Herode the 3rd. Profile picture
lets talk business @Tz Entrepreneur Development, Mkulima na Mfugaji, CEO at Tanzania ECO-FARM.
Jan 16, 2022 27 tweets 10 min read
MY LIFE EXPERIENCE JUU YA MAISHA YA KUJIAJIRI.

Mwaka 2010 Nilianza chuo SAUT, Mwanza campus, BSCP. Katika mazingira ya kipindi kile niliona fursa ya kufanya biashara ya kuuza nguo za mtumba za kiume. Hii ilinivutia sababu hakukuwa na wauza nguo za mituba maeneo ya Image Chuo. Sikuwa na mtaji mkubwa bali nilianza na 350k ambayo ilikuwa ni sehem ya boom langu. Nilinunua baloo la mashati ya kiume na nikayanyoosha vizur. Zilikuwa shati kama 200. Baada ya masomo jioni nikawa nazunguka kwenye hostel za boys nawauzia kwa bei ya 5k-7k.