Nimekuwa nikikutana na vijana mbali mbali everyday kuongea nao kuhusu biashara na ujasiriamali Vijana wengi wanadhani mafanikio ni kama kutuma 'SMS'. Kwamba unatype tu kidogo kisha unabonyeza SEND afu tayari. Ndo maana wamekuwa WALEVI WA BETTING.😂 Image
Ukweli ni kwamba mafanikio hasa katika biashara na ujasiriamali yanahitaji kupata MAARIFA sahihi ya kitu unachotaka kufanya. Kujiamini ni kuzuri lakini kudhani kuwa kujiamini kwako ndo kutaleta mpenyo kibiashara bila kuwa na maarifa sahihi ni kujitengenezea kachumbari ya disaster
! Biblia inasema Watu #wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA! Umeona ee?

So bila msaada sahihi UTAANGAMIZWA KIBIASHARA. Utasingizia biashara yako imerogwa na shangazi au na mpemba au shetani ameiinukia kumbe shetani yuko zake Brazil huko ni wewe tu huna maarifa sahihi.
(Shetani hana uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja...he is not #omnipresent).

Maarifa rafiki.

Kuwa mtu wa kufundishika. Itakusaidia.

Siku kadhaa zilizopita niliandika makala iliyosema ukitaka kufanikiwa kibiashara hasa unapokuwa unaanza basi epuka pesa za NDUGU,
MARAFIKI na MAJIRANI. Na nikaeleza sababu na kutoa mifano. Nashukuru iliwasaidia watu wengi mno kupata maarifa SAHIHI kuhusu eneo la wateja na sasa wanasonga mbele. Mungu ni mwema.

Maarifa ni muhimu usijiamini tu ukaishia hapo.
Wakati Yesu anasema wote watamkimbia na Yesu akijua kuwa Petro kwa kujiamini kwake atasema YEYE HATOFANYA HIVYO. Yesu akaona amsaidie Petro maarifa kiduchu ya kumsaidia. Akamwambia Simoni "Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano lakini nimekuombea wewe
ili imani yako isitindike"
(Luka 22:31 )

Lakini kwa kujiamini zaidi ndo hapo Petro akasema hatamwacha Yesu. Hata baada ya kupata information ambayo alikuwa hana.

Kumbe!

Yesu alitaka kumwonyesha Petro kuwa kujiamini kwako kutakwama tu mahali maana kuna vitu bado hujui.
Na kama huamini ngoja uone muda wa jogoo kuwika ukifika kabla hajawika utakuwa umeshanikana mara tatu wewe huyo huyo.

Kumbe shetani alikuwa na ruhusa ya kuwapepeta kina Petro na Petro hajui.

Kumbe Yesu alikuwa ameshamwombea Petro ili asiache njia na Petro hajui.
Ila anajiamini balaa!
Wakati hajui kinachoendelea.

UNAJIFUNZA KITU?

Kuna vijana ukikaa naye anakwambia mimi nataka kufuga kuku. Au kulima mananasi. Au kufanya biashara fulani. Lakini anaishia tu kujiamini sababu labda amepata mtaji wa pesa au ameambiwa inalipa au ameona
wanaoifanya wanapiga picha na hela mezani anadhani amemaliza kila kitu.

Au kwa sababu alifaulu Chuo kwenye masomo magumu anahisi hakuna ugumu tena zaidi ya ule.

Anahisi yeye noma.
Stress zikianza utaanza kujiona mjinga. Umeajiri watu bila kuwa na KNOWLDEGDE ya kutosha ya mambo.Unazama nao kwenye maji. Kiukweli inaumiza kuona mtu MZIMA na familia yake keshakufanyia kazi mwezi mzima halafu unaanza kumpa maneno ya kumfariji as if amefiwa.
Bila Petro kupata msaada wa kuombewa na Yesu imani yake ingetindika HAKIKA.

Ama bila kuokolewa pale majini alipoanza kuzama story yake ingeishia pale.

Msaada huwa upo tu always. Wachina wana msemo unaosema siku zote mwanafunzi akishakuwa tayari basi mwalimu huwa anatokea.
So....

Kama unataka kujifunza pia hasa kwa mtu unayeanza au ndo unataka kuanza kufanya biashara njoo tuongee. Hakika hutatoka bure. Utajifunza mengi ya kukufaa.
Biashara na ujasiriamali vinafanana na maisha ya ndoa tu in a way. Kuna dynamics zake. Watu husema "Usione Ukadhani". Yes, usione ukadhani. Confidence zako ni nzuri lakini ukifikiri kuwa ndo unachohitaji ili kudumisha ndoa unaweza kushangaa sana. Na ndivyo na ujasirimali ulivyo.
Unahitaji MAARIFA SAHIHI.

Confidence zilimliza Petro na akajifunza. Ujasiri wako ni kama puto. Lazima lifungwe kwenye uzi au kamba. Bila hivyo litapotea na upepo. Sawa unajiamini but jitahidi kupata maarifa (kamba) ufunge puto lako.
Usije kupata stress zisizo za lazima katika safari yako ya ujasiriamali na biashara bure kisa hukutaka kujifunza vitu muhimu.

Karibu sana kujifunza KAMA utakuwa interested. Mawasiliano NJOO DM IKO WAZI.
Good luck God bless you always!❤️
@threadreaderapp unroll this

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Badi 👴🏽

Dr. Badi 👴🏽 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @DrBadiBoy

Jun 26
Sisi watu weusi ni wavivu kwenye KUTAFITI vitu. Hivyo mtu mweusi amebaki na GENERAL KNOWLEDGE tu ya mambo yote muhimu. Mfano kuhusu uchumi, michezo, utawala, uongozi, biashara na uwekezaji, afya, hata mambo ya imani, mtu mweusi amebaki na GENERAL KNOWLEDGE tu.
Ufahamu wa jumla jumla tu. Hajui vitu in deep sababu hataki kujisumbua na kufanya utafiti. Mara nyingi general knowledge ina mchango mdogo sana kwenye mafanikio yako na wakati mwingine ina-mislead. Inapotosha.

Jiulize hivi mambo unayoyajua kuhusu maisha nani hayajui,
mfano eti kuna kupanda na kushuka. Nani hajui? Lakini hiyo knowledge imekutofautishaje na watu wengine.

But jiulize ni kitu gani HUJUI kuhusu maisha. Hicho ndo muhimu zaidi. Mambo yaliyo wazi sana kuhusu maisha yana mchango mdogo mno kwako.
Read 24 tweets
Jun 24
UNA NIDHAMU SAHIHI YA KAZI?
Ukisikiliza mtu anayetaka kuanza biashara huwa hawazi sana kuhusu kazi anawaza tu ATAFANYA hivi atafanya na hivi halafu wateja watakuja halafu atanunua gari halafu ataenda Ulaya😂.
Bila kujua utahisi wewe ni jembe kweli kweli kumbe una DELUSION. (Kama hujui maana ya hili neno Google tu utaelewa vizuri zaidi. Please do.) Yes watu wengi huanza na DELUSION. Mwisho kifo cha mende! Jichunguze kisha uone nini huwezi ili uajiri watu wanaokiweza uwalipe
UNA NIDHAMU SAHIHI YA MATUMIZI YA FEDHA?
Katika vitabu ambavyo natamani ningesoma enzi zile tunasoma THE RIVER BETWEEN basi ni RICH DAD POOR DAD! Nimekisoma baada ya kumaliza chuo na kuajiriwa. Yani wakati nimeshajenga nidhamu mbaya kabisa ya matumizi ya fedha.
Read 8 tweets
Jun 24
Kila wakati unawindwa, usichoke kua karibu na Mungu my dia
Nisikilize hapa..
Wachumba wawili walipanga kufunga ndoa baada ya uchumba wao wa muda mrefu, basi walienda kwa Mchungaji wao ili awaombee. Image
Basi mchungaji akiwa kwenye maombi alionyeshwa mtu fulani akileta zawadi mbaya na ilipofunguliwa tu wakafa hapo hapo. Mchungaji aliwapa taalifa izo wale wachumba, akawaambia waombe usiku na mchana ili MUNGU aangamize ilo tego.
Basi walianza kuomba muda uo uo, ilipofika usiku hakuna aliyelala wote walipiga magoti nakuanza kuomba.Wakiwa katikati ya maombi muda wa saa sita usiku mara walisikia mlango ukigongwa.
Basi mwanamke akainuka kwenda kufungua mlango, alipoufungua alishangaa kumuona rafiki yake
Read 7 tweets
Jun 21
Usisome makala hii ili kujifurahisha✍️

Unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake….
Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira, unashituka kuacha Ajira Yes kuacha watu wanaacha ,Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established.
Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya *kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja bado?
Read 10 tweets
Jun 21
Unatumiaje muda wako asubuhi hadi jioni. Una ratiba au kiholela tu.
Sikia
Kuna fursa nyingi tu za biashara zipo kila siku. Usipofanya kisa bado "unajipanga" it's up to you. Richard Branson (kama humjui Google kidogo) aliwahi kusema Kama mtu akikushirikisha fursa.....👇
halafu huna hakika kama waweza kuifanya basi SEMA NDIYO KWANZA kisha utajifunza jinsi ya kuifanya huko mbele ya safari".

So fursa zipo nyingi. Usipofanya maisha hayakusubiri wewe. Life must go on. Watu lazima wasafiri, wale, wavae, watume na kupokea pesa, wasuke na kunyoa....
Hawawezi kukusubiri wewe eti unajipanga. Life MUST go on. Wewe kama unajipanga wenzako wanafanya hizo fursa.

Tunaposema nchi zingine zimeendelea KIPIMO cha haraka haraka ni MIUNDOMBINU na HUDUMA ZA JAMII. Ninapoona leo nchi hii kuna #mwendokasi. Hata kama bado iko Dar es Salaam.
Read 11 tweets
Jun 20
UNAPENDA KUFANYA BIASHARA #LAKINI NI MANGAPI KATIKA HAYA UNAYAJUA KUHUSU BIASHARA?

Makala yangu mojawapo ilieleza AINA za biashara kuwa kuna biashara za aina mbili:

1. Zile zenye uwezo wa kukupa fedha tu
2. Zile zenye uwezo wa kukufanikisha kiuchumi ...
Nilifundisha tena kuhusu MITAJI. Nikasema hakuna mtaji mkubwa wala mdogo yaani hakuna biashara ya mtaji mdogo. Kila biashara ina mtaji kulingana na mahitaji yake na nature ya hiyo biashara. Na pia mtaji wa kwanza siyo pesa bali mawazo yako kichwani.
Nikazumgumzia kuhusu WATEJA nikasema ukitaka kupiga hatua hasa mwanzoni unapokuwa umeanzisha biashara basi epuka pesa na majirani na marafiki na ndugu. Yaani usilazimishe kuuza kwa hao na sababu nyingi nikatoa.
Read 6 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(