Hilda Newton Profile picture
Journalist/Activist/President Of Tanzania 2045
May 16 5 tweets 8 min read
‼️UKWELI KUHUSU BUYOBE, KWENYE SAKATA LA KUTEKWA MSHABAHA.‼️

Shuka na Thread hadi mwisho👇

Nakumbuka January 15, 2026 Buyobe alinitumia namba yake DM akasema nimchek WhatsApp kuna issue tuongee, nilimchek tukaongea.

Alinielezea jinsi alivotekwa na kikosi cha Mafwele, walimvotesa n.k pia alishukuru kwa jinsi tulivompazia sauti.

Katika maongezi hayo aliniambia kwamba pamoja na kwamba ameachiwa kwa dhamana bado watekaji wa Mafwele wanaendelea kumfuatilia hivyo maisha yake yapo hatarini , nilimwambia achukue tahadhari maana hao watu hawana masihara, akasema anafikiria kuondoka nchini, nikamwambia ni wazo zuri, akaniambia kama kuna Taasisi yoyote ambayo naijua inasaidia watu ambao wanachangamoto kama yake nimuunganishe nayo, nikamwambia hakuna Taasisi yoyote ambayo naijua so tukaishia hapo.

Baada ya siku kadhaa alinipigia simu akaniambia, kwamba yupo mahali nilipo anaomba tuonane, tusalmiane na kufahamiana maana hatujawai kuonana zaidi ya humu mitandaoni, nikamwambia kwasasa siwezi kuonana nae kwasababu za kiusalama, nikamwambia kukiwa shwari nitamtafuta mimi mwenyewe, tukaishia hapo.

Baada ya hapo alimpigia simu @Twaha_Mwaipaya akamuomba waonane, Twaha alinipigia simu kuniuliza kama namfahamu, nilimjibu Mwaipaya kwamba simfahamu zaidi ya kumuona online hivyo Mwaipaya na yeye akamkwepa badae akampigia simu @Sativa255 kumuomba waonane.

Baada ya issue ya Mshabaha kutekwa ndo nikajua kwamba kumbe wakati anawasiliana na mimi kuniambia habari za yeye kuondoka nchini kuna mtu mwingine ambae alimshirikisha huyo mtu ndo alimuunganisha na @lifeofmshaba ili amsaidie kutoka nchini kwasababu alisema vijana wa Mafwele walikuwa bado wanamuwinda.

Alifika Nairobi akapokelewa na @lifeofmshaba na kupelekwa mahali pa kuishi, muda wote alikuwa akidai kwamba anaumwa shingo, kichwa na miguu lakini pia alimwambia Mshabaha vitisho vya Mafwele kusema kwamba atamfira + kuonana na watekaji live ni vitu vilimuumiza sana kisaikolojia hivyo alitafutiwa Mwanasaikolojia lakin alipoambiwa aende Hospital kufanya checkup ili wajue Polisi wamemuumiza kwa kiwango gani ili apatiwe matibabu alikataa.

Muda wote wakati Buyobe yupo Nairobi. Mshabaha alikuwa anakwenda kwake kumjulia hali kutokana na madai ya changamoto yake ya afya alokuwa nayo.

Siku ya tatu, Buyobe alimpigia simu Mshabaha akamjulisha kwamba, nyumban kwake kuna mgeni ambae na yeye kalazimika kukimbia Tanzania kwasababu Mafwele anataka kumuua akaenda mbali zaidi akamdanganya kuwa mgeni huyo ni Mwanachama wa CHADEMA wakati si Mwanachama wa Chadema.

Mshabaha alifika mahali alipokuwa anaishi Buyobe akamkutana huyo mgeni ambae Buyobe alimtambulisha kuwa anaitwa Aidan Msuya ni rafiki ake wa miaka mingi.

Buyobe alimdanganya Mshabaha kwamba Msuya alikuwa Diwani wa Chadema wa Ubungo huku akijua fika kwamba Msuya hajawai kuwa Diwani.

Mshabaha alimuliza ndani ya CHADEMA anamfahamu nani Buyobe akasema @ExMayorUbungo na Hilda Newton japo kwasasa Msuya hana mahusiano mazuri na Bony.

Ili Mshabaha amuamini zaidi Msuya, Buyobe akamdanganya Mshabaha kwamba Msuya ni boyfriend wa Hilda Newton wakati huo anajua fika kwamba mimi na Msuya hatufahamiani kabisa.

Mshabaha alimwambia kama anamahusiano na Hilda mpigie simu, Msuya akasema hapana itamletea shida, maana amekuja hajajipanga Mafwele amefunga account zake zote za Bank na kama girlfriend wake, akijua yupo Nairobi na akashindwa kumuhudumia itakuwa aibu sana kwake, haya ni maswali walikuwa wanajibu Buyobe na Msuya kwa pamoja na kwasababu walijua wanasema uwongo, wakamuomba Mshabaha asiniambie chochote so Mshabaha akakausha.

Huo ndo ukawa mwanzo wa Mshabaha kumfahamu Msuya ikawa kila akienda kumuona Buyobe anamkuta Msuya kuna wakati walikuwa wanaenda kula pamoja, Mshabaha hakuwa na wasiwasi na Msuya kwasababu ya Utambulisho ambao alipewa na Buyobe, aliamini ni mtu Genuine.

Buyobe akatoa wazo wapate gari maana na hali yake ya kiafya na usalama ni muhimu wakawa na gari, mara wazo likawa linafanyiwa kazi na Msuya.

Part 2 inaendelea hapa 👇Image Mshabaha anasema mpaka muda huo, kuna mambo mengi yalikuwa yanaanza kwa Buyobe then yanatekelezwa na Msuya.

Kabla ya tukio la Mshabaha kutekwa siku nne nyuma Buyobe na Msuya walimtembelea mzee mmoja wa Kenya, kisha wakamtumia picha Mshabaha kwenye picha yuko Buyobe na Msuya na huyo mzee na mkewe wake.

Wakasema ni mwanaharakati ambae ana knowledge kubwa, kwasababu Mshabaha nae ni Mwanaharakati waliona ni muhimu Mshabaha akaenda kuonana nae kuna mambo atajifunza.

Mshabaha akakubali hivyo wakakubaliana kwamba watapanga siku waende.

Lakini pia Buyobe na Msuya walimueleza Mshabaha kwamba wangependa kufanya training kwa Wanaharakati wote wa Tanzania walipo Nairobi, Mshabaha aliwakatalia na kusema hawezi kuwatafuta watu na kuwakusanya kwasababu ni risk.

Msuya alipoona Mshabaha amekataa mambo ya training akamuomba amkutanishe na Hilda, Maria, Sativa, na Mwaipaya, Mshabaha alikataa mind you huyu mtu ambae anamuomba Mshabaha amkutanishe na mimi, kwenye utambulisho wake alisema kwamba mimi ni girlfriend wake,😂😂😂

Walipoona mpango wao wa kutaka kukutanishwa na watu ambao wanawawinda, umeshindikana ikabidi wamkomalie Mshabaha ili waende nae kwa yule Mzee Mwanaharakati wa Kenya ambae walikubaliana kwamba wataenda nae.

Ikumbukwe Msuya na Azizi walikuwa wanaishi nyumba moja, Buyobe alikuwa anakwenda kwa Msuya ambapo Azizi alikuwepo na ilikuwa ikifika usiku wakati mwingine Aziz alikuwa anakwenda kulala kwa Buyobe na wakati wote huo Buyobe alikuwa anatumia line ambayo imesajiliwa kwa passport ya Aziz.

Hata usiku wa kuamkia siku ya tukio la utekwaji, Azizi alilala kwa Buyobe so wakati wanaenda kwenye utekaji Azizi alitokea kwa Buyobe, Buyobe alipoulizwa ilikuaje akawa anaishi na watekaji, alijitetea kwa kusema kwamba eti alikuwa analala kwa kujifungia chumbani eti hiyo ndo ilikua pona yake.

Sasa tuje siku ya tukio la Utekaji, wakati wanatoka hiyo asubuhi Buyombe alihairisha safari, akawambia Msuya waende tu wenyewe na Mshabaha,wakati huo Mshabaha alijua wanaenda tu kumuona huyo Mzee Mwanaharakati then watarudi

So walikutana sehemu inaitwa China center maeneo ya Kilimani, wakaingia kwenye gari binafsi ambayo Msuya aliikodi, wakaingia Petrol station wakajaza mafuta, kisha wakaanza safari.

Ndani ya gari alikuwepo Mshabaha, Aziz, Msuya na Wakenya wawili, wakiwa njian Msuya aliomba kushuka ili achimbe dawa baada ya Msuya kushuka tu Dereva akakanyaga mafuta so ndani ya gari kukawa na taharuki hapo ndo Mshabaha akaanza kupambana na Aziz na Mkenya wa Africa Kusini, wakaanza kumkaba huku wanamnyeshwa vitu na kujaribu kumchoma sindano muda huo gari ilikuwa speed,

Mshabaha alifanikiwa kufungua mlango wa mbele, akaukanyaga ili usijifunge wakati huo alikuwa anavutana na Azizi huku gari ikiwa kwenye mwendo.

Wakasimama kufunga mlango, Mkenya akashuka lakin kabla hajafunga mlango watu wakiwemo bodaboda wakawa wameshajaa, walipoona nyomi yule Mkenya akarudi haraka kwenye gari, Dereva akawa anaondoa gari kabla hawajaondosha gari vizuri Mshabaha akaruka.

Ndipo Wananchi waliokusanyika eneo hilo wakaanza kumpatia huduma ya kwanza Mshabaha na kuwapigia Polisi na kuwapa details za iyo gari ndipo Polisi walianza kukimbizana na hiyo gari, akina Aziz walipoona mitutu wakasimama na kukamatwa, kisha wakapelekwa kituoni ambako walijaribu kuhonga milioni 10 ya Kenya lakin Polisi Kenya walikataa.

Mwisho walifikishwa Mahakaman kesi Inaendelea.

Baada ya hili tukio ndo simu zikaanza kutembea, badae Mshabaha alivotoka Hospital akanieleza kuhusu huu mkasa wote ndipo akanitumia picha ya Kiongozi wa watekaji (Msuya) akaniuliza kama namfahamu, nikamwambia Hapana simjui labda ngoja tumpost mitandaoni lazima tutapata tu mtu/watu ambao wanamjua.

Ndo hapo Mshabaha akaanza kushagaa kwamba inakuaje mimi simfahamu huyo mtu wakati Buyobe alimuaminisha kwamba mie ni girlfriend wa huyo Msuya, Binafsi nilishangaa sana kwanini Buyobe aliamua kunisingizia jambo la uwongo?

Ndo hawa kwenye hii picha hapa

Inaendelea part 3👇