Hilmi Hilal Profile picture
An activist. I fight for; The Sovereignity of Zanzibar & Tanganyika. Rights and justice of Zanzibaris & Tanganyikans. Democracy. I'm a proud Zanzibari.
May 19, 2021 7 tweets 2 min read
JAMHURI YASHINDWA RUFAA DHIDI YA UAMSHO

Hukumu ya rufaa ya Jamhuri dhidi ya Masheikh imesomwa leo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Majaji watatu wa Mahakama hiyo wametupilia mbali rufaa ya upande wa Jamhuri ya kutaka mashta 14, dhidi ya Masheikh yaliyofutwa na Mahakama... Kuu ya Tanzania yarudishwe.
Katika Mahakama hiyo leo Mawakili 9, wanaowatetea Masheikh na wanasheria 11, wa upande wa serikali walionekana wakisikiliza kwa umakini mkubwa wakati hukumu hiyo ikisomwa.
Mahakama ya rufaa imeitupa rufaa ya Jamhuri kwa hoja iliyotokana na pingamizi...
Nov 2, 2020 5 tweets 4 min read
USHENZI ULOFANYWA ZANZIBAR

Hivi ndivyo alivyoungua Bibi yangu. akisimulia dada mmoja na machozi yakinilenga.

Ilikua majira ya saa 2 asubuhi Oktoba 27, 2020, Unguja, maeneo ya Garagara Mtoni Kidatu.

Mara ghafla nyumbani kwetu askari wengi wemejazana mlangoni. Wanagonga...🧵 mlango kwa kishindo kikubwa huku wakisema "Fungua Fungua" tupo nyumbani mimi, ndugu zangu, mama na Bibi yetu ambae ni mgonjwa ana stroke.

Mara mama akajibu "hatufungui Mlango".

Askari wakajibu "Nasema fungua" dozen ya Askari mlangoni mara malango ukavunjwa.

Wanaingia ndani...