Hili jopo lote la viongozi waliopo kwenye picha hii na wengine wengi ambao hawapo pichani wote wanatumia magari aina ya Toyota Land cruiser V8.

Magari ambayo bei zake ni ghali na pia gharama za matunzo yake pia ni ghali, aidha hutumia mabilioni za fedha 🧵
za kodi za Watanzania maskini.

Wakati matumizi hayo ya hovyo na anasa yakifanywa na viongozi wa serikali ya @ccm_tanzania mamia kwa mamia ya watoto wa walipa kodi wanasomea chini ya miti kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa mashuleni.
Na kama haitoshi watoto wengine wa walipa kodi wanakaa kwenye mawe huku wengine wakikaa kwenye vipande vya tofali vilivyovunjika wakati wanasoma kutokana na uhaba wa madawati.

Haya mambo ya aibu yanatokea kwenye nchi ambayo ina miaka 61 tangu ipate uhuru wake.
Gharama za maisha zimepanda kwa wanchi ukizingatia kuwa Watanzania wengi bado ni maskini.

Mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu umekuwa mkubwa huku upatikanaji wa fedha ukibaki kuwa kitendawili.

Lakini pamoja na yote hayo viongozi wala hawana hata chembe ya huruma kwa wananchi.
Kinachothibitisha kuwa viongozi wamelewa madaraka na hawana habari na wananchi ni utitiri wa tozo zilizoanzishwa na serikali kwa kisingizio kuwa pesa zinazopatikana kupitia tozo hizo zinatumika kujenga shule na vituo vya afya.

Viongozi wanashindwa kutafakari
na kuamua kuchukua maamuzi ya kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima na kuziba mianya ya ubadhilifu serikalini ili kuokoa fedha zinazoliwa na watu wache ili fedha hizo ziwaletee wananchi ahueni wa maisha badala yake wanazidi kujaza matozo tu.
Viongozi hawa wa serikali pamoja na vilio vya Watanzania kuhusu tozo na gharama za maisha kuwaelemea lakini wao wameweka pamba maskioni wala hawasikii vile vile wamevaa miwani ya mbao wala hawaoni.

Wanawapita wanchi na kuwatimulia vumbi tu wakiwa ndani ya V8
Wanapulizwa na viyoyozi wakiwa wanawahi maofisini kugawana posho.

Je hawa viongozi wetu ambao ni wasomi kabisa hawawezi kutumia magari mengine ya bei za kawaida na zenye kutoa gharama nafuu katika uendeshaji wake tofauti na V8 ili kupunguza matumizi mabaya ya kodi za wanchi?
Hebu tujaribu kuangalia mzigo mzito waliobebeshwa Watanzania kutokana na matumizi ya magari aina ya Toyota Land cruiser V8 serikalini.

Bei ya Toyota Land cruiser V8 toleo la mwaka 2021 jipya 0km
Ni dola za kimarekani $100,124 bei ya awali na $100,124 bei kikomo sawa na shilingi za Tanzania Tshs 230, 239, 200M bei ya awali na Tshs 239, 945, 200M bei kikomo.

Haya tuchukue least price ambayo ni Tsh 230, 239, 200M kama mfano wetu kuwa ndio bei
ambayo serikali inatumia kuagiza kila gari moja ya Toyota Land cruiser V8.

Hii ndio orodha ya viongozi wa serikali wanaotembelea Land cruiser V8.

1. Rais 1 + 20 zingine kwenye msafara wake yani na za wasaidizi wake
2. Makamu wa rais 1 + 10 zingine za wasaidizi wake
3. Waziri mkuu 1 + 6 zingine za wasaidizi wake - 1
4. Mke/Mme wa rais - 1
5. Mke wa makamu wa rais - 1
6. Mke wa waziri mkuu - 1
7. Rais mstaafu - 1
8. Marais wastaafu - 1 x 4
9. Wake wa Marais wastaafu 1x5
10. Makamu wa raiswastaafu=?
11. Wake wa makamu wa rais wastaafu =?
12. Mawaziri wakuu wastaafu =?
13. Wake wa mawaziri wakuu wastaafu =?
14. Jaji mkuu - 1
15. Majaji wakuu wastaafu =?
16. Speaker wa Bunge - 1
17. Ma speaker wa Bunge wastaafu =?
18. Naibu Speaker - 1
19. Katibu mkuu kiongozi - 1
20. Makatibu wakuu viongozi wastaafu =?
21. Majaji wote Tanzania =?
22. Majaji wastaafu =?
23. Mawaziri wote - 33
24. Manaibu waziri - 33
25. Makatibu wakuu wote - 33
26. Wakuu wa taasisi zote =?
27. Waadhiri wakuu =?
28. Majenerali wa Jeshi =?
29. Majenerali wastaafu wa Jeshi =?
30. IGP - 3
31. Ma IGP wastaafu =?
32. Mkuu wa magereza - 3
33. Wakuu wa magereza wastaafu =?
34. Mkuu Jeshi la Zimamoto - 2
35. Wakuu wa Jeshi la zimamoto wastaafu =?
36. Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji -3
37. Wakuu wa Jeshi la uhamiaji wastaafu =?
38. Mkuu wa TANAPA - 2
39. Wakuu wa TANAPA wastaafu =?
40. CAG - 1
41. Ma CAG wastaafu =?
42. DCI - 1
43. Ma DCI wastaafu =?
44. Wakuu Mikoa zote =?
45. Wakuu wa Wilaya zote =?
46. Mabalozi wa Tanzania nje - 41
Huo msururu mrefu wa viongozi wanatumia Toyota Land cruiser V8 kwa makadirio ni viongozi 300.

Tujaribu kufanya hesabu ndogo tulikubaliana kutumia bei ya chini ya V8 ambayo ni Tsh 230, 239, 200M x 300 ya idadi ya viongozi.
Jibu linakuja Tsh 69,071,760,000B. Hapo hatujapigia hesabu gharama za mafuta na mategenezo 😇

Hayo mabilioni ya fedha ni kwenye magari, wala hatujaangalia ufujaji mwingine huko serikalini.

Je badala ya kuweka tozo za kila aina viongozi wakiacha
Matumizi ya magari aina ya Toyota Land cruiser V8 si wananchi watapata unafuu?

#KataaTozoo #KataaTozoo #KataaTozoo #KataaTozoo

Kwa pamoja tuungane kudai katiba mpya, @ccm_tanzania nchi imewashinda

#KatibaMpya #KatibaMpya #KatibaMpya #KatibaMpya
//MAREKEBISHO//
_________________________________
Bei kikomo kwa dola za kimarekani sio $100,124 bali ni $104,324, sawa na Tshs 239, 945, 200M. Natoa pole kwa wote mliopata usumbufu 🙏

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with 🇹🇿KATIBA MPYA🇹🇿

🇹🇿KATIBA MPYA🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(