata masomo yake, binti huyu alikuwa amesomea nchini Ubelgiji na baadae chuo kikuu
Binti huyo alisoma nchini Uingereza ambapo alikuwa amehitimu kwenye fani ya masuala ya mifumo ya kompyuta na tehama.

Baada ya kumaliza tu masomo yake ya chuo kikuu, binti huyo aliwaambia wazazi wake kwamba anataka kurejea nchini kwao Somalia ili akaitumikie nchi yake kuwa kama.. Image
sehemu za juhudi za nchi hiyo kujikomboa toka kwenye umasikini.

Yaani kwamba binti huyo alikuwa tayari kuacha ajira nono Ulaya, maisha mazuri na badala yake akaja Somalia ambako kuna kila aina ya hatari, ili tu aje kuisadia nchi yake kwa ujuzi wake.

Jasusi Sanbalolshe...
akasuuzwa roho haswa na uzalendo wa binti huyu.

Uzuri ni kwamba kipindi hiki idara ya Ujasusi ya Somalia ilikuwa iko kwenye mchakato wa kuundwa na kusukwa upya mchakato ambao ulikuwa umeanza tangu mwaka 2013.
Kwa muda wa miaka 20 Somalia haikuwa na Idara ya Ujasusi tangu kufutwa
kwa Idara ya Ujasusi ya zamani, NSS mwaka 1990.
Ndipo mwaka 2013 kwa msaada mkubwa wa CIA serikali ya Somalia wakasaidiwa na Marekani kuunda idara mpya ya Ujasusi.
Kwa hiyo mpaka mwaka huo 2017 bado idara hii ilikuwa iko kwenye mpito wa kuundwa upya.

Hivyo Sanbalolshe aliposikia Image
historia ya huyu binti anayefanyakazi ofisini kwa Meya.. uzalendo wake huo ukamvutia na kuamua kum-recruit na kumuingiza NISA.

Binti huyu jina lake anaitwa Ikran Tahlil Farrah.

Binti Ikran akapatiwa mafunzo stahiki kwa miezi tisa mpaka kuiva na kisha akawa Jasusi rasmi, Afisa..
wa Intelijensia Idara ya NISA akipangiwa majukumu yake kwenye kitengo cha Cyber Security.

Kutokana na Uzalendo na Uchapakazi, Ikran akapanda ngazi haraka kwenye kitengo mpaka kufikia kuwa moja ya wakuu kwenye kitengo cha Usalama wa Kimtandao ndani ya Idara ya Ujasusi ya NISA...
Sasa, idara ya NISA inafanyakazi kwa ukaribu mno na Jeshi la Somalia.
Kwa mfano, ndani ya idara kuna kitengo kinaitwa "Gaashaan" ambacho kinahusika na Counterterrorism. Hii Gaashaan ina "Alpha Group" na "Bravo Group".. Alpha Group ina wanajeshi 40 na maafisa 3 ambao wote wametoka Image
kwenye special force ya jeshi la Somalia.

Najaribu kuonyesha kwamba Idara ya NISA na jeshi la Somalia utendaji wao kazi ni wa karibu mno mno.
Kwa hiyo hata taarifa nyingi za jeshi la Somalia zina-flow kupitia NISA.

Sasa, mwishoni mwa mwaka jana, huyu binti Jasusi, Ikran Tahlil
aligundua kwamba kulikuwa na kiasi kikubwa cha 'inconsistencies' katika taarifa za jeshi la Somalia kuhusu wanajeshi wake hasa wanajeshi wapya wanaojiunga.

Yaani Kwamba hakukuwa na uwiano kati ya vijana ambao walikuwa wanajiunga na jeshi na wale ambao wanahitimu na kupewa ajira Image
Yaani ukikokotoa wanajeshi ambao wamekuwa wanajiunga jeshi, Ukatoa ambao hawakuhitimu/walifukuzwa/kufa, unapata kwamba kulikuwa na kiwango kikubwa cha wanajeshi walikuwa hawaonekani kwenye hesabu.
Yaani hawajafa, hawajariwa, hawajafukuzwa lakini hawajulikani huwa wanakwenda wapi.
Baadae namalizia huu Uzi

Nimeandika Kitabu kuchambua masuala ya Ujasusi, Intelijensia na Matukio ya Uhalifu hapa Tanzania, Afrika Mashariki na Dunia.
NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI
Kitabu kina kurasa 442 na utakipata kwa 50,000/-
Nipigie au sms 0759 181 457 kupata nakala. ImageImage
Tumalizie mkasa huu..

𝗣𝗔π—₯𝗧 𝗧π—ͺ𝗒

Sasa, baada ya Binti Ikran kuona hii sintofahamu kuhusu baadhi ya vijana wa Jeshi kutojulikana wanakwenda wapi akaanza kufanya uchunguzi wake kimya kimya. Hiyo ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka jana.

Ajabu ni kwamba, kadiri ambavyo alikuwa.. Image
anachimba kwenye uchunguzi wake huu akabaini kwamba idadi ya vijana wanaojiunga na jeshi ambao wakishajiunga tu hatma yao baada ya hapo haijulikani huwa wanakwenda wapi ilikuwa inaongezeka

Yaani kwamba vijana wengi zaidi jeshini walikuwa wanapotelea kusikojulikana kadiri ambavyo
siku zilikuwa zinakwenda.

Ikran akahisi kwamba hii si bahati mbaya, kuna jambo la siri lilikuwa linaendelea.

Jambo ambalo Ikran akaja kuligundua lilikuwa ni zito na hakuna ambaye alidhani linaweza kufanywa na serikali.

Wakumbuka pale juu mwanzoni kabisa nilieleza kuhusu...
kukamatwa kwa jasusi nguli, Mkuu wa kitengo cha Oparesheni za Idara ya NISA, shushushu "Jiis Marihan" kwenye uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya akiwa na kiasi cha USD 1.5 Millions.??

Sasa, jambo ambalo lilikuwa linafanyika ni kwamba.. Rais wa Somalia Muhamed Abdullahi alikuwa Image
analipa rushwa kwa majenerali wa jeshi la Ethiopia ili wasogeze majeshi yao kwenye majimbo ya Jubaland na Dhusamareb ili kubadili upepo wa uchaguzi ambao ulikuwa unafanyika mwaka jana.

Nchi ya Somalia namna wanavyofanya uchaguzi ni tofauti na uchaguzu wa mahala kokote duniani..
Uchaguzi wao uko complex haswa kwa mtu wa nje kuuelewa.
Wananchi huwa hawapigi kura kuchagua wabunge wala Rais au Waziri Mkuu.
Kama umesoma makala yangu ya Operation Gothic Serpent nimeeleza namna gani pale Somalia Koo zina nguvu kuliko hata serikali.
Wasomali wana koo kubwa tano
Hawiye,Β Dir,Β Darod,Β IsaaqΒ naΒ Rahan eyn. (Kuna koo kadhaa ndogo ndogo upande wa kusini ambazo hazina nguvu sana).

Sasa, Wazee kutoka kwenye hizi koo ndio wanaochagua Wabunge na madiwani (sio wananchi.. bali wazee wa ukoo).
Kisha Wabunge hawa pamoja na Wazee wanachagua Rais na... Image
Waziri Mkuu.

Kwa hiyo kwa uchaguzi wao pale Somalia unafuata mfumo complex wa namna hiyo.

Sasa huyu Rais aliyeko sasa madarakani, muhula wake ulishaisha tangu mwezi February mwaka huu.
Mwaka jana tarehe 01 December kulipaswa kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge. Kisha february..
Wabunge wamchague Rais.
Lakini uchaguzi wa Wabunge mwezi desemba mwaka jana haukufanyika kwa hivyo hata uchaguzi wa Rais february mwaka huu nao haukufanyika.

Sarakasi hizi za kutofanyika uchaguzi zinatokana na woga wa Rais kutokana na ushawishi wake kupotea kabisa. Na ndio maana
Rais Mohamed Abdullahi alikuwa anatumia majeshi ya Ethiopia ku-intimidate viongozi wa Jubaland na Dhusamareb ili kubadili upepo wa uchaguzi

Ndio sababu ya yule Jasusi aliyekamatwa Nairobi akiwa mafwedha akitaka kwenda Ethiopia kuhonga Majenerali wa jeshi

Sasa,

Twafahamu kwamba Image
Mapema mwaka huu pale Ethiopia kukatokea machafuko kati ya majeshi ya serikali dhidi ya vikosi vinavyoegemea siasa za jimbo la Tigray.

Ni kwenye kipindi hiki pia ndipo ambapo yule msichana niliyemueleza, Ikran Tahlil akagundua kupotea kwa maelfu ya vijana wanaojiunga na jeshi...
Kwenda kusikojulikana.

Baada ya kasi ya vijana hawa wa jeshi kupotea kuwa kubwa sana, Ikran naye akaongeza juhudi zake za kufuatilia.
Baada ya muda akaanza kuunganisha nukta. Akaanza kupata mwanga wa nini ambacho kilukuwa kinatokea.

Kwa bahati mbaya sana, Ikran akafanya kosa..
kubwa la kwenda kumshirikisha taarifa hii bosi wake, chief spy wa idara ya NISA, Mkurugenzi Fahad Yasin (pale Somalia kwenye duru za masuala ya usalama huwa wanamuita jina la utani "Mr. Fix it")

Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana, sababu serikali ya Somalia kuna "project" ya siri Image
ambayo walikuwa wanaiendesha kinyume na sheria. Na ilikuwa ni mwiko kwa mtu mwingine yeyote kufahamu isipokuwa watu wachache mno waliomo kwenye 'cycle' inayohusika na hii project.

Mkurugenzi Fahad Yasin akamjibu Ikran kwamba, vijana hao wa jeshi aliogundua kwamba hawapo kwenye..
Data base, baadhi yao walikuwa wanapelekwa nchini Eritrea kwa ajili ya mafunzo 'advanced' ya weledi wa jeshi na baadhi yao wengine walikuwa wanapelekwa nchini Qatar na kuajiriwa kwenye kampuni fulani ya ulinzi ambayo ilikuwa na mkataba wa siri na jeshi la Somalia.
Akamsisitiza... Image
Kwamba suala hilo (hasa la wanajeshi kuajiriwa Qatar) linavunja sheria fulani za kimataifa na ndio maana serikali wamelifanya siri. Lakini vijana hao wanajiingizia kipato kizuri huko Qatar kwa faida yao na familia zao.

Hili lilikuwa ni jawabu tamu sana, kakini lilikuwa la uongo.
Na Ikran alihisi kabisa kuna vitu ambavyo Boss wake bado alikuwa anamficha.
Kwa hivyo akaendelea kulichimba zaidi suala hili.

Ikran alikuwa ni shushushu aliyeiva haswa, kwa hiyo baada ya muda akavumbua ukweli nini ilikuwa hatma ya maelfu ya vijana wale ambao hawakuwa wanaonekana
kwenye database.

Ukweli wenyewe ambao aliuvumbua ulikuwa unatisha haswa. Ulikuwa ni mzito kuzidi kifua chake. Lilikuwa ni jambo la hatari haswa kumzidi kimo chake.
Ikran akabakia kwenye bumbuwazi asijue afanyie nini siri nzito hiyo aliyoivumbua.
Ndipo akapata wazo, kwamba sababu Image
suala hili ni zito mno kwake, basi amshirikishe mtu mzito haswa ambaye atakuwa na misuli ya ushawishi na weledi wa kuifanyiakazi taarifa hii (kosa kubwa la pili akalifanya).

Ikran akafanya kikao cha siri na Jasusi Sanbalolshe.. unamkumbuka? Yule somo ambaye alim-recruit kipindi
anafanyakazi ofisini kwa Meya wa Mogadishu na kumuingiza idara ya NISA. Naam yule Mkurugenzi mstaafu wa idara ya Ujasusi ya NISA

Akakutana naye kwa siri na kumpa taarifa yote kuhusu kupotea kwa utata kwa maelfu ya vijana wanaojiunga na jeshi na ni nini alichogundua kuhusu hatma Image
ya vijana hao.

Hili lilikuwa ni kosa kubwa kwake sababu jambo ambalo Ikran hakuwa akijua ni kwamba tangu siku ile ya kwanza alipokwenda kumuuliza bosi wake Fahad "Mr. Fix it" kuhusu suala hilo, Fahad alikuwa amemuwekea vijana wa "kumfunga mkia", walikuwa wanafuatilia nyendo zake
zote. Kila sehemu anayotembelea na kila mtu ambaye alikuwa anaongea naye.
Kwa hiyo kikao chake hiki cha siri na 'role model' wake Sanbalolshe taarifa zilimfikia "Mr. Fix it".

Ubaya ni kwamba Sanbalolshe ana uadui mkubwa sana na Rais Mohamed Abdullahi ndio sababu hata akamuondoa
kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa NISA na kumuweka "Mr. Fix it".
Huyu "Mr. Fix it" (Fahad) ni mshirika wa karibu sana wa Rais Mohamed Abdullahi, na yeye ndiye alikuwa meneja wake kampeni kipindi cha uchaguzi, na baada ya kuupata Urais akamtunuku Fahad Ukurugenzi wa NISA.

Kwa hiyo.. Image
Ikran bila kujijua alikuwa anahamisha siri nzito toka kambi moja kwenda kambi nyingine. Na hivyo usalama wa siri hiyo ulikuwa matatani.

Sasa, huyu Ikran alikuwa anaishi kwenye kota za idara ya NISA. Yaani kwamba pale Mogadishu, NISA wana eneo kubwa sana ambalo upande mmoja... Image
unatumiwa kama majengo ya ofisi na upande mwingine wamejenga kota za maafisa wao kuishi.

Sasa, siku moja tu baada ya Ikran kuonana na Sanbalolshe, siku hiyo akiwa anatembea kutoka ofisini kwenda nyumbani.. ghafla ilitokea gari isiyo na namba na kufunga breki kwa nguvu mbele yake
𝐏𝐀𝐑𝐓 3

Ile gari ambayo ilisimama ghafla mbele ya Ikran, kwa haraka wakashuka watu wawili wanaume. Wakaongea nae maneno machache na kisha wakamtutusa kwa nguvu na kumtupia ndani ya gari
Kisha gari ikang'olewa kwa kasi na kutokomea
Na hii ndio ilikuwa mara ya mwisho kuonekana Image
kwa Binti Jasusi Ikran Tahlil Farah.

Kwenye siku za kwanza zilipopita hakuna ambaye alikuwa anajua nini kilikuwa kimetokea. Lakini zilipopita karibia siku nne pasipo Ikran kuonekana ndugu na marafiki zake wakaanza kuuliza ofisini kwao kuhusu mahala alipo Ikran.

Wiki moja baadae
kelele zikawa nyingi zaidi mpaka kufika kwenye vyombo vya habari watu wakihoji shushushu huyu binti amepotelea wapi?

Ndipo ikabidi NISA watoe taarifa rasmi na kueleza umma kwamba wako kwenye uchunguzi kuweza kubaini afisa wao huyo amepotelwa wapi ghafla.

Siku kadhaa baadae...
NISA wakawasilisha kwa umma kuhusu matokeo ya uchunguzi wao juu ya kupotea kwa shushushu Ikran.

Kwenye hii ripoti yao kwa ufupi walidai kwamba, kwa intelijensia ambayo wameikusanya, wamebaini kwamba kundi la Al-Shabab ndilo limehusika kumteka Ikran na kwa mujibu wa intelijensia Image
yao kuna uwezekano wamemuua na kuutupa mwili wake mahala pasipojulikana.

Siku ambayo NISA waliwasilisha ripoti yao hii nchi nzima ya Somalia ilikuwa kama imelipuka moto kwa hasira.
Wananchi walikasirishwa kuona kwamba NISA kuna jambo walikuwa wanalificha. Kuna masuala kadhaa...
kwenye hii ripoti yao yalikuwa hayaingii akilini

Kwa mfano,

Pale Somalia moja ya maeneo salama zaidi na yenye ulinzi mkali ni hili eneo lenye Makao Makuu ya NISA pamoja na kota za maafisa wake.

Chukua mfano kwenye ofisi za idara yetu Oysterbay, tuifanye ndio compound ya NISA.. Image
Kwanza ukitota tu barabara kubwa Ally Hassan Mwinyi ukunje pale St. Peter's unakutana na check point hapo barabarani. Unakaguliwa vitambulisho na usalama wa chombo chako cha usafiri.
Ukiruhusiwa mbele kabisa kwenye geti la kuingia kwenye compound kuna check point ya pili. Hapo...
Utajieleza kuhusu nani unaenda kuonana naye. Wataangalia kama una ruhusa ya kuingia, appointment, vitambulisho n.k.
Baada ya hapo ndio waingia kwenye compound ya NISA. Na ukitaka kuingia sasa kwenye jengo lenyewe la ofisi kuna sehemu ya kukaguliwa metal detectors, begi, na upewe Image
beji ya kuvaa uingie ndani.

Na eneo lote la hii coumpound limetapakaa maafisa wanaopiga doria wakiwa na silaha.

Sasa, kwenye ripoti yao NISA walikuwa wanapiga chenga hawaelezi kinaga ubaga namna gani Ikran alitekwa. Kwenye mazingira yapi. Hata footage ya CCTV camera walikataa.. Image
kuweka hadharani. Bahati nzuri kuna maafisa wazalendo wa NISA wakavujisha hiyo footage.

Ukiitizama hiyo footage, Ikran anaonekana yuko ndani kabisa ya compound ya NISA upande wa kota za makazi. Hiyo gari isiyo na plate number ilikuja kumteka tokea hapo.

Sasa, swali laja.. gari Image
hii ilipitaje check point zote zile za ukaguzi?
Walijieleza wao ni akina nani na wamekuja NISA kufanya nini? Kwa nini, ripoti ya NISA haielezi watu hao waliruhusiwa kuingia kama akina nani na kwa nini? Kama walijitambulusha kwa majina ya uongo kwa nini NISA hawayasemi majina hayo
ili watu waanze kuunga nukta
Na kwa nini gari isiyo na plate number iruhusiwe kuingua sehemu nyeti kama hiyo?

Mbaya zaidi, siku moja tu baada ya NISA kutoa ripoti yao, kundi la Al-Shabab likajitokeza na kukana kuhusika kumteka binti Ikran.
Kwa kawaida matukio kama haya Al-Shabab
huwa ni wepesi kujitokeza na kuchukua credit kwamba wao wamehusika ili waendelee kuogopwa. Lakini kwenye tukio hili walikana kabisa kuhusika.

Tukio la Ikran lilikuwa limewaunganisha Wasomali. Historia yake namna alivyoacha maisha yenye kheri barani Ulaya na kurejea Somalia ili.. Image
kusaidia nchi yake, ilifanya aonekane shujaa kwa watu wa milengo yote.

Kwa hivyo mpira ukarudi tena kwa NISA na serikali.. wananchi wakachachamaa na kuwanyooshea kidole kwamba wao ndio wahusika wa kupotezwa kwa Ikran.
Familia ya Ikran nayo ikaja juu, wakaanza kufanya mahojiano.. Image
na vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa nao wakiitaka serikali waseme ukweli kuhusu alipo mtoto wao na wamrejeshe eidha akiwa hai au mwili wake wauzike.

Moto ukiwa unawaka kwa nguvu namna hii, Jasusi Sanbalolshe akajitokeza kwa mara ya kwanza na kuongea.

Sanbalolshe...
akawapa NISA siku tatu kumrejesha Ikran la sivyo atamwaga mboga kueleza ni kwa nini binti huyo amepotezwa.

Sanbalolshe ni jabari pale Somalia. Ni aina ya watu ambao wakiongea nchi inasimama kumsikiliza.

Kwa hiyo hii kauli yake ikafanya watu wote nchi nzima wainue masikio... Image
kusubiri wasikie mwamba huyu ana jambo gani la kusema.

Siku tatu alizotoa zikapita.

Sanbalolshe akarejea tena kwenye vyombo vya habari na kuanza kueleza mkasa mzima

Akaeleza namna gani ambavyo alim-recruit Ikran na kumuingiza NISA.
Kisha akaanza kueleza namna ambavyo kuanzia..
mwaka jana, Ikran alianza kugundua mkanganyiko wa kupotea kwa utata kwa taarifa za vijana ambao walikuwa wanajiunga na jeshi.
Akaeleza namna ambavyo Ikran akaripoti sintofahamu hii kwa mabosi zake lakini akapewa jawabu la kisanii kwamba vijana hao wanapelekwa arabuni nchini Qatar Image
kuajiriwa kwenye kampuni za ulinzi.

Sanbalolshe akaeleza namna ambavyo Ikran hakuridhishwa na jawabu hilo na akaamua kuchimba zaidi.
Na alipopata ukweli kuhusu hatma ya vijana hao, ndipo akamfuata yeye na kumpa hiyo taarifa ili wajue wanafanya nini

Hapo ndipo ambapo Sanbalolshe
akamwaga mboga na kutoa siri nzito ambayo ilifanya serikali ya Somalia kupitia idara yake ya Ujasusi kumpoteza Ikran.

Sanbalolshe akaeleza kwamba, Ikran aligundua kwamba kulikuwa na maelfu ya vijana mara tu wakimaliza mafunzo ya jeshi walikuwa wanaahidiwa kupelekwa nchini Qatar Image
kuajiriwa kwenye makampuni binafsi.
Lakini vijana hawa walikuwa wanadanganywa ili tu wakubali kuondoka Somalia na badala yake kulikuwa na programu ya siri na hatari inafanywa na kikundi cha watu fulani ndani ya serikali ya Somalia.

Kwamba, serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia...
Abiy Ahmed walikuwa wanalipa mamilioni ya dola kwa kikundi cha watu ndani ya serikali ya Somalia ili vijana wale waingizwe nchini Eritrea na kupelekwa mpakani mwa Eritrea na jimbo la Tigray na kisha vijana hao walikuwa wanapigana vita front line dhidi ya vikosi vya Tigray kwa.. Image
niaba ya serikali ya Ethiopia.

Kikundi hicho ndani ya serikali ya Somalia ambacho kilikuwa kinahusika na project hii ya hatari, walikuwa wanafanya hivi kwa ajili ya malipo hayo ya mamilioni ya madola lakini pia kama kulipa fadhila kwa Ethiopia namna ambavyo nao huwa wanawasaidia
Kwa kupeleka majeshi yake Jubaland na Dhusamareb ku-intimidate wazee wa ukoo ili kubadili upepo wa uchaguzi (nilieleza mwanzoni).

Sanbalolshe akaeleza zaidi kwamba, kutokana na suala hili lilikuwa linafanyika kinyume na sheria za nchi na sheria za kimataifa na lilikuwa linavunja Image
haki za kibinadamu. Maelfu ya vijana ambao walikuwa wanakufa huko vitani Tigray walikuwa wanazikwa kwa siri kama mizoga huko huko Ethiopia na kisha taarifa zao zote jeshini zinapotezwa ili kuficha ushahidi

Somalia yote ilizizima kwa mshituko baada ya Sanbalolshe kumwaga siri hii
π…πˆππ€π‹π„

Mshituko ulikuwa mkubwa wananchi waliposikia kwamba vijana wao wanakufa kwenye vita isiyowahusu kwenye ardhi ya ugenini kinyume na sheria. Vijana wanakufa kwenye ardhi ya kigeni kwa manufaa ya kikundi fulani ndani ya serikali.

Mamia wakajitokeza kutoa shuhuda namna Image
gani ambavyo wamepoteza mawasiliano na watoto wao mara tu baada ya kuhitimu mafunzo ya jeshi, na namna gani kwa miezi mingi wamekuwa wakifuatilia jeshini kujua waliko ndugu zao na hawakuwahi kupewa majibu ya maana.

Kwa hiyo hii skandali ndio kama ikaibua hasira za ndugu hawa...
kutema nyongo zao.

Maandamano yakaibuka pale Mogadishu kuishinikiza serikali iseme alipo Ikran na pia kupinga kitendo cha serikali kufanya project ya siri ya kupeleka vijana wa kisomali kwenye vita ya Tigray.

Sasa,

Mwishoni mwa mwaka jana kutokana na serikali kushindwa kuandaa Image
Uchaguzi, Bunge lilimfuta kazi Waziri Mkuu wa Somalia.
Akateuliwa Waziri Mkuu wa mpito Bw. Mahdi Gulaid na baadae Rais akamteua Waziri Mkuu rasmi anayeitwa Mohamed Hussein Roble.

Huyu Roble ni sura ngeni kwenye siasa za Somalia, hakuwa akijulikana kabisa.
Watu wengi walihisi...
Kwamba Rais alikuwa ameteua sura ngeni kama Roble ili amfanye kuwa kibaraka wake wa kukubali kila jambo lake.
Lakini ndani ya muda mfupi Roble, msomi wa fani ya uhandisi toka nchini Sweden, baada ya kuapishwa tu akaanza kutema cheche kwa kumchachafya Rais wake.

Roble alikuwa... Image
anampinga Rais wake wazi wazi kwa kitendo chake cha kuendelea kuwepo madarakani licha ya muhula wake kuisha tangu mwezi February

Kwa hiyo kwa miezi kadhaa sasa, Waziri Mkuu Roble na Rais wake wamekuwa si watu wenye kuiva kwenye chungu kimoja. Kumekuwa na uhasama mkubwa baina yao
Sasa, baada ya kutokea sekeseke hili la kupotea kwa binti Shushushu Ikran, na dalili zote kuonyesha kwamba serikali kupitia NISA wamehusika kwenye kupotea kwa shushushu huyo.. Waziri Mkuu Roble akaingilia kati.

Akamfuta kazi Mkurugenzi Mkuu wa Idara wa NISA yule "Mr. Fix it"... Image
ambaye ni swahiba wa kushibana wa Rais.
Pia akamfuta kazi jasusi "Jiis Marihan" ambaye alikuwa ni mkuu wa kitengo cha Oparesheni za NISA.

Waziri Mkuu akaeleza kwamba Mkurugenzi wa NISA ameshindwa kuonyesha nia ya dhati ya kufanya uchunguzi wa weledi kuhusu kupotea kwa afisa wa.. Image
Idara hivyo ni vyema akae pembeni ili uchunguzi ufanyika.

Pia akaeleza "Jiis Marihan" anamfuta kazi sababu shutuma zinaonyesha kwamba yeye ndiye aliyeagiza watu wa kufuatilia nyendo za Ikran na baadae kutoa amri ya kumteka.
Hivyo naye anapaswa kukaa pembeni kupisha uchunguzi..
Hii lilikuwa ni pigo chungu kwa Rais Abdullahi maana watu wote wawili hawa walikuwa ndio washirika wake wa karibu kwenye masuala yake.

Siku moja tu baada Waziri Mkuu kuwafuta kazi "Mr. Fix it" na "Jiis Marihan", Rais Abdullahi alijitokeza na kusema kwamba kitendo kilichofanywa.. Image
na Waziri Mkuu ni kinyume na Katiba sababu Waziri Mkuu hana mamlaka ya kuteua au kumfuta kazi Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi.
Kwa hiyo akabatilisha maagizo ya Waziri Mkuu na kumtaka "Mr. Fix it" na "Jiis Marihan" kuendelea na majukumu yao.

Lakini kesho yake, Waziri Mkuu Roble...
naye akajibu mapigo.

Akamweleza Rais kwamba, ni yeye Rais ndiye hana mamlaka kikatiba kuteua Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi sababu madaraka yake ya Urais yalishakoma tangu mwezi February. Kwa hivyo nchi hiyo sasa ni kama haina Rais, na kwenye ombwe la namna hiyo ni Waziri Mkuu.. Image
ambaye anashika hatamu. Hivyo akakazia maamuzi yake kwamba akiwa kama Waziri Mkuu, ambaye kwa sasa ndiye mwenye mamlaka kikatiba kufanya maamuzi ya mwisho ya mustakabali wa nchi kutokana na nchi kuwa na Rais aliye Ikulu kama "kinyago cha mpapure" tu bali mamlaka yake yalishakoma
akasisitiza kwamba "Mr. Fix it" na mwenzake "Jiis Marihan" hawaruhusiwi kuonekana kwenye ofisi za NISA.
Na kuonyesha msisitizo akamteua Brigedia Jenerali Bashir Mohamed JamaΒ (maarufu kwa jina la "Goobe") kuwa Mkurugenzi mpya wa Idara ya NISA.

Uzuri Bunge la Somalia lote likawa.. Image
nyuma ya Waziri Mkuu. Wakaunga mkono maaamuzi yake ya kuwafuta kazi MkurugeNzi Mkuu wa NISA na Mkuu wa kitengo cha Oparesheni ili kupisha uchunguzi huru juu ya kupotea kwa Shushushu Ikran Tahlil.

Kutokana na kuzidiwa kete kwa kitendo cha Bunge kuthibitisha, kufutwa kazi kwa...
maswahiba zake "Mr. Fix it" na "Jiis Marihan", Rais Abdullahi akamteua "Mr. Fix it" kuwa Mshauri wake wa Masuala Usalama (National Security Adviser).

Tangu hapo mpaka leo hii Somalia imengia kwenye mkwamo wa kiutawala.
Rais na Waziri Mkuu wake hawazungumzi wala kushirikiana kwa Image
jambo lolote la kiungozi.

Wazazi na ndugu wa maelfu ya vijana waliojiunga na jeshi na baadae kupelekwa kwa siri kupigana vita Tigray kila uchwao wanaandamana kutaka haki itendeke ili hatma ya ndugu zao ijulikane.

Hata Waziri Mkuu wa Ethiopi Abiy Ahmed amechafuka damu na taswira
yake kwenye jumuiya ya kimataifa licha ya kupewa tuzo ya Nobel juzi tu kutokana na tuhuma hizi kwamba serikali yake inalipa hela kwa kikundi cha watu ndani serikali ya Somalia ili vijana wao wakapigane front line na kufa Tigray kinyume na sheria na haki za binadamu.

UN pamoja na Image
AU wametoa matamko kuishinikiza serikali ya Somalia, mosi kutoa taarifa kamili ni wapi alipo shushushu Ikran Tahlil, na pia kufanya uchunguzi wa taarifa ambayo Ikran alikuwa anaifanyia kazi kuhusu vijana wa Kisomali wanaopelekwa Tigray kupigana vita kinyume na sheria za kimataifa
Serikali ya Somalia nayo iko kwenye mpasuko.
Waziri Mkuu na Rais wamegeuka chui na paka na inatishia hata juhudi za uchuguzi ambao unapaswa kufanyika mwezi ujao.

Kama hali itaendelea namma hii, kuna dalili ya Somalia kurejea tena kwenye hali ya vurugu na vita ya wenyewe kwa...
wenyewe ambayo tumewahi kushuhudia kwenye miaka ya nyuma.

Kama hilo litatokea, basi hii itakuwa ni hasara kubwa na kudorora kwa hali ya kiusalama kwa Ukanda wote wa Afrika Mashariki.
Twafahamu kile kinachoendelea kusini mwa nchi yetu Tz. Twafahamu kuhusu mashambulizi yanayotokea Image
mara kwa mara nchini Kenya. Twafahamu pia hali tete ya kiusalama Kaskazini mwa Uganda miaka kadhaa iliyopita.
Ili hali iwe shwari kwenye maeneo yote haya inategemea mno uwepo wa utulivu na serikali imara ndani ya nchi ya Somalia

Na ndio maana nasema kwamba sekeseke la Binti huyu Image
Jasusi Ikran Tahlil Farah linaitikisa Afrika Mashariki yote hii.

Tunaendelea kufuatilia mkasa huu kadiri unavyojiri na tutaudadavua hapa.

Until next time.. thank you for reading na tukutane tena kwenye makala nyingine.

Asante.

Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond

β€’ β€’ β€’

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
γ€€

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

Mar 25, 2023
Ukitaka kuelewa chanzo cha vita ya Ukraine basi unapaswa kufahamu mkasa wa huyu unaye muona pichani na Zitto… anaitwa Victor Yushchenko

Miaka kadhaa iliyopita huyu somo alikumbwa na kadhia ya kulishwa sumu na kupata madhara kama yale ambayo yalimkuta Dr. Mwakyembe..

Thread..
enzi zile za Richmond na Dowans mpaka akapelekwa India kutibiwa.
Ngozi ya mwili yote iliharibika na kuanza kupukutika kama unga

Huyu Yuschenko yeye kadhia hii ilimtokea mwaka 2004 kipindi hicho akiwa anagombea Urais wa Ukraine
Yushchenko alikuwa anachuana mwanasiasa Yanukovych..
ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu wa serikali ambayo ilikuwa inamaliza muda wake

Uchaguzi huu wa Ukraine kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni mchuano wa kiushawishi kati Marekani na Urusi wakitunishiana misuli.
Marekani walikuwa wanamuunga mkono huyu somo pichani Bw. Yushchenko wakati Urusi
Read 24 tweets
Aug 18, 2022
Roman Abramovich: Utajiri wa Damu Mpaka Kumuingiza Ikulu Putin

Thread,

Namna ambavyo mtoto yatima aliyelelewa katka umaskini ameweza kuibuka moja ya binadamu wenye ukwasi mkubwa duniani na mpaka kuweza kumuingiza Ikulu Vladmir Putin ni mkasa wa aina yake…

(Usisahu ku-Retweet) Image
Wazazi wake wote wawili licha ya kuishi maisha yao yote nchini Russian lakini asili yao ni Waisrael. Mama yake aliitwa Irina na alifariki kipindi Roman bado angali mchanga kabisa wakati baba yake ambaye aliitwa Arkady alifariki kwa ajali ya gari miaka michache baadae Roman akiwa
bado mtoto mdogo kabisa.

Hii ndio ilikuwa sababu ya Roman kwenda kulelewa kwa ndugu zake Komi kaskazini mwa Urusi ambako kuna baridi kali na umasikini uliokithiri

Ujanani mwake, Roman aliwahi kujiunga na jeshi kabla ya kuacha na kuamua kwenda Moscow kutafuta maisha
Akiwa Moscow
Read 23 tweets
Dec 21, 2021
TUMEWAHI KUWA NA CHANJO KWA MALENGO YA KISHUSHUSHU

Thread..

Kadiri ulimwengu unavyobadilika, stadi ya Ujasusi inazidi kuwa complex kwa kuhusisha mbinu ambazo nyingine ukizisikia unaweza kudhani labda watazama sinema au waota, lakini ndio uhalisia wa ulimwengu ulipo sasa katika
katika juhudi za mataifa na makampuni makubwa kupanua ushawishi wao juu ya dunia yote na kulinda maslahi.

Kuna kisa cha tofauti sana ningependa nikijadili leo hii. Kisa cha tofauti kabisa..

Wengi tutakuwa tumewahi kusikia shirika linaloitwa β€œSave the Children”. Ni moja ya…
Shirila kubwa zaidi la misaada ya kibinadamu ulimwenguni ambalo limejikita hasa kwenye kutoa misaada inayolenga kuboresha hali za maisha ya watoto wadogo.

Mwaka 2011 shirika hili lilikuwa kwenye shughuli zake mahala paitwa Khyber nchini Pakistan.
Save the Children walikuwa na…
Read 43 tweets
Sep 4, 2021
π—žπ—”π—•π—Ÿπ—” 𝗬𝗔 π—œπ—žπ—¨π—Ÿπ—¨.. π—žπ—ͺ𝗔𝗑𝗭𝗔 𝗔𝗗𝗛𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 π—žπ—œπ—™π—’

Thread..

Ukiwa unatoka Lusaka kwenda Jimbo la Magharibi, kabla hujaingia mji wa Mongu kuna kipande cha barabara kinajulikana kama Limulunga Road.
Kipande hiki cha barabara mwaka juzi kimetupa tukio la kipekee Image
ambalo kwa kiwango kikubwa tukio hili limebadili mwelekeo wa siasa la bara zima la Afrika na hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Pengine pasipo tukio hili huyu Hichilema tunayemuona leo asingelikuwa Rais. Lilikuwa tukio la kipekee kabisa..

Kila mwaka pale Zambia huwa wana
sherehe maarufu zinaitwa "Kuomboka Ceremony".
Wenzetu mpaka leo hii bado wanatambua cheo cha asili cha "Litunga" ambaye ni Mfalme wa kabila la Walozi.
Kila mwaka mwishoni mwa msimu wa mvua mfalme huwa anahama kutoka makazi yake ya bondeni ya Lealui na kuhamia makazi yake yaliyo..
Read 41 tweets
Aug 10, 2021
π—¨π—§π—”π—π—œπ—₯π—œ π—ͺ𝗔 π— π—”π—¦π—›π—”π—žπ—” π—ͺ𝗔 π—ͺπ—”π—Ÿπ—œπ—‘π—­π—œ π—ͺ𝗔 π—©π—œπ—’π—‘π—šπ—’π—­π—œ

Thread..

Mwaka juzi kwenye hafla ya mapokezi ya ndege kwenye nchi fulani hivi hapa Afrika Mashariki kuna incident ndogo tu ilitokea lakini wengi ikatufikirisha sana.

Dakika chache baada ya Rais wa...
nchi hiyo kumaliza kuongoza hafla hiyo ya mapokezi ya ndege akashuka jukwaani na akianza kuandoka.
Lakini kabla hajakwenda kupanda gari, kama ambavyo ilikuwa ada kwa Rais yule akaelekea upande waliokaa wananchi wake na ili awasalimie.
Na kusalimia huku akaanza jukwaa ambalo...
walikuwa wamekaa wageni VIP.

Wageni wale mashuhuri wakasimama na Rais akawa anapita akiwapa mkono.

Mojawapo ya wageni wale mashuhuri alikuwa ni mfanyabiashara maarufu sana mwenye asili ya kihindi.
Rais alipopita mbele yake, mfabiashara huyu akanyoosha mkono ili asalimiane na...
Read 25 tweets
Jul 20, 2021
UZI
πŸ‘‡πŸ‘‡

Tujadili kidogo Executive Protection.
Hapa chini nimeweka picha za inner cycle za ulinzi wa Rais JPM, Samia, Ndayishimiye (Burundi) na Mnangagwa (Zim).

Kwa kila Rais utaona 'First Ring' zao (hao walinzi wanaomzunguka Rais muda wote) lazima kuna afisa mmoja au wawili..
amebeba begi la mkononi

Umewahi kujiuliza hilo begi lina dhumuni gani.?

Hiyo picha hapo juu, JPM alikuwa chato na hapo alikuwa anakwenda kwenye kibanda cha simu kusajili line yake kwa alama ya vidole
Kwa hiyo hakuwa kwenye ziara au anakwenda kikaoni.. sasa hilo begi ni la nini?
Na si yeye tu.. siku ukibahatika kuwa mahala ambako Rais SSH yupo, tazama kwa makini wale walinzi wake, hasa ile 'first ring', wale walinzi wenye suti wanaomzunguka.. utaona vivyo hivyo pia, kuna maafisa wawili au watatu wana mabegi ya dizaini hii wamebeba mkononi.
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(