Dunia ya leo imejikita zaidi katika demokrasia. #Demokrasia kwa ufupi ni dhana inayolenga ushiriki wa wananchi katika kuweka misingi sahihi ya uendeshaji wa nchi wao wakiwa ndio msingi wa mamlaka yote ya nchi na walio na uwezo wa mwisho wa kuipa serikali madaraka na mamlaka yake.
Moja ya misingi mikuu inayolenga kukuza demokrasia ni Katiba ya Nchi. Katiba ni msingi mkuu wa uendeshji wa nchi, ukuaji wa demokrasia na utawala wa Sheria. Katiba ndiyo sheria kuu (mama) na ambayo kwayo sheria zote nyinginezo hupata uhalali na hufungamana na Katiba.
Katiba huweka bayana misingi ya utawala, vyombo vya utawala, na mgawanyo wa madaraka baina ya vyombo vikuu vya dola 👉🏽
Bunge, Mahakama na Serikali (Watendaji wakuu) Kubwa zaidi, Katiba ndiyo
inayoainisha nafasi waliyonayo wananchi katika kuweka utaratibu wa kuendesha nchi yao.
Kwa muda mrefu sasa, hasa baada ya mabadiliko ya sera za kiuchumi na Kutoka kwenye mfumo wa chama kimoja na kuingia katika mfumo wa vyama vingi, umma wa Watanzania umeghubikwa na hoja mbalimbali za msingi sana kuhusu
mustakabali wa taifa letu la Tanzania.
Hoja kubwa ni 👉🏽Katiba.
Tangu miaka ya 1990‘s Hoja kubwa ya watanzania ilikuwa ni suala la kuwepo kwa Katiba Mpya. Makongamano na warsha mbalimbali ziliitishwa kuijadili Katiba na madai
mbalimbali yakatolewa yakikosoa muundo wa Katiba hii ya sasa, kulingana na
mazingira tuliyonayo na hivyo…
watanzania walidai kuitishwa kwa kongamano la kikatiba nchini ili kuunda Katiba Mpya, na matunda yake ilikuwa ni kutungwa kwa Sheria ya
Marekebisho ya Katiba 2011 ambayo hata hivyo ililamikiwa sana kwa kutungwa
bila kuwapa watanzania nafasi ya kushiriki..
na pia kumrundikia Rais madaraka yote
bila hata kuwashirikisha wapiga kura wake. Wananchi hawakushirikishwa kikamilifu kabla ya kutungwa kwa Sheria ya marekebisho ya Katiba 2011. Sheria ambayo ilitoa nguvu ya kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya uliogota 2014.
Ukweli Mchungu, dunia ya leo demokrasia na utawala wa kidemokrasia ni moja ya dhana muhimu sana zinazoleta mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi. Demokrasia na utawala wa
kidemokrasia sio tu vichochezi vya maendeleo bali ni mihimili mikubwa ya kupambana na umaskini.
Pasipokuwepo na demokrasia na utawala unaojali demokrasia na kanuni ambatanishi
kama vile utawala wa Sheria, heshima kwa haki za binadamu na Utawala Bora, uwezekano wa kupambana na umaskini na ufukara ni ndogo sana.
Taifa lolote lisilojali demokrasia ya dhati , Utawala Bora na Utawala wa Sheria huanguka ama hubaki maskini na tegemezi kwa vile
huwa linaua fursa muhimu mbadala ambazo kama zingepewa nafasi, zingeleta
matokeo chanya katika maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Ili Taifa libadilike kiuchumi, kisiasa na kijamii ni lazima watu washirikishwe kikamilifu katika kuandaa mazingira ya mabadiliko hayo na hasa
ushirikishwaji katika kuweka misingi imara ya mabadiliko yenye manufaa na
yanayolenga mbali na upeo wa leo.
Ushirikishwaji sahihi wa umma katika kuweka
misingi ya kuiendesha nchi ndicho chanzo pekee cha kuimarisha demokrasia Utawala wa Sheria, Utawala Bora, Haki na Usawa.
DEMOKRASIA ni kuwa mamlaka yote iko kwa umma na kwamba serikali itapata mamlaka yake toka kwa umma. Ni hakika na dhahiri sikuzote kuwa, Wananchi ndio wenye nchi. Wananchi ndiyo wanapaswa kuwa na sauti ya mwisho jinsi wanataka nchi iendeshwe kwa kuilinda, kuitetea Katiba.
Ili wananchi wawe ndio wenye nchi na wenye mamlaka ya mwisho juu ya mustakabali wa mambo yahusuyo nchi na rasilimali zake, utashi wa kisiasa na uchumi, basi ni lazima uwepo
mfumo imara uliotokana na ridhaa yao na unaoweka bayana kanuni na taratibu za
msingi na za kidemokrasia.
Msingi huo mkuu wa mfumo huo muafaka si mwingine bali ni Katiba ya nchi. Kukosekana kwa katiba yenye ridhaa halisi ndicho chanzo kikubwa
cha kuparanganyika kwa jamii na kudumaa kwa maendeleo na ustawi wa nchi hasa katika
nchi nyingi za dunia ya tatu hasa Barani Afrika.
Katiba itokanayo na umma (wananchi) hutoa
uthibitisho na uhakikisho kwa umma kuwa, sura na utaratibu wa uundwaji wa serikali utatokana na namna au utaratibu ule ambao wao (umma) wameukubali na kuridhia kitaifa. Katiba ndiyo inayoweka bayana mihimili ya
utawala wa dola.
Katiba madhubuti itokanayo na umma ni
kiashiria kwa wananchi kuwa utawala wa sheria na heshima kwa binadamu na misingi yote ya
haki italindwa na kuhifadhiwa ndani ya Katiba na kwa mujibu wa Katiba hiyo serikali itatekeleza wajibu wake.
Kwa hali hiyo, ni mwiko kwa serikali kutumia
madaraka yake isivyo halali na au kwa mabavu na pia haitaweza kamwe kufanya maamuzi kandamizi au kutunga sheria au sera yoyote kandamizi na inayokiuka misingi ya haki kama ilivyobainishwa ndani ya Katiba.
Katiba ni sheria mama (grundnorm
or the basic law) Katiba iliyo madhubuti hutoa hakikisho kwa umma kwamba, sheria zote, nguvu ya kisheria na kiutawala, sera zote na kanuni zozote zile, lazima zifungamane na kupata uhalali wake kutokana na Katiba waliyoiridhia wananchi wenyewe.
Katiba hutoa hakikisho la jamii huru na vilevile huihakikishia jamii hiyo uhuru, uwiano na fursa sawa katika shughuli zozote zile, ziwe za kiuchumi, kijamii au kisiasa. Hivyo, Katiba huweka mazingira yenye kanuni na taratibu sawia kuhusu ukuaji na ustawi wa taifa husika.
Katiba madhubuti inatoa fursa Taratibu kama za Uchaguzi Uuru na wa haki unaojali uwazi na unaotoa mwanya wa asiyeridhika kuwasilisha hoja zake mbele ya chombo huru cha utoaji haki ( mahakama) bila kikwazo chochote au gharama kubwa, ni
sehemu muhimu ya Katiba iliyo madhubuti.
Katiba iliyo madhubuti huwa ni msingi mkubwa wa utawala bora, na unao zingatia uwazi, uwajibikaji na utawala wa sheria , dhana ambazo kwa pamoja ni misingi mikubwa ya demokrasia na maendeleo ya nchi.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Goodluck 全能神的僕人

Goodluck 全能神的僕人 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @RealHauleGluck

Mar 29
#Jielimisheni: mchakato wa kupata Katiba Mpya Tanzania ulianza tangu mwaka 2010, wakati Rais wa wakati huo, @jmkikwete alipoamua kuutangazia umma dhamira na nia ya serikali ya CCM kuanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya.

👇🏻
Mchakato wa Katiba Mpys ukaanza rasmi mwaka 2011 kwa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 na baadaye ikatungwa Sheria nyingine ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitamka kuanzishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilianzishwa chini ya Waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba, ikaratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya Katiba.
Read 7 tweets
Mar 29
Spika wa Bunge la Space si alikuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba na alishiriki kupigia kura Katiba Pendekezwa na Ma-CCM wenzie Katiba ambayo CHADEMA walisusia na kutoka nje na kuunda UMOJA WA KATIBA YA WATU (UKAWA)?

Je, Katiba Pendekezwa ilikidhi matakwa ya wananchi?

👇🏻
Katiba iliyopendekezwa ina mapungufu makubwa pia ilitupilia mbali maoni muhimu ya wananchi kama:

> Kupunguzwa kwa madaraka ya Rais: wananchi
walipendekeza madaraka makubwa ya Rais hasa ya uteuzi yapunguzwe na ziundwe Taasisi za kikatiba za kumshauri Rais kabla hajafanya teuzi.
> Kutenganisha Mamlaka ya Mihimili ya Dola Wananchi walipendekeza Uhuru zaidi kwa Bunge na Mamlaka zaidi kwa Bunge kuisimamia, kuiwajibisha na kuishauri Serikali. Pendekezo hili linaenda sambamba na kutenganisha serikali na Bunge, hali ambayo iko sasa.
Read 24 tweets
Mar 27
#Tanzania: Mvutano mkali unaendelea kutamalaki miongoni mwa watu binafsi, wanaharakati, wanasiasa, vyama vya siasa na viongozi wa chama tawala na vyama vya upinzani na serikali kuhusu uwezekano wa kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya kabla ya UCHAGUZI MKUU 2025.
Madai ya Tume Huru yanasukumwa na hoja kwamba uwanja wa shughuli za siasa hauna usawa, bali unaweka mazingira ya kukipa faida zaidi chama tawala, huku kukiwa na madai ya mara kwa mara ya ukiukwaji wa sheria, ukosefu wa uhuru na kuwepo kwa mamlaka makubwa ya Rais juu ya Tume hiyo.
Madai ya Katiba mpya yanasukumwa na dhana kwamba Katiba Mpya ndilo jawabu la mambo mengi yanayolalamikiwa yakiwemo: mfumo wa uendeshaji nchi, madaraka ya Rais, Haki, Usawa, demokrasia, Uhuru wa kufanya siasa, Uhuru wa Mihimili katika kutekeleza majukumu yao na hata Tume Huru.
Read 14 tweets
Mar 26
#TunduLissu asema waliompiga risasi ni Kikosi Kazi (TASK FORCE) cha Ofisi ya Rais (Dr. Magufuli) chini ya aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa DGI-TISS kwa sass Balozi Dr. Kipilimba.
@TunduALissu anasema alitarajia Rais @SuluhuSamia ataondokana na kivuli cha Rais JPM.
Comrade @TunduALissu awataja waliohusika kumshambulia.

Bw. Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.
Kimeua watu wengi sana, Kikosi kazi hicho kilijumuisha watu wa Usalama wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya na uwindaji haramu (Poaching).
Read 5 tweets
Mar 26
Cries of victims in Ethiopia and Yemen go unheard as the West focuses on Ukraine.

For the past one month, the entire world has been justifiably horrified by the events in Ukraine. Ever since Russia started its invasion of Ukraine in February 2022… opindia.com/2022/03/victim…
For the past one month, the entire world has been justifiably horrified by the events in Ukraine. Ever since Russia started its invasion of Ukraine in February 2022, thousands have died, and millions have become refugees leaving their homes.
The Western world has acted as one and has imposed strict sanctions on Russia while providing Ukraine with Billions of dollars worth of aid and weapons. Meanwhile, there are other conflicts around the world, including in Ethiopia, Yemen and other places,
Read 4 tweets
Mar 21
Kwa kifupi, mabadiliko hayo yalianza mwaka 1979 yaliyopelekea kuunzishwa na kuingizwa kwenye Katiba Mahakama ya Rufani baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mabadiliko ya pili yalikuja Mwaka 1980 ambayo yalilenga kupunguza kero mbalimbali za muungano.
Mwaka huo huo kulitokea mabadiliko ya tatu ambayo yalifafanua mfumo mzima wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, serikali yake pamoja na Baraza la Wawakilishi. Mabadiliko ya nne yalitokea mwaka 1982 yakiwa na kusudio la kuboresha uteuzi wa wakuu wa Mikoa.
Mwaka 1984 yalitokea mabadiliko mengine ya tano na kuingiza tamko la Haki za Binadamu kwenye Katiba ya Mwaka 1977. Mwaka 1990 kulitokea mabadiliko mengine mawili katika nyakati tofauti ya sita na saba na kuanzisha tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC)
Read 11 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(