Fortunatus Buyobe Profile picture
Jan 14, 2022 47 tweets 13 min read Read on X
In Every Crime,there is always a trail of evidence that is left behind.

Fatilia mkasa huu wa mauaji ya kutisha yaliyotokana na kifo cha mtu mmoja tu.

"A CHAIN OF MURDER CRIMES"

UZI👇

#simulizizabuyobe
Usiku wa manane kuamkia 26 july 2013,ndugu WILLY MUSHI ONESMO anapigwa risasi na kufariki akiwa kazini
WILLY MUSHI ONESMO alikuwa ni mfanyakazi wa mgodi wa madini TANZANITE ONE huko MIRERANI Simanjiro. Kulikuwa kuna tabia ya wachimbaji wadogo wanaouzunguka mgodi huo,kuingia chini kwa chini na kwenda kuiba madini mgodi wa Tanzanite(Wenyewe wanaita "MTOBOZANO" au "KUTEKA NJIA")
Siku ya tukio bwana WILLY ONESMO MUSHI akiwa na wafanyakazi wenzake KENEDY na LEONARD walishuka shimoni kufanya patroal ndipo akakutana na wateka njia ambapo alifyatuliwa risasi kifuani na kufikwa na mauti.(inasemekana aliombwa "suruhu wayamalize" akakataa).
Baada ya kifo cha ONESMO wafanyakazi wa TANZANITE ONE wakafanya mgomo hatua zichukuliwe kwa waliohusika huku TETESI zikimtaja mmiliki wa mgodi wa jirani bwana JOSEPH DISMAS MWAKIPESILE aka CHUSA kuhusika na sakata hilo.
Kufuatia mgomo huo na madai hayo,Serikali,iliifunga migodi minne inayozunguka mgodi wa Tanzanite one hali iliyoibua tena maandamano ya wachimbaji wadogo mkoani Manyara chini ya chama chao cha MAREMA. Kwa ufupi Kifo cha WILLIAM ONESMO kilizua balaa.
Tarehe 29 July 2013,ONESMO akazikwa kijijini kwao USWAA MACHAME,wilayani HAI.
Kufuatia makelele mengi yaliyotaka haki itendeke,aliyetuhumiwa kwa mauaji hayo JOSEPH DISMAS MWAKIPESILE aka CHUSA akakamatwa na kushikiliwa gereza la BABATI na baadaye HOSPITALI YA MLALE chini ya ulinz
Haikupita hata wiki tangu CHUSA akamatwe,huko mtaani Arusha "kikaumana" tena..

Mchana wa jua kali "in a broad daylight", mfanyabiashara mwingine wa madini "akapokonywa uhai".

Si mwingine bali ni ERASTO MSUYA. Tukio hili likazaa kesi Maarufu kwa jina la "BILIONEA MSUYA"
Msuya anasemwa alirithishwa mgodi na baba yake ambao haukumtoa kivilee, baadae akapiga "MAWE YA LEMAKOO"(watu wa chuga tu ndo watanielewa). Mawe ya LEMAKOO yakamfanya afingue SG PREMIUM RESORT HOTEL. Baadaye MAWE YA BOMU ndio yakampa heshima Arusha nzima.
Bilionea Msuya alisemekana kuwa karibu sana na mfanyakazi wa TANZANITE ONE aliyeuwawa(WILLIAM ONESMO MUSHI) ambaye alikuwa anamuuzia madini kutoka mgodi anaofanyia kazi. Madini haya ya deal yaliitwa "MAWE YA BOMU".
Sasa kuuwawa kwa ONESMO lilikuwa pigo kwa MASUYA. Ilinong'onwa,Washindani wa MSUYA hawakupenda kitendo cha ONESMO kuwa anamuuzia MSUYA peke yake MAWE YA BOMU.
Kibaya zaidi,wao "WAKITEKA NJIA"(kuingia kisiri chini kwa chini kutoka migodi yao hadi TANZANITE ONE) wakikutana na ONESMO kwenye "MTOBOZANO" anakuwa hataki kusomeshwa.
Kiufupi MSUYA alinasa kwenye mtego wa kuitwa akauziwe madini katika eneo la MJORORONI barabara ya Arusha na Moshi. Akawasha RANGE ROVER VOGUE na kuishia kupigwa risasi.(Biashara zilikuwa na usiri mkubwa hasa kwenye transaction) ndio maana zilikutwa pesa nyingi eneo la tukio.
Baada ya Mauaji haya tuhuma zikamwandama tena bwana "CHUSA"(alikuwa bado yuko mahabusu babati), kuwa kuna mkono wake hapa. Polisi waliendelea na upelelezi na hazikupita siku nyingi wakawa wanadaka muhusika mmoja mmoja.Pongezi ni kwa RPC wa Arusha kipindi hicho Bw. BOAZ
Wapelelezi waoianzia kwenye eneo la tukio ambapo waliokota Jacket moja lililotelekezwa na wauaji na pia walikuta simu mbili za marehemu. Kwa kutumia watu wa cybercrime waligundua SMS mbili za mwisho alizotumiwa marehemu zingewaongoza ktk upelelezi wao.
Walikuta ujumbe uliotumwa kwa marehemu tarehe 6 August 2013(siku moja kabla ya kuuwawa) ulisema "NINA RIZIKI" na pia ujumbe mwingine kutoka namba hiyohiyo ya Airtel ulituma tarehe 7 August 2013(Siku ya tukio) ulisema "NIPO KIA NAKUSUBIRI HAPA"
Polisi wakawaandikia barua Airtel kutaka kujua taarifa za mmiliki wa namba hiyo ambapo walibaini line hiyo ilisajiliwa siku nne kabla ya tukio kwa jina la MOTII MONGILULU. Wakaulizia wakala aliyesajili wakaambiwa ni wakala aliyepo Kituo cha mabasi Arusha.
Wakala alipofatwa alimtaja kijana wa kimasai aitwaye ADAM LEYANI alipohojowa alisema alitumwa na MUSA MANGUNGU(mshtakiwa wa

tatu)asajaili line NNE za Airtel. MANGUNGU alivyodakwa naye akamtaja mfanya biashara SHARIF MOHAMED(mshtakiwa wa kwanza) kuwa ndio alimwagiza.
Washtakiwa hawa wakabanwa na wakawataja watu wengine wanne akiwemo CHUSA. Kumbukeni hayo yote yanafanyika kati ya August na September 2013.
Kwa kufuata mtiriko wa maelezo ya UNGAMO yaliyowasilishwa mahakamani kama ushaidi wa Jamuhuri,hivi ndio mambo yalivyokuwa.
1.Mshatakiwa wa kwanza SHARIFU MOHAMED alienda gereza la BABATI kumsalimia CHUSA ambaye alikuwa anashikiliwa kwa kesi ya mauaji ya ONESMO
CHUSA akamtaka asimamie na kugharamia biashara zake machimboni. Baadae chusa akamwambia kwa sauti ya chini "Unajua kama MSUYA ndio sababu ya mateso yangu haya?Yeye ndio kahonga nipewe hii kesi".

CHUSA akamwambia inabidi SHARIFU amsaidie kumwondoa MSUYA.
SHARIFU akapigwa butwaa! SHARIF anasema alimkatalia kwa kumwambia yeye hana ugomvi na MSUYA na hata kama angekuwa na ugomvi asingeweza kufanya kitendo hicho.CHUSA akamwambia kama hawezi basi akitoka atafanya mwenyewe.
Mara ya pili SHARIFU akaenda kumwona CHUSA aliyekuwa kalazwa chini ya ulinzi hospitali ya MLALE na akamuuliza alitaka aifanyeje kazi hiyo? Akamjibu afadhili tu pesa na akitoka atamlipa. CHUSA akamwambia aonane na SHAIBU JUMANNE aka MREDII aliyekuwa katoka jela BABATI karibuni tu
SHARIF na SHAHIBU JUMANNE MREDII walikutana town kisha wakaongozana tena kwa CHUSA ili athibitishe kama kweli ndio huyo muhusika. CHUSA akasema "NI YEYE"(in TID's voice🤣🤣) basi jamaa wakarudi Arusha ambapo walikutana na watu wengine watatu kwa ajili ya mpango kazi
Wakanunua pikipiki mbili, na wakaenda kukodi siraha kwa shilingi millioni 4 mpakani NAMANGA na wakaipata kesho yake.(vikao vya mkakati vilifanyikia SHAMOO GUEST HOUSE iliyokuwa inamilikiwa na mtuhumiwa wa kwanza SHARIFU.
Sharifu alitoa jiwe moja la TANZANITE ili litumike kama chambo ndipo mshtakiwa aliyejulikana kwa jina la ALLY aka MAJESHI akamtumia sms MSUYA ikidai "NINA RIZIKI" msuya akajaa na MAJESHI akamvuta mpaka KIA amvapo Mshitakiwa aliyetajwa kwa jina la KARIM akammimia MSUYA" risasi 22
Jamuhuri ilileta mashaidi zaidi ya 32(wa kuongea na wa maandishi) upande wa utetezi uliteteqa na wanasheria wanne akiwemo MAJURA MAGAFU. Mashaidi wengi ushahidi wao ulipanguliwa. Nakumbuka mabishano ya kisheria lilipoletwa KOTI lililopatikana tukioni ka kielelezo
Hoja ya KOTI iliibuka baada ya MKEMIA WA SERIKALI alivyotoa ushaidi jinsi alivyochukua vimelea vya jasho kwenye koti na kisha kuonisha na DNA za watuhumiwa waliokamatwa. Hoja ya utetezi ilisema haijulikani koti lilitoka wapi na limefikaje kwa shahidi(CHRONOLOGICAL HANDS)
Wakati kesi ikiendelea watu walishtuka pale mkurugenzi wa mashtaka DDP kwa kutumia mamlaka yake katika ibara 91 ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai(CPA) ya mwaka 2002 alisema hana nia ya kumshitaki CHUSA hivyo akatolewa kwenye orodha ya washtakiwa.
Uamuzi huo nahisi ulimshangaza hadi Jaji wa kesi hiyo SALMA MGHIMBI kwani wakati kusudio la kutokuwa na nia ya kumshitaki CHUSA ( NOLLE PROSEQUI) alitaka hivi; "DPP kwa sababu anazozijua yeye.... hana nia ya kumshitaki.... hivyo namfutia mashtaka"
Kesi ikazidi kuunguruma, huku washtakiwa wakianza kukataa viapo vya ungamo walivyotoa polisi huku wakijitetea walilazimishwa kwa mkono ubavu kukubali kilichoandikwa( Mmoja wa washtakiwa aliyekuja kuachiwa huru bwana MREDII anasema waliteswa sana kiasi kwamba yeye alihasiwa)
Mahakama iliwakuta hatiani washtakiwa watano na wawili waliachiwa huru. Kilichonichekesha ni kwamba kila mtuhu alikana kuwepo arusha siku ya tukio MREDII alidai alikuwa shamba BABATI,MANGU alikuwa singida anauguza akatoa hadi ticket ya MOHAMED TRANS,KARIM alikuwa anavuna karoti
Mshtakiwa wa tano SADIK JABIR aka MSUDAN anadai siku ya tukio yeye alikuwa dar baadae akaenda Kaliua Tabora akashangaa anakamatwa kijijini LIMBULA tarehe 13 sept 2013 akiwa anafanyiwa "DUA AFANIKIWE KIMAISHA" na Sheikh KHALID SANKAMULA.(polisi walidai kumkuta kwa SANGOMA🤣🤣)
Mshtakiwa wa tatu "MAJESHI" yeye alidai siku ya tukio alikuwa zake Honeymoon kijiji cha MAGUGU Babati mkoni Manyara baada ya kufunga ndoa na MWANAISHA JUMA tarehe 6 August 2019. Yaani kila mtu alikuwa anajaribu "KUTEMA NDOANO"
Pamoja na yote Jaji aliwakuta na hatia na wakahukumiwa kunyongwa hadi kifo. Baada ya kesi hii haikuwa mwisho wa MAUAJI kuiandama familia ya Bilionea MSUYA. Kwanza ukaibuka Mgogoro wa Mirathi.
Wisia wa marehemu ulisema akifa 40% iende kwa wazazi wake na 60% ibaki kwa mkewe kwa ajili ya wanae. Mke wa marehemu MIRIAM MRITA akaanza kutuhumiwa kuuza magari na viwanja kabla hata hawajaanua matanga.
Familia ya Msuya ikaenda na kufuli kufunga Hoteli na nyumba ya marehemu mgogoro ambao uliingiliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya wa Arumeru wakati huo @jerrymuro1980 na amuomba mama wa marehemu akafute shauri alilofungua mahakamani
Wakati haya yanaendelea kuna wakati dada wa marehemu ANTUJE MSUYA alimwagiwa tindikali akiwa amelala. Pia dada mwingine wa marehemu ESTER MSUYA akiwa na mumewe walishambuliwa kwa risasi maeneo ya HONGERA BAR SINZA. Funga kazi ikaja kwa mauaji ya dada mwingine ANETHE MSUYA
Anethe Msuya alikuwa ni mwajiliwa wa Wizara ya fedha kama mchumi daraja la pili, aliyekuwa akiishi na mwanae(Alen)KIBADA kigamboni.Siku moja kabla hajauwawa kinyama kwa kuchinjwa, mfanyakazi wake wa ndani alitoroka nyumbani ikabidi ANETHE aombe ruhusa ili kushughurikia hilo.
Akiwa nyumbani peke yake Ndipo wauaji waliingia na kutekeleza unyama na kuondoka bila kuchukua chochote. Mtoto wa marehemu ambaye bado alikuwa mdogo alitoka shule akawa anamwamsha mama yake bila mafaninio(kwa umri wake hakujua kama kama kachinjwa)
Mtoto alilala bila kula na asubuhi akaenda tena kumwamsha mama yake amvalishe nguzo za shule(alilala na za jana) na pia alisema njaa ilijuwa inamuuma. School bus ikaja ikapiga honi hadi ikaindoka. Mtoto akaenda kuomba kwa jirani wamsaidie kumwamsha mama yake.
Majirani walipofika wakapiga mayowe baada ya kumkuta ANETHE kwenye lindi la damu. Baadae wakaja polisi na baadae wakamkamata aliyekuwa mme wa ANETHE ambaye inasemekana juzi yake alienda na bodaboda akagonga lakini hakufunguliwa.
Baade kutokana na taarifa za kipelelezi, Mke wa marehemu MSUYA(MIRIAM MRITA) na mfanya biashara wa Arusha REVOCATUS EVARIST walikamatwa na kufikishwa mahakamani AUGUST 2016 huku aliyekuwa mme wa marehemu WILBARD KIMARIO akiachiwa baada ya kukosa ushaidi wa kutosha.
Kiufupi kesi hii bado inaendelea ingawa mke wa marehemu "AMEUNGAMA" kuwa alimkodi REVOCATUS EVARIST kutekeleza unyama huo kwa kuwa marehemu alikuwa akimdhihaki kwa kumtumia picha za wanawake vibonge wasio na shepu akiwafananisha na yeye.
Kuna mengi yanazungumzwa kuhusu mahusiano mabaya waliyokuwa nayo ANETHE na wifi yake kabla hata kaka yake hajafa. Yanayoelezwa ni mabaya na kwa kuwa hayajathibitishwa sina haki ya kuyaandika. Kwa kuwa shauli hili bado halijaisha naomba tuishie hapa tusije "KUINGILIA MUHIMILI"
MWISHO

Wameiba toolbox wamemwacha Fundi

Usiache kukanyaga follow @fbuyobe

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Fortunatus Buyobe

Fortunatus Buyobe Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @fbuyobe

Oct 7
Sometimes March 2013

Wakili Fatuma Karume alisafiri kutoka Dar kwenda mkoani Kilimanjaro.

Wakili huyu alikuwa amesafiri akiwa amebeba nyaraka furani ya muhimu.

Nyaraka ile alikuwa anaenda kumsomea na kumkabidhi mzee fulani aliyefahamika kwa jina la JumaImage
Actually, Mzee Juma naye alikuwa ni wakili ambaye sasa amestaafu akiwa amefanikiwa kurithisha taaluma hiyo pia kwa mwanae ambaye alikuja kuwa ni wakili maarufu sana mkoni Arusha.

Fatma hakujua kama nyaraka aliyobeba ingeleta taflani kubwa ndani ya familia ya Mzee Juma. Image
Fatma aliwasili nyumbani kwa ambako alikuta waombolezaji ambao walikusanyika baada ya kusambaa taarifa za msiba za mmoja wa watoto wa Mzee Juma.

Fatma alitegemea kuikuta hali hii nyumbani pale na hata safari yake ilitokana na yeye kupata taarifa hizi. Image
Read 40 tweets
Sep 17
Nimesikiliza hotuba ya leo ya mheshimiwa rais, na hii ndio analysis yangu.

1. Hotuba hii imekuja siku chache baada ya rais kuviagiza vyombo vyake vya ilinzi vimpelekee taarifa ya nini kilicho nyuma ya matukio ya utekaji na mauaji hasa baada ya kifo cha Ali Kibao
2. Inaonekana rais alipokea ripoti hii mapema kama alivyoagiza na yafuatayo ndiyo yalikuwa ndani ya ripoti hiyo:

(a)Kuwa haya yote anayoyasikia juu ya mauaji na utekaji, ni zao ya kikao cha siri kililichofanyikia Ngurero mkoani Arusha mnamo Sept 11, 2024
(b) Maazimio ya kikao kile yaliamua kutumia vibaya 4R alizoziasisi mheshimiwa rais ili kuzua ghasia nchini, kufitini jeshi la polisi na kufanya fujo misibani.

Kama ripoti hii ni sahii, kuna mambo yanayohitaji ufafanuzi..
Read 12 tweets
Sep 10
Satiiva ammedai kumtambua Mafwele kama mtu aliyeenda usiku kwa Land Cruiser kwenye karakana ya polisi Oysterbay alipotekwa

Kuwa ndiye mtu mwembamba, mkakamavu, aliyekuwa kavaa Jezi ya Simba na pensi

Amemtambua baada ya kuona picha ya Mafwele ikisambaa mtandaoni. Image
Pia Sativa ameshaujulisha uongozi wa Jeshi la polisi juu ya utayari wake wa kuhojiwa na jeshi hilo ili kuwashirikisha anachokifahamu nyuma ya kutekwa kwake.

Jeshi limemjibu likipata nafasi litamuita kumuhoji Image
Lakini ni jeshi hilihili, lilipata nafasi ya kunitumia timu ya makachero watatu, mmoja akiwa wa cheo kikubwa cha SACP, Mwingine akiwa ni katibu wa DCI, kusafiri kutoka makao makuu ya polisi Dodoma hadi Central DarEsSalaam kunihoji habari za ASP Fatuma Kigondo. Image
Read 7 tweets
Sep 10
Kifo cha Ali Kibao kimekuwa ni kama sauti ya wote waliokuwa wanabeza kuwa hakuna matendo ya utekaji na summary executions nchini.

Ni sauti iliyowasemea victims wote wa matendo haya.

Lakini pia kinaweza kuleta mwanga kwa kuwa sasa watu wameanza kugusia jambo fulani muhimu. Image
Jambo la kwanza kugusiwa ni dai la kuundwa kwa chombo huru kinachotakiwa kuufatilia utendaji wa jeshi la polisi.

Majirani zetu nchini Kenya wanacho chombo hiki kwa jina la IPOA

Independent Policing Oversight Authority

Nini umuhimu wa kuwa na chombo hiki? Image
Ni kwa sababu si rahisi kujichunguza kwa uhuru dhidi ya tuhuma unazotuhumiwa wewe mwenyewe.

Watu wanaojitambulisha kama askari polisi, ndio wanaotuhumiwa kwa utekaji na mauji hivyo haiwezekani hata kidogo chombo hiki kikaachwa kijichunguze chenyewe kisha tutarajie majibu chanya.

Image
Image
Image
Read 41 tweets
Sep 8
SECURITY TIPS TO HOOFMEN

Imeshathibitika kuwa, watu wanaojitambulisha kuwa ni askari wanaweza kumkamata mtu mbele ya watu, kuondoka naye na baadaye unakuja kupatikana mwili wake usio na uhai au asionekane kabisa.

Pia kwa kuwa @tanpol wameishia kutoa matamko bila suluhisho..
Yafuatayo ndiyo mambo tutakiwayo kufanya wote kwa pamoja ili kuokoa maisha ya wengine.

Kwani wakimaliza kwa huyo, wewe ndie utakayefata

1. Kataa kabisa kukamatwa kwa sasa hata kama utatolewa kitambulisho. Piga kelele zote uwezavyo, fanya fujo kwani upole wako hautakusaidia.
2. Kama mtu anakamatwa eneo la watu wengi, wengine saidieni kwa kuongeza fujo, kuhoji makosa yake na kuwarekodi kwa simu zenu wakamataji.

MSIOGOPE: Ni wao ndio wametufikisha kwenye ujeuri kwa ajili ya maisha yetu.

Wingi wenu dhidi ya uchache wao ni silaha tosha.
Read 11 tweets
Jul 31
Kuna kitu fulani wataalamu wa siasa hukiita "Political Paranoia"

Paranoia ni ugonjwa wa akili ambapo mgonjwa huwa na wasiwasi mkubwa kuwa kuna watu wanamfatilia mambo yake, wanapanga kibaya juu yake, wanamdanganya etc

UZI👇

CHOCHORO ZA MADARAKA -2 Image
Mgonjwa wa Paranoia mara nyingi hutuhumu watu fulani wana njama fulani dhidi yake.

Hata jambo fulani ambalo linaweza kutokea kwa bahati mbaya (just coincidence) ambavyo hata watu wengine huamini hivyo, lakini mgonjwa wa paranoia huamini si bahati mbaya bali makusudi. Image
Viongozi wengi barani Afrika, ni Paranoid.

Muda wote hutembea na hisia kuwa kundi fulani linakula njama za kuwatoa madarakani

Hii ndio maana unaona wengi wa viongozi hawa hupanga na kupangua safu za wasaidizi wao. Image
Read 21 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(