Madinidotcom Profile picture
Apr 7 25 tweets 5 min read
CORONA VIRUS NI KAZI YA MAABARA? WHY CHINA?
#PichaLinaendelea sehemu 2

Lakini SIDE B kuna issue ya LABARATORY THEORY niliyokugusia mwanzoni ambayo mataifa mengi
yameanza kurudi kujiuliza na CHINA inatumia POWER yote kuhakikisha hilo halifanyiki. Ni Theory gani
hii?
Kwanini kuna hizi maabara za VIRUSI hatari duniani?By the way leo tunaongelea CHINA tu lakini
marekani pia wana mahabara kama hizi kibao na zimejaa virusi hatari kibao,vya faida gani?Kwanini MAREKANI na CHINA wanatupiana mpira?.PICHA LINANOGA
So kama tulivyosikia dunia ina maswali mengi kuhusu Corona na kubwa linalojitokeza ni LAB THEORY
ambayo imeanza kuuliziwa vikali na wakubwa.Kabla haijathibitika kama kweli ni kazi ya maabara ama
lah,Kuna mwingine utauliza kwani tukijua ndo isaidie nini?Well
dunia inataka kujua kama endapo kuna
virusi wengine tuambiane mapema?Ukifuatilia hadi mwisho utaelewa zaidi.
acha tuangalie nini tunafahamu mpaka sasa kuhusu MAABARA ILIYOPO CHINA inayoshutumiwa na yote haya?Hii ndio sehemu ambayo wachunguzi wa huu msala wanataka wakakague
mle ndani kama ndo chanzo.China wamesema“hatutaki wageni na msituambie ivo sisi".So kunani?
Well,Hii ni WUHAN INSTITUTE OF VIROLOGY ambayo ni maabara kubwa zaidi ya utafiti na hii ndio BANK kubwa zaidi ya VIRUS barani Asia. Ndani ya hii maabara ama taasisi hii iliyo chini
serikali ya China kuna aina buku jero(1500) ya virusi .Vyote wanafanyiwa utafiti na hapa tunazungumzia wanasayansi sio wanasiasa,so ukifikiria CHINA usifikiri tunazungumzia serikali ya china,lakini kwa namna flani wataalamu hawa wanasimamiwa na serikali kuu.
Watu wanahofia siku hizi virusi vikitua mikononi mwa watu wabaya km magaidi n.k?Picha linaanza hii maabara ipo kilomita 5 na nusu kutoka soko la machinjio ya WUHAN ambapo ugonjwa
wa Corona unatajwa kugundulika kwa mara ya kwanza.Wagonjwa wengi wa kwanza walikuwa wametoka eneo
Hili kununua vitoweo Hii maabara ina historia ya majaribio mengi yenye utata,mwaka 2005 ilipost research moja ambayo walifanya kuhusu ORIGINAL ya virusi aina ya SARS ambapo waligundua kuna aina ya POPO ambao
wamegundulika wana virusi wanaofanana sana na wale wanaosababisha
ugonjwa huo wa SARS ambao
ulikiki sana enzi hizo. so jamaa wakaanza kazi ya kuwasaka popo hao popote walipo China kwaajili ya
kuwacheki kama wana maniaje niaje yanayosababisha watu kufariki kwa kukohoa.Mara zikaja taarifa zilivuma miaka ya 2012 kuwa kuna mgodi mmoja kusini
mashariki mwa China ambao
kuna popo wengi,wananchi wakasema ukimdaka ukamtia kwenye sufuria ili upate supu swaaafi ya kugonga na chapati 2,ukishashiba tu unaanza kukohoa mara NEMONIA MARA unarest in peace yaani unarudi zako kwa mola.
So wataalam ikabidi watumwe kwenye mgodi
huo uliotelekezwa eneo moja linaitwa MOJIANG kwenye jimbo la YUNNAN ambapo kuliripotiwa kesi za watu kuugua kiajabuajabu so wiki 2 baada ya kikundi cha madaktari hawa watafiti kuingia hapa kwenye huu mgodi,baadhi yao waliugua na wengine walifariki kwa Nimonia ya ajabu ajabu
Mmoja alikaa hosipital miezi 5
Walipofanya utafiti wao wakagundua virusi hao wanaitwa RAT -G-13 (tamka RAT G ONE, THREE).hapa sasa ndo mchezo unaanza kubadilika.Miaka miwili baadaye MAREKANI yaani wanasayansi wa kutoka chuo cha NORTH CAROLINA cha marekani waliingia kwenye
utafiti huu na kuanzisha ushirikiano kwenye utafiti huu wa Pamoja kati yao na wanasayansi wa maabara hii ya WUHAN ya china wakafanya kile
knachitajwa na kinachofahamika kama GAIN OF FUNCTION RESEARCH ambayo kwasasa watu wengi
wanahoji kwanini ilifanyika.
Hiki kinachoitwa A GAIN of FUNCTION RESEACH ni idea ya kutengeneza kirusi hatari mara 15 zaidi ya kirusi original, kwa kuchukua sehemu ya virusi waliopo kwa wanyama ambao hawana uwezo wa kuwaathiri binadamu kisha kuwa ongezea uwezo wa kushambulia seli za binadamu.
Ni kati ya tafiti hatari kufanyika na zinazohitaji uwekezaji mkubwa sana na lengo ni kufahamu zaidi kuhusu virus husika na kuvitafutia dawa mapema endapo vitaingia kwa binadamu.Lkn hata wanasayansi wengi hupinga aina hizi za TAFITI wakisema ni wazi ni kama kucheza na hatari bila
Sababu yeyote kwasabab endapo virus hao wakitua mikononi mwa wahuni,kila mtu duniani ata suffer Lengo jingine la tafiti hizi ni kujua ni virusi gani walio ndani ya wanyama tulionao ambao wanaweza baadaye kujifanyia manuva kiasili na kuwa na uwezo wa kuwaathiri binadamu.
Mpk sasa takwimu zinaonyesha hakuna dawa wala ugonjwa uliowahi kupatiwa ufumbuzi kupitia aina hii ya utafiti,lkn
wanasayansi wanaamini miaka ijayo GAIN OF FUNCTION research inaweza kuwa suluhu.Wengi wanasema ni jambo lisilo na maana na hatari kwa watu wengine.
So china na marekani mwaka 2014 walishirikiana kufanya hii research wakati huo rais wa USA akiwa BARAKA OBAMA.Utafiti huu ulionekana ni hatari kwasababu kirusi hiki ambacho ni MAN MADE kiliongezewa nguvu mara 15 zaidi ya kirusi original na endapo ikitokea uzembe kidogo
inamaanisha dunia ipo mashakani. So baadaye serikali ya marekani ilijitoa kwenye research hii.Tunaposema kujitoa inamaanisha waliacha kufadhili mchongo huu official na sabab ilikua hii hii ya kiusalama,viongozi weng
wa wkt huo walikataa kupitisha wakiona hatar zote zilizokuwepo
Lkn sasa taarifa zinaeleza Marekan ilizidi kufadhili mchongo huu kinyemela.Kivipi?Hapa kumbuka
tunazungumzia wanasayansi na sio wanajeshi wala wanasiasa. So kvp? Mwaka huohuo 2014 taasisi ya
kupambana na magonjwa ya kuambukiza na aleji yaani NATIONAL INSTITUTE OF ALLERGY AND
INFECTIOUS DISEASES kwa kifupi N.I.AID kupitia boss mkurugenzi kitambi meneja wao ankali Dr.ANTONY FAUCI (tamka FAUCHI) walituma kitita cha dolla milion 3.4 ambayo kibongobongo ni zaidi ya BILIONI 7 na milioni mia 8 themanini na tano.Hili ni zaidi ya Dili la Haji manara na Simba.
Taarifa zinaonyesha pesa hizi zilienda kwenye taasisi moja ya AFYA iliyopo NEW YORK ndani yamarekani inaitwa ECO HEALTH ALLIANCE(tamka IKO HELTH ALAYANS).Hawa jamaa wa ECOHEALTH wakaonekan wamelipa pesa flan kwenda kwa ile maabara ya WUAN ya china dolla laki 5 na elfu 95 na mia 5
(598,500$) ambayo ni sawa
na Bilioni 1 na milioni mia 3 themanini na 8 za kibongo.Kifupi inakaribia BILIONI 1 na nusu za kibongo na
hizi waliwatumia kila mwaka kwa miaka 5 mfululizo,kwaajili ya kufanya utafiti wa virusi wa SARS.
Dr.Fauchi juzi kati akawekwa kwenye KITIMOTO
kuulizwa kwanini alikuwa anawalipa CHINA hizi pesa na akasema Hajawahi kufanya hivyo,lkn kwenye maelezo yake ya baadaye baada ya kubanwa na
wajumbe wa kamati maalumu ya bunge la marekani,ikabidi aseme hakuwa na nia mbaya,na kilichokuwa sio GAIN OF FUNCTION RESEARCH
ila ni kitu kingine Ubishani ulikua ni mkali.Lakini dr FAUCI
ambaye ndiye anayesikilizwa marekani nzima kuhusu COVID19,alishikilia msimamo wake....

#PichaLinaendelea post ijayo lkn hizi story zote zinapatikana kwenye kitabu cha madinidotcom kwa 10k

Pia story iko audiomack

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Madinidotcom

Madinidotcom Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @madinidotcom

Apr 9
KUTENGANA KWA KOREA KUSINI NA KASKAZINI ,CHANZO NA MATOKEO
YAKE

#PichaLinaendelea Wote tunajua kuna KOREA 2,Wale wa kaskazini kama Johmakini na wa kusini kama konde boy .Sasa STRAIGHT To the point, nini sababu ya wao kutengana?JIBU fupi Ni vita vya pili vya dunia.Ilikuwaje? Image
Korea ilikuwa nchi moja tangu karne ya 7 means tangu miaka ya 1700 mpaka
1945.Karne za kutosha wamekaa pamoja chini ya HIMAYA YA SILLA
WANAITA SILLA DYNASTY(sila dainasti).Mwanzo ulisikia chanzo cha ketengana ni VITA VYA PILI VYA
DUNIA(1945) lakini story kidoogo
ilianzia nyuma ya hapo.Kuna ‘ndondi’ flani zishawahi kupigwa kati ya JAPAN na CHINA,hii vita inaitwa First Sino -Japanese war,imagine wanasema ni vita kati ya CHINA na JAPAN lakini picha halisi ni tofauti kabisa.JAPAN alikua ndo Baba lao miaka hyo kutokana na walichukua mfumo
Read 25 tweets
Apr 7
CORONA VIRUS NI KAZI YA MAABARA? WHY CHINA?

#PichaLinaanza CORONA VIRUS!True story hatimaye tumepata HIT SONG iliyosikilizwa na wote wazee,vijana,
watoto,wanasiasa,madaktari na wahuni wa skani.Mara ya mwisho tumepata hit song ya aina hii ilikuwa #MUZIKI ya Darassa ft Benpol. Image
Kabla ya hapo CONGO WALITULETEA ‘’TWANGA PHOTO WAAAAH,
ekotiteee,ekotiteee’’ ya Kofii olomide. au Mbele tukasikia DESPACITO…
Hii sio mara ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho kusikia virusi kusambaa duniani kutoka nchi china. So
why CHINA?
Dunia imeshaingia kwenye process ya CHANJO na mjadala wake ni mkubwa na mzito .We unaamini nini?Ni hiari na maamuzi yako.Kwanini China ndo chanzo cha haya yote?
PICHA LINAANZA #2019 China wakijiandaa kudamshi na mwaka mpya ,BREAKING NEWZ watu walianza
kupata kikohozi kikavu
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(