Wiki hii nilikuwa busy sana baada ya kufiwa na Jirani yangu ambaye tulikuwa na ukaribu sana.
Ilinibidi kwenda mpaka kijiji cha MBASA Ifakara kumzika jirani huyu.
Msiba huu umenifunza mengi..
Tuna familia za Kipumbavu sana sisi waafrika.
Nimethibitisha hili👇
Jirani yangu alifanikiwa kujenga mjini nyumba ya kawaida tu.
Lakini kwenye familia yao ndiye alikuwa mtu pekee aliyethubutu kufanya hivyo Mjini Dar
Jamaa ameacha watoto wawili wadogo na mkewe akiwa mjauzito.
Shida ilianza tangu Hospitalini Muhimbili
Wakati mkewe akidamka na ujauzito wake na kushinda hospitali, Familia ya mume ikawa inamsema kuwa hana msaada wowote kwa ndugu yao.
Mjane wa watu akaamua kuwaita wazazi wake wamsaidie kuuguza wajinga wakasema kajaza watu kwenye nyumba ya kaka yao.
Siku aliyofariki mmewe, jambo la kwanza ndugu wakampokonya simu ya marehemu mjane. Pia wakampokonya mjane simu aliyokuwa amenunuliwa na marehemu mumewe.
Bila soni mdogo wa marehemu ndiyo anatumia simu hiyo kwa amani kabisa.
Sasa tuendelee
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Lutueni Kanali E.A Sambila ambaye ndiye Commanding Officer wa 831 KJ anapokea taarifa nyeti ofisini kwake kutoka kwa askari wake wawili wahusikao na ulinzi amani kikosini (MPs)
Askari hawa wawili ambao ni P.12925 Captain Theresia Cylil Massawe na MT. 88710 Sergeant Mohammed Faki Haji walifika ofisini kwa Lt.Gen Msambila wakieleza kuwa wana taarifa ya dharula
Kuwa kuna uwezekano wa muda wowote amani kutoweka mle kikosini
Wakaruhusiwa kuingia
Taarifa inayotolewa mbele ya CO, inalazimu muda mfupi unaofuata, askari wale wawili, kwa maelekezo ya CO wavamie ofisini kwa serviceman MT. 85115 Sergeant Sahani
Askari yule anawekwa chini ya ulinzi, na kwenye upekuzi, wanachukua simu mbili anazomiliki
Tarehe 28 August 2025, chama tawala, CCM kilizindua kampeni zake za uchaguzi mkuu wa urais na wabunge katika viwanja vya Tanganyika packers
CCM walilazimika kutumia jukwaa hilo la uzinduzi wa kampeni kujibu mashambulizi kutoka kwa mwanachama wake mwandamizi Humphrey Polepole
Tangu kujiuzuru kwake July 13, mwaka huu kwa kile alichoeleza kama "kutoridhishwa na mienendo" ya serikali yake, balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Cuba, amekuwa akitoa tuhuma mbalimbali dhidi ya viongozi waandamizi wa chama chake na serikali
Polepole ameeleza juu ya uwepo wa kikundi anachokiita "CCM mtandao" ambacho huakikisha wanaohodhi madaraka ya rais
Kuwa mtandao huo nchini tangu mwaka 1995 zilipoanza siasa za vyama vingi na mtandao huu una agenda ya kuhakikisha kila rais anakuwa chini ya himaya yao
Mwaka 2012, Blandine Nyoni akiwa katibu mkuu wizara ya afya, alinukuliwa akitoa kauli tata ya kuwabeza madaktari kuwa "wanajiona bora wakati ni wachafu na hawajui kiingeleza"
Katibu huyu akaendelea kusema kuwa hata yeye alisoma mchepuo wa PCB na kufaulu vizuri tu lakini kwa kutambua ubovu wa Medicine mzazi wake akamsomesha Accounts so hajui madaktari wanalalamikia nini.
Kauli hii ikang'oa kilaka kwenye jeans ya bishoo!
Ni kwamba mwaka huo, madaktari walikuwa katikati ya mgomo wa kihistoria
Kauli hii ikawatibua madaktari wakalianzisha upyaaaaa
Wiki hii tumeshuudia waliokuwa wanachama wa Chadema wakitangaza kuachana na chama hicho huku wakiahidi kuelezea hatima zao za kisiasa siku za mbeleni
Kati ya waliohama ni waliowahi kuwa viongozi waandamizi wa chama hicho
Hii inamaanisha nini?
Kabla sijajibu swali hilo ni vyema tukipitia kwa ufupi mtiririko wa matukio (A quick refresher)
1. Dec 12,2024, Tundu Lissu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA taifa
Nia hii ya Lissu ilikuja baada ya kuwa uchokozi wa wazi dhidi yake ndani ya chama
Kabla ya uamuzi huu, Lissu aliyekuwa ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA, alishamwandikia barua katibu mkuu wake kumjuza nia yake ya kuendelea kugombea kubaki kwenye nafasi hiyo.
Ulikuwa ni utaratibu wa CHADEMA kwa viongozi wa juu kutoshindania nafasi moja endapo mmoja ataonesha nia