Habari ndugu , karibu jamvini tuelezane kidogo juu ya uelewa wa jamii juu ya HEDHI na HEDHI SALAMA. Utakuwa nami Salome Mosha @Sally_mosha .
#ElimikaWikiendi

Karibu thread 👇..
HEDHI NI NINI?
Hedhi ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). Kitendo hiki hutokea kila mwezi kwa mwanamke huitwa mzunguko wa hedhi (Menstruation period).
#Elimikawikiendi
MZUNGUKO WA HEDHI NI NINI?
kipindi ambacho wanawake hutokwa na damu ukeni. Wanawake wengi hupata hedhi kila baada ya siku 28. Kwa baadhi ya wanawake huchelewa hadi 30. Wasichana wengi huanza hedhi katika umri wa miaka 12 wengine huanza katika umri mdogo au mkubwa
#Elimikawikiendi
HEDHI SALAMA NI IPI?
Hedhi salama ni ile yenye mzunguko imara usioharibika , kupata kiwango salama cha hedhi kisichopitiliza wala kidogo sana pia maumivu ya kawaida . Kutumia vifaa salama kwa ajili ya hedhi na namna bora ya kujisafisha na kutupa taulo zilizotumika kwa usalama.
UELEWA WA JAMII JUU YA HEDHI NA HEDHI SALAMA.
Mzunguko wa siku za hedhi kwa wanawake ni jambo ambalo huwa halizungumzwi hadharani katika jamii nyingi barani Afrika kutokana na imani za kidini na kitamaduni. Lakini tunapashwa kujua swala la hedhi ni salama la kiafya kwa mwanamke
Ni jukumu la kila mwanajamii wanawake kwa wanaume kujua hedhi na hedhi salama ni ipi kwa wanawake.Ushiriki wa wanaume katika suala la hedhi kwa msichana bado lina utata, baadhi wanaunga mkono na wengine wanapingana nayo na kuona kwamba ni suala la siri.
Swala la hedhi halipaswi kuwa siri tena kila mwanajamii anapaswa kujua juu ya elimu hii na kuona ni swala salama la kiafya kwa wasichana na wanawake hii itasaidia wanawake kujivunia kuwa katika siku zao na kutokuwa na hofu kabisa.Hii ni muhimu hata kwa afya ya akili kwa wasichana
CHANGAMOTO ZA HEDHI NI ZIPI.
1. HEDHI NZITO NA NYINGI.
Kupata hedhi nzito na nyingi kupita kiasi husababishwa na ukuta wa uterus kusisimka zaidi. Msisimko huu hutokana na wingi wa estrogen, inapelekea ukuta kumomonyoka kupita kiasi.
Tatizo hili linaweza kurekebishwa kwa kurekebisha lishe yako na kutumia tiba ya mimea kwa ajili ya kurekebisha homoni. Upungufu wa vitamin A na C inaelezwa kuchangia bleed nzito. unaweza kutumia virutubisho kama.
HEDHI KIDOGO NA MAUMIVU
Kama unapata hedhi nyepesi, nyekundu inaweza kuashiria kwamba mzunguko kwenye mfuko wa mimba ni mdogo. Unaweza kupunguza hali hii kwa kufanya masaji kwenye eneo la tumbo ukitumia mafuta ya mnyonyo, ama kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya moto.
2.KUKOSA HEDHI
Inaweza kutatiza pale ambapo unashika ujauzito lakini hupati hedhi kabisa. Kuwa na mzunguko mzuri ni hatua ya kwanza katika kujua kwamba unaweza kushika ujauzito. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuchangia hedhi yako kuvurugika kama;
msongo wa mawazo, lishe duni, uzito mdogo sana, kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kuvurugika kwa homoni, umri kwenda (kukaribia menopause) na matatizo mengine ya kiafya.
HITISHO
Swala la hedhi ni la wote kumekuwa na changamoto ya baadhi ya maeneo nchini wasichana wanashindwa kupata taulo za kike (pedi)kwa ajili ya kujikinga na hedhi ni muhimu kwa serikali na wadau kuangalia kwa upande wa pili upatikanaji rahisi wa taulo za kike.
#Elimikawikiendi

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Salome Mosha🇹🇿

Salome Mosha🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(