Paul_Makubi Profile picture
Mar 7 17 tweets 5 min read
SIRI AMBAYO BENKI NA MICROFINANCE HAWATAKI UIJUE KUHUSU MIKOPO NA RIBA

Ukitaka kukopa Pesa kitu cha Kwanza kufahamu ni RIBA. Je Riba ya hiyo taasisi ni kiasi gani pia ni kwa muda gani, na aina gani.

Nitaeleza jinsi ya kuchambua RIBA kwa muda.
Na mambo mengine muhimu.
Taasisi Nyingi hasa Bank wana RIBA ya 16-18% kwa mwaka moja.

Ila kwa Microfinance Bank RIBA zinatofautiana Sana baadhi ya hizi taasisi wanaweka Riba ya asilimia 4-5 kwa mwezi.
Hichi ni kiwango kikubwa Sana kwa mtu wa kipato cha chini ukipiga
Kwa mwaka ni 48-60% Moto huu🔥
Tuchukue RIBA ni 18% kwa mwaka Basi gawanya kwa miezi 12 iliufahamu kwa mwezi moja RIBA ni kiasi gani. Kawaida Tunaona RIBA ni 1.5% kwa mwezi moja.

Baada ya kujua RIBA hapo ndipo utafanya maamuzi.

Kwa wepesi zaidi tumia hii kanuni
I=P(1+RT)
Wakati unakula madini haya Nifollow pia Retweet Nawengine wapate uelewa huu.
Kama tayari Basi tuendele
Wateja wengi wakiambiwa RIBA ni 18%.Wenyewe wanajua ukikopa 10M maana yake unalipa ((10M + 18% ya 18M) kwa muda wote wa marejesho kitu ambacho sio kweli.

malipo ya mkopo yanategemeana na Muda na sio tu kiasi cha Riba Kama watu wengi wanavodhani
Pia ni vizuri kumuuliza afisa mikopo kwamba huu Mkopo wenu je niwa aina gani?
Reduced interest rate.
Flat interest rate.

Ukisikia anakuambia tu ni Flat rate Kama unauwezo wa kukimbia kimbia maana sikushauri mikopo ya aina hii.
Reducing rate Ni kuwa Riba inapungua kadri unavokuwa unakaribia kumaliza Deni lako hii ni nzuri Sana kwa Wakopaji japo Taasisi nyingi wanairuka.

Flate rate/ Costant rate Hii inakuwa Riba yako haibadiliki inakuwa costant mpaka pale utakapomaliza Deni lako. Huu ni Mwiba
Baada ya Kujua MIKOPO ya muda mrefu na muda mfupi , nashauri chukua mkopo wa muda mfupi kwakua unakuweka huru mapema
Ukizingatia na yule wa muda mrefu.

Riba kwa mwaka 18% gawa kwa 12 utapata kwa Mwezi ni 1.5%.

Chukua mkopo wako mfano mill 6 kwa miez 6 utalipa. Mill 6.540 tu.
Kama bado ujanifollow ni follow then retweet ili upate nyuzi zangu kwa urahisi . Kama tayari Basi tuendele
MIKOPO ya muda mrefu ina RIBA kubwa tuseme kwamba

Unataka mkopo wa million 10 rejesho miaka 5 na Riba Ni 18%

Hapa kwa miaka 5 yote utalipa
Mill 19. nawewe ulikopa mill 10.
Unakuwa umelipa mkopo mara mbili. Hasara Hii

Nimekuwekea formula hapo ya kucalculate
Kama unashidwa kucalculate RIBA Kuna website Kama.
calculator.net/loan-calculato…

bankrate.com/loans/loan-cal…
Zitakusaidia kujua kiwango Cha RIBA katika MKOPO wako ila. Ukitaka kufahamu zaidi tafuta wahusika wakusaidie

Naona @CRDBBankPlc @azaniaBank_ltd na wengine wana online calculator
Nashauri pia kama utataka mkopo wa muda mrefu tafuta Taasisi yenye RIBA nafuu tafuta Taasisi nyingine ili uweze kuuza Deni lako kwa Taasisi hiyo ili kupunguzia Mzigo wa marejesho
Au kushindwa kulipa kabisa mkopo wako na kufilisiwa.
Na Kama ulishachukua mkopo wa Muda mrefu kwa RIBA kubwa ambayo unaona inakuumiza itakubidi utafute sehemu wanayotoa MIKOPO kwa RIBA nafuu na uweze kuhamisha deni
kutoka Taasisi moja kwenda Taasisi nyingine.
Pia kwenye kutafuta unafuu wa mkopo kuna gharama za kufanyika kwa mkopo wako (loan processing fee)
Taasisi zenye RIBA kubwa wanakuambia ukiomba MKOPO mfano wa Million 5,
Wanakupa yote Million 5 ila nyuma ya pazia Kuna processing fee lazima utailipia Tu.
Tunakuja kwa Taasisi nyingine hizi ukiomba mkopo mfano million 5 watakupa million 4.9 wanakata na (processing fee) na sometimes inaweza chukua hata siku 2-3 au wiki/mwezi kupata mkopo wapo.
Watu wengi Wanaingia kwenye mikopo mikopo kwasababu ya shida na uharaka wa kutatua mambo yanayowasibu kwa uharaka lakini wanakosa uelewa wa undani kuhusu uendeshwaji wa Mikopo na Makato na jinsi ya kurejesha.
Kwa hiyo mda mwingine RIBA inakuwa kubwa kwa sababu ya kutaka mikopo ya haraka 24hrs na shida zako mwenyewe kingine ni kutokufanya utafiti kuhusu MIKOPO hapo ndipi RIBA inakuwa kubwa na unajikuta unalipa Deni usilostahili.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Paul_Makubi

Paul_Makubi Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(