Fortunatus Buyobe Profile picture
Jan 31, 2022 42 tweets 8 min read Read on X
ASKARI MSTAAFU ALIYEKUWA ANANYONGA WATU GEREZA LA ISANGA -DODOMA.

Kifo kinatisha; kifo hakina huruma; kifo hutenganisha wapendanao, lakini kwa bahati mbaya, siku ikifika hakuna anayeweza kukikwepa. Image
Akionyesha hofu ya kifo alipokuwa na bendi ya Orchestra Makassy, Remmy Ongala aliimba kibao kinachoitwa “Siku ya Kufa”. Maudhui ya kibao hicho yalirejewa na Remmy mwenyewe japo kwa mahadhi tofauti alipojiunga na bendi ya Super Matimila. Huko alitunga kibao kiitwacho “Kifo” Image
Kana kwamba ana uwezo wa kufanya majadiliano na kifo aliimba: “Kifo, kifo, siku yangu ikifika eeh, kifo niarifu mapema, niage wanangu, niage familia yangu yote, pesa zangu nizigawanye, zimebaki nizile mwenyewe, kifo nakusubiri kwa hamu.”
Mwanamuziki huyo, aliyefahamika zaidi kwa jina la Dk Remmy, alifariki dunia akiacha kifo kikiendelea kuchukua uhai wa mamilioni ya watu duniani katika mazingira tofauti.
Baadhi hufa ghafla ajalini, wapo wanaofariki dunia baada ya kuugua, wengine huuawa na wenzao kwa hasira au kisasi au kwa bahati mbaya au bila kujua, lakini kuna wanaouawa kwa hukumu inayotolewa na vyombo vya haki; huhukumiwa kunyongwa hadi kufa. Image
Wanaopatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia huhukumiwa kifo. Japokuwa kila nafsi itaonja mauti, wanaohukumiwa kifo ndio huweza kujua siku na aina ya kifo.
Hivi mtu akihukumiwa kifo na mahakama, je, wanaofanya kazi hiyo ni nani? Kitanzi kikoje? Hali inakuwaje kabla? Je, hupata fursa ya kuaga ndugu na jamaa? Wanaotekeleza hukumu ya kunyonga wenzao hadi kufa pia wanakuwa wametenda kosa la kuua, je, huchukuliwa hatua gani kisheria? Image
Je, wanaoajiriwa kufanya kazi hiyo wanapatikanaje? Wanajisikiaje kukatisha uhai wa wenzao?

Lakini pia katika utumishi wao, ufanisi wao unapimwaje? Je, hupata utulivu wa moyo na amani kiroho? Image
Kwa kawaida kazi nyingi hutangazwa wazi magazetini na wale wanaojiona wana sifa zinazohitajika, huandika barua za kuomba na kusubiri kuitwa kwa mahojiano. Lakini, ni vigumu kukutana na tangazo la kazi hii ngumu kuliko zote.
Pia, najua kwamba baadhi ya kazi huhitaji wasomi wa kiwango cha juu, nyingine watu wenye ujuzi fulani lakini zipo zinazohitaji wenye nguvu.

Binafsi nadhani kazi hii inahitaji watu wenye moyo wa ujasiri ambao hawawezi kukosa utulivu wa moyo wala amani kiroho.
Maswali hayo na mengine mengi nimekuwa nikijiuliza kwa siku nyingi na katika kufuatilia nililazimika kufunga safari hadi mkoani Dodoma ambako nilifanikiwa kumshawishi mtekelezaji wa hukumu hizo afanye mahojiano nami. Image
Saa 12.00 jioni, nikiwa na mwenyeji wangu wa Dodoma tulifika nyumbani kwa mtu tuliyekuwa tukimtafuta, Anangisye (siyo jina lake halisi).
Huyu ni askari mstaafu aliyefanya kazi Jeshi la Magereza miaka 32 huku akitumia miaka 22 kufanya kazi hiyo maalumu ya kutekeleza hukumu za kifo
Tulipokewa na mjukuu wake, ambaye alituambia kuwa babu yake aliondoka nyumbani tangu asubuhi. “Shuuuuu,” tulishusha pumzi ikiwa ni ishara ya kukata tamaa, lakini kijana yule alitusihi tuvute subira.
Kijana yule alitukaribisha ndani na wakati tunaingia mama mwenye nyumba, Matilda (pia siyo jina lake halisi) alitupokea na kutukaribisha sebuleni.
Tunaingia katika nyumba hii, ya matofali, ina vyumba vitano na sebule. Vyumba vitatu vimepangishwa na vingine vinatumiwa na Anangisye na familia yake.
Mimi na mwenyeji wangu tukaendelea kukaa sebuleni tukimsubiri Anangisye huku mama mwenye nyumba akituelezea jinsi jino linavyomsumbua.

Baada ya robo saa hivi, sauti ya mwanamume ilisikika nje huku mama mwenye nyumba na yule kijana wakisema, “huyoo”.
Alipokuwa anaingia sebuleni, sote tulisimama na kusalimiana naye huku tukikumbatiana kana kwamba tulifahamiana siku nyingi. Punde alimwita mjukuu wake na kumtuma dukani akatununulie soda.

“Mnasema mnataka kujua kuhusu kazi maalumu?” aliuliza Anangisye nami nikajibu, “ndiyo baba”
“Mnanitafutia kazi nini maana nimestaafu tangu mwaka 2006,” alisema katika hali ya masihara.

Mara alibadilika na kusema kwa utani. “Lakini endapo itatokea kazi ya kunyonga niko tayari kufanya kwa sababu hakuna mtu yeyote anayeiweza kazi hiyo zaidi yangu,” alisema.
Anangisye ni mcheshi na mkarimu na wajihi wake ni mrefu, mnene, mwenye sauti nzito na anayependa masihara.

Baada ya masihara ya hapa na pale, Anangisye alianza kusimulia historia yake, alivyosoma, alivyopata kazi na jinsi alivyokuwa akitekeleza wajibu wake huo bila hofu.
Na hii ndiyo simulizi yake:👇

Mimi bwana ni mzaliwa wa Mbozi, sasa iko mkoani Songwe. Nilisoma hadi darasa la nane katika Shule ya Kati wilayani Mbozi. Mwaka 1974 niliomba kazi ya uaskari magereza. Nilipopata ajira nilipangwa gereza la Sengerema, Mwanza.
Huko nilifanya kazi kwa muda mrefu tu nikiwa askari wa kawaida wa magereza.

Mwaka 1984, yaani baada ya kufanya kazi kwa miaka 10 lilitolewa tangazo na Wizara ya Mambo ya Ndani kwamba anahitajika mtu kwa ajili ya kazi ya maalumu. Niliposikia tangazo lile niliomba nafasi
Basi, baada ya muda nikaitwa na Kamishna Mkuu wa makao makuu ya Magereza, Dar es Salaam. Nilipofika Kamishna akaniuliza: “Wewe ndiye Anangisye?”

“Nikamjibu, “ndiyo”.

Akaniuliza tena kama niliomba kazi maalumu na nikamjibu “ndiyo”.

“Basi umekubaliwa,” akasema.
Baada ya kuambiwa hayo nilielezwa zaidi kuwa Jeshi la Magereza limechagua watu wawili, yaani mimi na mwenzangu mmoja ambaye niliambiwa tutakutana Gereza la Isanga, Dodoma ambako kutakuwa kituo kikuu cha kazi yetu.
Niliambiwa kuwa kuanzia siku hiyo nitapelekwa Isanga na nitaripoti kwa RPO. Kwa hiyo nikawa nimeondolewa Sengerema Image
Nilipofika Isanga nilitambulishwa kwa mwenzangu na nikaambiwa kuwa tupo wawili tu nchi nzima na tutafanya kazi hii maalumu pale inapotokea na maelekezo mengine tutaendelea kuyapata.

Tuliambiwa kuwa tutakuwa tunafanya hiyo kazi nchi nzima, tutakuwa tunazunguka mikoani pale kazini Image
Kozi ya kunyonga.

Kitu cha kwanza baada ya kukubaliwa kupata kazi hii mimi na mwenzangu tulipewa mafunzo maalumu kwa muda wa mwezi mmoja palepale Isanga, tukafuzu, sisi wawili tu.
Mafunzo yetu yalihusisha namna ya kufanya kazi hiyo, namna ya kutumia kamba, mikanda ya kumshikilia mtu anayenyongwa pamoja na maandalizi yake.
Kuna namna ya kufunga kile kitanzi, ni lazima kiwe imara na salama ili yasitokee makosa. Lakini pia mikanda na eneo lenyewe na tulielekezwa jinsi ya kumweka mhalifu katika kitanzi chenyewe.
Katika ufanyaji kazi tulikuwa tunalindwa na askari magereza. Kwa mfano, siku ya kufanya kazi, tulikuwa tunasindikizwa na askari wakati wa kwenda na kurudi. Ilikuwa lazima tulindwe na ulinzi mkali wa askari ili isije kutokea tukapata madhara na kushindwa kutimiza wajibu wetu
Kwa mfano, tulipotakiwa kufanya kazi Mbeya tulikuwa tunapewa ulinzi wa askari kutoka Dodoma hadi Mbeya na tulikuwa tunapewa huduma za hali ya juu za malazi na chakula ili tuwe na nguvu.
Kitu kingine ni kwamba ule usiku wa kuamkia siku ya kazi, tulikuwa tunapewa pombe. Mimi nilikuwa nakunywa bia aina ya Safari; basi unawekewa hata kreti zima, tunakunywa, tunakunywa hadi asubuhi.
Hadi ninapoamka asubuhi bado nakuwa na pombe kichwani; kabla ya kazi kuanza bado nakuwa na mning’inio wa pombe kichwani. Jambo hili lilikuwa linatusaidia sana kufanya kazi yetu vizuri na kwa ujasiri.
Mwisho wa mwezi tulikuwa tunalipwa mshahara mzuri tu na pia tulikuwa tunalipwa posho. Kwa wakati ule, kila tukitekeleza kazi tulikuwa tunapewa Sh700 kwa kichwa, baadaye katika miaka ya 1990 posho hii iliongezeka hadi Sh5,000 na baadaye miaka ya mwanzoni mwa 2000 tulipewa Sh50,000
Matanga kabla ya kifo

Unajua vifo vingine vyote hutokea ghafla, lakini kifo cha kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kinajulikana. Mhalifu anajua kifo chake tangu siku anaposomewa hukumu yake ila anachosubiri ni kutekelezwa kwa hukumu hiyo basi.
Kwa utaratibu wa magereza, mhalifu aliyehukumiwa kifo, hutayarishiwa matanga siku moja kabla ya kunyongwa. Wanamweka katika chumba maalumu; kila mmoja kwenye chumba chake. Wanamfungia humo na wanampa chakula na huduma yoyote anayoitaka, hayo ndiyo matanga yake.
Wakati waliohukumiwa kifo wakiwa kwenye matanga, wafungwa wengine huimba nyimbo za maombolezo kama sehemu ya kuwaombea wenzao kabla kifo hakijawameza. Matanga hayo ni ya siku moja tu.
Kabla ya kumweka kitanzini, mfungwa yeyote huwa na maandalizi yake. Viongozi wa dini zote mbili za Kiislamu na Kikristo huitwa, wanafika magereza na kuwaongoza wahalifu sala ya toba.
Huo ndio utaratibu. Wakishafanyiwa sala ya toba au kuongozwa sala yoyote ile inayofaa kabla ya kifo, huwekwa tayari kwa ajili ya kunyongwa.

Anakuwepo pia mwanasheria wa magereza. Haiwezekani wakanyongwa bila ya kuwepo viongozi wa dini.
Hanyongwi mtu mmoja, inawezekana kwa siku moja wakawa watu wanane au kumi, inategemea na waliohukumiwa mwezi huo. Baada ya kutekeleza hukumu hiyo kwa mtu mmoja, nilikuwa naenda kupumzika kwa dakika 45 kabla ya kuendelea na kazi hiyo kwa mtu mwingine.
Kwa kawaida kazi huanza saa 2.00 asubuhi, baada ya kumaliza kazi tunakwenda kupumzika ofisini, tunakunywa kinywaji pale, baada ya dakika 45 tunarudi tena kuendelea na kazi.
Baada ya mapumziko ya dakika 45, tunakwenda kuangalia kama ameshafariki dunia, tukimaliza kuhakiki tunaendelea na wengine hadi waliopangwa siku hiyo wameisha. Kwa siku walikuwa watu wanane kutegemeana na idadi ya waliohukumiwa na kitanzi kinaweza kutumiwa na watu watatu kwa mpigo
“Kwa hiyo, tukimaliza watatu, tunasubiri na kuendelea na kazi.”

Follow account yangu @fbuyobe kisha weka notifications nitaendelea baadae.

Usisite kunifata telegram kwa

t.me/fbuyobe

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Fortunatus Buyobe

Fortunatus Buyobe Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @fbuyobe

Jan 24
Before writing this masterpiece to this X street, I gave myself ample opportunity to scrutinize and verify the facts.

The matter beforehand today is fragile as it can defame someone's business and reputation.

But why should I lie when I can speak the Truth?

Tariq M. Machibya Image
Bwana Tariq Machibya alipofikishwa mahakamani kwa kuendesha biashara ya upatu, watu wengi tulimuhurumia kwa kuhisi Serikali inamuonea kijana mdogo mjasiliamali.

Kijana ambaye alibeba ndoto na maono ya wenye mitaji wasiojua pa kuwekeza.

Some sort of financial intermediary

Alas! Image
Kwa tuliosoma mambo ya Finance, tunafahamu Benki kuu ndiyo huratibu mzungungo wa fedha nchini ili kuzuia mfumuko wa bei na mengineyo.

Kutokana na hili, taasisi zote za kifedha husajiliwa na kuratibiwa utendaji wake na benki kuu.
Read 48 tweets
Dec 13, 2023
Naam!

Aliyekuwa mke wa marehemu bilionea Msuya anayeshitakiwa kwa mauaji ya wifi yake Aneth Msuya inakaribia ukingoni.

Dalili za "kutema ngeze" ziko wazi baada ya wazee wa baraza kutoa maoni haioni hatia dhidi yake.

Uzi huu ni mtiririko wa matukio A-Z

Image
Image
Image
Usiku wa manane kuamkia 26 july 2013,ndugu WILLY MUSHI ONESMO anapigwa risasi na kufariki akiwa kazini

WILLY MUSHI ONESMO alikuwa ni mfanyakazi wa mgodi wa madini TANZANITE ONE huko MIRERANI Simanjiro. Image
Kulikuwa kuna tabia ya wachimbaji wadogo wanaouzunguka mgodi huo,kuingia chini kwa chini na kwenda kuiba madini mgodi wa Tanzanite

Wenyewe wanaita "MTOBOZANO" au "KUTEKA NJIA" Image
Read 43 tweets
Nov 30, 2023
Bado nipo kwenye coma nikijiuliza kama kulikuwa na ulazima wowote kwa askari huyu kuingia na mtutu wa bunduki kwenye eneo la starehe.

Bado najiuliza,

Kulikuwa na ulazima wa kumuelekezea bunduki namna hii yeyote awaye(hata kama ni kahaba) ambaye hajainua silaha yoyote

Najiuliza Image
Kuna mambo mengi yamekuwa yakifanywa na polisi kiholela sana.

Moja ya mambo haya ni kazi ya kukamata walevi au wenye bar wakipitisha muda wa kufunga bar.

Polisi hapaswi kukamata kosa hili bila kuwepo kwa mlalamikaji ambaye ni afisa biashara wa manispaa aliyetoa leseni ya kileo Image
Polisi kazi yake ni kumuimarishia ulinzi afisa biashara wakati anambana aliyekiuka masharti ya leseni

Polisi wakiona unatambua sheria hii wanakutupia kesi yoyote ikiwemo uzembe za uzururaji

Hata sheria kuhusu makahaba mlalamikaji ni afisa ustawi wa jamii wa manispaa husika Image
Read 31 tweets
Nov 16, 2023
KUWENI MAKINI NA MCHANGA WA KABURINI:

#X-Ushirikina

Kuna watu wamepata nuksi, mikosi na mabalaa makubwa katika maisha yao kwa sababu ya matumizi ya mchanga wa makaburini bila kuzingatia au kufuata maelekezo. Image
Unapokuwa unafanya kitu chochote kile kinacho yahusisha makaburi, iwe ni kutumia mchanga, kuzika vitu, kuoga, kuchoma ama kutambika, unatakiwa kuwa makini sana na kufuata na kuzingatia kanuni na taratibu zake kwa sababu usipo zingatia hayo yatakupata makubwa. Image
Kwa bahati mbaya sana watu wengi wamekuwa wakitumia mchanga wa makaburini bila kufuata taratibu na matokeo yake wamevaa nuksi,mikosi na mabalaa makubwa ya maisha. Image
Read 23 tweets
Nov 7, 2023
Miaka minne iliyopita, Jimmy Kizota alishitakiwa kwa kosa la kumuua mchumba wake aliyekuwa akiishi naye jijini Dar es salaam.

Ni baada ya kumfumania akifanya mapenzi na mwanaume mwingine sebuleni kwao aliporudi nyumbani ghafla akitokea kazini majira ya saa tano asubuhi. Image
Mwanaume aliyefumaniwa alifanikia kumzidi nguvu Jimmy na kukimbia

Wivu na hasira kaishia kwa kumpiga mchumba wake hadi akapoteza fahamu.

Baadae mwanamke huyu akafariki akipatiwa matibabu hospitali.

Jimmy akashitakiwa kwa mauaji ya kukusudia

Kesi ilimkalia vibaya sana Image
Hata hivyo Jimmy alikuja kuokolewa na mfanyabiashara maarufu jijini Dar mwenye kila sifa za umafioso

Mfanyabiashara huyo aliitwa Mzee Beka

Ilitokea tu kama bahati kuwa Jimmy alifahamiana na mke wa Mzee Beka aitwaye Nasra tangu wakiwa mkoani Mwanza

Familia zao zilikuwa jirani Image
Read 55 tweets
Nov 6, 2023
Ndani ya behewa moja, kulikuwa na abiria aliyekuwa ametulia kimya kwenye kiti akiwaangalia abiria wenzake waliokuwa kwenye harakati za kushuka.

Mtu huyo aliyeonekana kutokuwa na haraka, alikuwa amekaa kwa kuuegemeza mguu mmoja juu ya mwenzake kama bado akiendelea na safari. Image
Mtu huyo ambaye safari yake ilianzia kituo cha treni cha Kingorwila Morogoro, alipanda akiwa hana mzigo wowote aliobeba mkononi

Tangu anaingia hadi kupata siti kwenye behewa aliloingia, hakuzungumza na abiria yeyote, hakuinuka kwenda kokote, hakutikisika wala kumwangalia yeyote. Image
Baadhi ya abiria walimwangalia kwa mashaka. Wengine wakimhisi ni mwendawazimu.

Dhana hiyo ikawajengea woga dhidi ya mtu huyo wakawa makini naye muda wote wa safari.

Moja ya sababu ya kumwogopa, ni ukimya wake alioujenga tangu alipoingia kwenye behewa walilokuwemo. Image
Read 11 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(