BARUA YANGU KWAKE 💔

Habari mpenzi.

Imekua kitambo kidogo. Natumai ujumbe huu utakukuta ukiwa mzima wa afya. Nimekua nikikuombea hivyo siku zote, pasi kujali ni nyakati za aina gani tumekua tukizipitia. Na hii ni kwa sababu naguswa na uwepo wako...

#UZI
... Nazifurahia nyakati zako nzuri na kuogopeshwa na nyakati ambazo huwa ni mbaya kwako. Zinaogogya zaidi kwangu kwa sababu huwa zinaniathiri pia. Na hii yote ni kwasababu ninakujali.
Nakumbuka siku ya kwanza tunakutana. Nilishindwa kukuzuia, ila nilitamani usiondoke. Nuru ya uso wako iliangaza mboni za macho yangu. Kila sekunde na dakika tulizokaa pamoja zilikua ni za thamani kwangu.
Naweza sema zilikua ni nyakati za dhahabu nilizoziota kwa siku nyingi na kutamani zitokee. Ulizileta, ulikuja nazo kama zawadi.
Sikuacha kukufikiria tangu ile siku. Hata nilipokosa nafasi ya kukuona nilitamani tukutane japo kwenye njozi. Au kama ingewezekana nipite tu nje kwako, utoke usimame nje na usiseme lolote. Nikuone nafsi yangu iridhike na kisha niondoke zangu.
Sidhani kama hili lingekua ni gumu kwako. Lakini niliogopa kujaribu. Kwa wakati ule kubeba tumaini ilikua ni bora kwangu kuliko kujihakikishia nafasi yangu kwako. Hii yote ilitokana hofu ya kukukosa endapo nisingeweza kukupata. Umtu kando ulinifaa zaidi.
Unakumbuka siku niliyokata shauri?
Nilijiuliza mara mbilimbili kama nina uhakika na ninachoenda kukifanya. Sikuwa na mashaka juu ya azma yangu, bali wasiwasi wangu mkubwa ulikua ni namna ambavyo wewe utanipokea na kulipokea jambo langu.
Pia sikuwa na mashaka juu ya utimamu wako.Kwa sababu licha ya kuja kuomba niwe kama nusu yako, tayari ulikwisha kutimia. Nakiri kuwa wewe ni mwanamke wa ndoto ya kila mwanaume
Ulinisikiliza, ukanielewa, ukanipokea na kunihakikishia kuwa niko salama nikiwa mikononi mwako. Na ni kweli, sikuwahi kujihisi salama zaidi kama wakati nipo kwako. Sitaki kuwa mchoyo wa fadhila, ulinifaa.
Siku zote ulikua mwema kwangu. Niliishi nikiwa kwako na akili yangu ilipoa
Kuna wakati niliwahi kujiambia kuwa kwa sasa haya mambo yanatosha na wewe ndiye utakaekuwa wa mwisho kwangu. Niufunge ukurasa wa kukimbizana, tutulie tujenge maisha yetu. Na hata nilipojaribu kukueleza juu ya haya yote ulionesha kukubaliana na mimi. Haukuwahi kunitia shaka.
Mpaka muda huu sielewi ilikuaje mpaka ukafika wakati nikawa nahofia hata kukuandikia ujumbe mfupi au kukupigia simu. Na hii sio kwa sababu nyingine. Ni kwasababu majibu yako yenye kuonesha kutokujali huwa yananiumiza zaidi.
..Ukanilazimisha nijifunze kutokujali pia, kitu ambacho kilikua ni kigumu na kitaendelea kuwa kigumu kwangu.
Umeniweka kwenye wakati ambao natakiwa nichague kuondoka au niendelee kuwepo. Nasikitika kukiri kuwa haya yote ni magumu kwangu. Nawaza maisha bila wewe lakini pia naumizwa kuendelea kukaa kwenye hii hali.
Nina hisia za kutokupendwa na kutokuhitajika, lakini nakosa uthibitisho kutoka kwenye maneno yako. Maneno yako ndiyo yanaweza kunitoa kifungoni nitaondoka kama ukitaka nifanye hivyo, lakini naomba unitamkie kwa kinywa chako kwanza.
Nimejaribu kukueleza uhalisia ulivyo. Lakini moyo na hisia zangu zinanieleza tofauti. Najipa matumaini kuwa nikupe muda huenda mambo yatakuja kukaa sawa. Lakini bado najiuliza nitasubiri mpaka lini?.. kwa sababu kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo mambo yanavyozidi kuwa mazito.
Kama kuna ukweli unaoshindwa kunipa kwa kuihofia hali yangu basi nakuomba unipe tu. Hata kama ni mchungu nitajitahidi kuumeza. Kama nilikuja kwako kwasababu ulinihurumia na sasa umegundua kuwa sikustahiki kuwa hapa naomba unijuze pia.
Nitoe kifungoni, nieleze ukweli niwe huru.

Ahsante.!

#BusaraZaBonge
4th July 2022.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Mr Bonge (#AbaaShots📸) /Mkama Said Khamis

Mr Bonge (#AbaaShots📸) /Mkama Said Khamis Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(