#Tujielimishe: ⚡️SHERIA NA TARATIBU ZA UMILIKI WA ARDHI TANZANIA BARA

- Chimbuko na misingi ya mfumo wa umiliki na matumizi ya ardhi yaliyopo sasa umepitia katika vipindi vifuatavyo:-

Uzi 🧵…..

👇🏻
MFUMO WA MILKI YA ARDHI KABLA YA UKOLONI

Katika kipindi hiki mfumo wa milki ulikuwa na sifa nne zifuatazo:-

· Ardhi yote ilikuwa ikimilikiwa kimila.
· Ardhi ilikuwa kwa ajili ya matumizi tu. mf-Kilimo,makazi,ufugaji,matambiko nk
· Wananchi walikuwa na sauti ya mwisho katika ardhi yao.
· Viongozi wa mila na jadi walikuwa wasimamizi na wasuluhishaji wa migogoro.
MFUMO WA MILKI YA ARDHI WAKATI WA UKOLONI (1890- 1960)

- Tanganyika ilitawaliwa na Wajerumani na Waingereza.
Wajerumani walitawala (1890–1919)

- Tamko la Wajerumani la mwaka 1895 liliweka bayana kuwa ardhi yote ni mali ya Mfalme Kaiza wa Ujerumani.
- Walianzisha umiliki kwa njia ya Hati.
Waingereza walitawala (1919–1961)

- Walitunga sheria ya Ardhi na 3 ya 1923 kuweka msisitizo katika mfumo ulioanzishwa na Wajerumani na kutamka kuwa ardhi yote ni mali ya umma chini ya Gavana.
- Umiliki wa hati ulikuwa na nguvu kisheria dhidi ya umiliki wa kimila
Katika kipindi cha ukoloni wazawa walipoteza sauti juu ya ardhi yao.
KIPINDI CHA UHURU HADI SASA

Kipindi cha miaka ya 1961- 1990

- Mamlaka ya Gavana juu ya ardhi ilihamishiwa kwa Rais.
- Mwaka 1967 Azimio la Arusha lilitangazwa kuweka misingi ya uzalishaji mali mikononi mwa umma.
- Sheria zilizotungwa katika kipindi hiki ni pamoja na Sheria ya Utwaaji Na. 47 ya 1967 ambayo iliwezesha utwaaji wa ardhi kwa matumizi mbalimbali kama vile uanzishwaji wa Mashamba ya NAFCO na NARCO na Sheria ya Vijiji
na Vijiji vya Ujamaa Na. 21 ya 1975 ambayo ilihalalisha uanzishwaji wa Vijiji vya ujamaa.
Kipindi cha kuanzia 1991 hadi sasa
- Licha ya kuwepo kwa Sheria hizo bado vijiji vingi viliendelea kuwa na migogoro kutokana na kuingiliana kwa haki na maslahi kati ya wakazi wa vijiji vipya na vya zamani
- Migogoro hiyo ilipelekwa kuundwa kwa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Masuala ya Ardhi mwaka 1991.
- Mwaka 1992 ilitungwa Sheria ya Milki ya Ardhi Tanzania ambayo ilifuta Vijiji vya asili na kuhalalisha vijiji vya ujamaa.
Tume ilitoa mapendekezo yake mwaka 1992 ambayo ni pamoja na:-

- Ardhi ipewe ulinzi wa Kikatiba
- Kuwepo na Sera na Sheria ardhi za kizalendo
- Kuweka milki ya hatma kwenye vyombo vyenye uwakilishi mpana wa wananchi
- Kuunda mfumo wa usuluhishi na utatuzi wa migogoro ya ardhi kuanzia ngazi ya kijiji
- Ardhi igawanywe katika makundi
Mapendekezo hayo yalipelekea kutungwa kwa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na Sheria za Ardhi Na. 4 na Na. 5 za mwaka 1999.
MASUALA MUHIMU KATIKA SERA NA SHERIA ZA ARDHI NCHINI TANZANIA
SERA YA TAIFA YA ARDHI YA 1995

Sera hii inaweka kanuni za msingi zinazotawala mfumo mzima wa umiliki, usimamizi na matumizi ya ardhi nchini. Kanuni hizo ni pamoja na:-
· Kutambua kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na kuwa imewekwa mikononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya raia wote.
· Kulipa fidia kamili, ya haki na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki inafutwa matumizi yake.Pia kuwezesha ardhi kugawiwa kwa haki na kupatikana kwa raia wote
· Kuwawezesha raia wote kushiriki katika kutoa maamuzi ya mambo yanayohusiana na milki au matumizi yao ya ardhi.
· Haki ya kila mwanamke kupata,kumiliki,kutumia na kuuza au kuigawa ardhi kuwa sawa na haki ya mwanaume yeyote kwa viwango na masharti sawa.
SHERIA ZA ARDHI ZA MWAKA 1999 NA SHERIA ZINGINE ZENYE MGUSO KATIKA ARDHI.

Maana ya ardhi

Ardhi ni ile inayojumuisha vitu vyote vilivyo juu na chini ya uso wa nchi vikiwemo majengo, uoto wa asili na maendelezo yote yaliyofanywa isipokuwa madini na bidhaa za mafuta na gesi.
Makundi ya ardhi
Ardhi imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:-
1. Ardhi ya kawaida/jumla: ni ardhi yote ya umma ambayo siyo ardhi ya hifadhi wala ardhi ya kijiji. Hata hivyo,
kwa mujibu wa sheria ya ardhi Na.4,1999 inajumuisha ardhi ya kijiji ambayo haikaliwi wala kutumiwa na wanavijiji. Kamishna wa ardhi ndiye msimamizi wa kundi hili la ardhi.
2. Ardhi Hifadhi: ni ardhi iliyotengwa kwa shughuli maalumu kama vile hifadhi za misitu, barabara, vyanzo vya maji nk. Kundi hili liko chini ya usimamizi wa mamlaka mbalimbali za aina ya ardhi husika.
matumizi kabla au wakati wa ya kipindi hicho
3. Ardhi ya Kijiji: hii ni ardhi iliyo ndani ya kijiji kilichosajiliwa na kubainishwa mipaka. Kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa (Mamlaka za Wilaya), ya mwaka 1982 na kuwa chini ya usimamizi wa Halmashari ya Kijiji.
Pia ardhi ya kijiji ni ardhi iliyotengwa chini ya sheria ya uundwaji wa vijiji,1965.Vilevile, ardhi ya kijiji ni ardhi ambayo si hifadhi, na kwa muda wa miaka kumi na miwili kabla ya sheria ya ardhi ya vijiji,
Na.5 kutungwa, wanakijiji wamekuwa wanaikalia na kuitumia kama ardhi ya kijiji na pasipo kuwepo na aina yoyote ya umiliki au matumizi kabla au wakati wa ya kipindi hicho.
MFUMO YA UMILIKAJI WA ARDHI

Kuna aina kuu mbili za umilikaji wa ardhi nchini Tanzania
· Umilikaji ardhi kimila: Huu ni utaratibu wa umilikaji ardhi kwa kufuata taratibu za kimila na desturi za jamii husika.
Aina hii ya umiliki hutumika katika ardhi ya kijiji kama ilivyobainishwa katika sheria ya ardhi ya vijiji Na.5,1999
· Umilikaji ardhi kwa Hati: huu ni utaratibu wa hati unaotumika na kutolewa katika kundi la ardhi ya kawaida/jumla.
Katika utaratibu huu mtu anaweza kumiliki ardhi kwa hati ya miaka 33, 66 au 99 na anakuwa na hadhi ya upangaji.
Upatikanaji wa Ardhi

Ardhi inaweza kupatikana kwa njia zifuatazo:-

i. Kurithi
ii. Kusafisha pori/eneo lisilo na mmiliki
iii. Kununua
iv. Kupewa zawadi
v. Kugawiwa na serikali.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Goodluck 全能神的僕人

Goodluck 全能神的僕人 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @RealHauleGluck

Jun 14
Comrade @TunduALissu tunaomba tueleze ni kwa mujibu wa Katiba au Sheria gani ardhi ndani ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ni mali ya wananchi?

🧵

👇🏻
Kipindi cha miaka ya 1961- 1990
- Mamlaka ya Gavana juu ya ardhi ilihamishiwa kwa Rais.
- Mwaka 1967 Azimio la Arusha lilitangazwa kuweka misingi ya uzalishaji mali mikononi mwa umma.
- Sheria zilizotungwa katika kipindi hiki ni pamoja na Sheria ya Utwaaji Na. 47 ya 1967 ambayo iliwezesha utwaaji wa ardhi kwa matumizi mbalimbali kama vile uanzishwaji wa Mashamba ya NAFCO na NARCO na Sheria ya Vijiji na Vijiji vya Ujamaa Na. 21 ya 1975
Read 9 tweets
Jun 12
#FactChecking: in 2017 Tanzania ended a 25-year-old hunting tourism deal with a United Arab Emirates company called ‘Otterlo Business Corporation’.
The deal, was set up in 1992 (President Mwinyi), was reported to be in exchange for millions of dollars to Tanzania’s armed forces.
However, despite the announcement in November 2017, OBC did not leave Tanzania. Just a few days later, Prime Minister Kassim Majaliwa said that OBC would stay.
Under the deal, Otterlo Business Corporation (OBC) gained exclusive hunting rights over an area of 400,000 hectares to the east of Serengeti National Park in Loliondo and Sale divisions of Ngorongoro District.
Read 14 tweets
Jun 9
For over a century, Tanzania's Maasai pastoralists have shared the famed Ngorongoro conservation area with zebras, elephants and wildebeests. But now they face the prospect of eviction as their exploding population poses a threat to wildlife according to the Tanzanian government.
#NgorongoroConservation: Since 1959, the number of humans living in the World Heritage Site has shot up from 8,000 to more than 100,000 last year. The livestock population has grown even more quickly, from around 260,000 in 2017 to over one million today.
Tanzania has historically allowed indigenous communities such as the Maasai to live within some national parks, but the relationship between the pastoralists and wildlife can be fractious, with animals attacking people and livestock.
Read 20 tweets
Jun 9
#UpinzaniNiMafichoYaCCM: ⚡️Vyama vya upinzani vilivyozaliwa mwaka 1992 na mwanzoni mwa 1993, dhamira ilikuwa moja tu; kuiondoa CCM madarakani na kuchukua dola.

Hoja zilikuwa sera mbaya na uongozi mbaya wa CCM. mwananchi.co.tz/mw/habari/kita…
Hata hivyo, kuelekea Uchaguzi Mkuu 1995, oksijeni ya vyama vya upinzani iliegemea kwa wahamiaji kutoka CCM.

Katika wapambanaji wa mageuzi 1992 na 1993 mwanzoni, ni Cheyo peke yake ndiye aliyejitokeza kwa kujiamini katika Uchaguzi Mkuu 1995,….
Uchaguzi mkuu wa kwanza kuhusisha vyama vingi vya siasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Cheyo aligombea urais kupitia UDP. Vyama vingine vilivyosimamisha wagombea urais 1995 ni Cuf na NCCR ambavyo wagombea wao hawakuwepo nyakati za mwanzo za vuguvugu la mageuzi.
Read 4 tweets
Apr 1
Dunia ya leo imejikita zaidi katika demokrasia. #Demokrasia kwa ufupi ni dhana inayolenga ushiriki wa wananchi katika kuweka misingi sahihi ya uendeshaji wa nchi wao wakiwa ndio msingi wa mamlaka yote ya nchi na walio na uwezo wa mwisho wa kuipa serikali madaraka na mamlaka yake.
Moja ya misingi mikuu inayolenga kukuza demokrasia ni Katiba ya Nchi. Katiba ni msingi mkuu wa uendeshji wa nchi, ukuaji wa demokrasia na utawala wa Sheria. Katiba ndiyo sheria kuu (mama) na ambayo kwayo sheria zote nyinginezo hupata uhalali na hufungamana na Katiba.
Katiba huweka bayana misingi ya utawala, vyombo vya utawala, na mgawanyo wa madaraka baina ya vyombo vikuu vya dola 👉🏽
Bunge, Mahakama na Serikali (Watendaji wakuu) Kubwa zaidi, Katiba ndiyo
inayoainisha nafasi waliyonayo wananchi katika kuweka utaratibu wa kuendesha nchi yao.
Read 23 tweets
Mar 29
#Jielimisheni: mchakato wa kupata Katiba Mpya Tanzania ulianza tangu mwaka 2010, wakati Rais wa wakati huo, @jmkikwete alipoamua kuutangazia umma dhamira na nia ya serikali ya CCM kuanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya.

👇🏻
Mchakato wa Katiba Mpys ukaanza rasmi mwaka 2011 kwa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 na baadaye ikatungwa Sheria nyingine ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitamka kuanzishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilianzishwa chini ya Waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba, ikaratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya Katiba.
Read 7 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(