Martin Maranja Masese Profile picture
MMM | Full-time Father | Public-spirited | Sperm That Won The Race, ME | Think Deep Don’t sink | Cogito, ergo sum |
#MZINDAKAYA🇹🇿 Profile picture Mobam🐦 Profile picture WalasInc Profile picture Alison Urnini Profile picture LewangaCM Profile picture 9 subscribed
Aug 8, 2023 68 tweets 12 min read
“Martin Maranja Masese’s open letter to Samia Suluhu Hassan”

Dear madam president, HE. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania

As-salamu alaykum! Image Madam President, I am honored to be writing to you about issues that are important to our country’s interests. Writing to you directly instead of starting with your assistants may seem unfair since the President is an institution. But, I decided to write to you straight away.
May 15, 2023 6 tweets 2 min read
Unaagiza MZIGO wa nguo wa TZS 43,200,000/- unalipa kodi TZS 26,892,000/-.

Mfanyabiashara kurejesha faida yake atapaswa kuuza mzigo bei gani ili alipe kodi na tozo nyingine?

Waziri wa fedha na Mipango, @mwigulunchemba1 lengo lako ni kodi katika kila kitu katika eneo moja? ImageImage . @TRATanzania wanafanya hivi miaka yote, hapo bado TBS, service levy 0.3% ya mauzo (haijalishi umepata faida) bado gharama ya usafirishaji kutoka bandarini ambayo ina kodi kibao... Yote hii ni uvivu tu wa kufikiri, wanakamua wachache badala ya kuongeza tax base ili kodi zipungue
Apr 28, 2023 20 tweets 4 min read
MSEMAJI wa serikali anasema @Nnauye_Nape na wizara ya Habari wanashawishi Instagram kuleta ofisi Tanzania. Ofisi za Instagram za kazi gani @MsigwaGerson? Tumieni akili ndogo mlizonazo kushawishi Volkswagen, Mercedes-Benz, Ford, Jeep, Hyundai, Honda, BMW, TVS wafanye assembling TZ ImageImage Mfano, gari zilizoshushwa kutoka katika meli ya mizigo 9 April 2022 katika bandari ya Dar es Salaam, gari 1,105 (sawa na 27%) ya mzigo ulioshushwa bandarini zilibaki Tanzania na gari 2,936 (73%) zilikwenda nchi jirani (Sudan, Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia).
Mar 17, 2023 66 tweets 11 min read
"JPM ALICHELEWA KUWA RAIS WETU. NDIYO"

Tulitakiwa kuwa na JPM kabla ya miaka 20 iliyopita. JPM alichelewa kuwa Rais wetu kwa katiba ya kifalme/kisultan tuliyonayo. Miaka 5 na miezi 5 ilituonyesha rangi za udikteta. Ingawa rangi hiyo haikufika kwa mtu mmoja mmoja, wapo walioguswa Bado tulihitaji kuwa na JPM kwa miaka mingi au tuseme kwa lugha rahisi kabisa, JPM alichelewa kuwa Rais wetu. Ndiyo. Kabla ya JPM, kuna masuala mengi ya hovyo hatukuwahi kuyaona au kupitia katika siasa za nchi yetu, lakini katika uwepo wake tumeona masuala mengi ya kuogofya.
Nov 7, 2022 6 tweets 2 min read
“Shujaa Mvuvi — Muokoaji”

Majaliwa Jackson (Maja Munyama), mvuvi wa dagaa anasema alipoona ndege imetua ndani ya maji (kutoka upande wa Kyaka) isivyo kawaida, kwa kuwa ilikuwa asubuhi, saa 8:53 EAT, aliwasanua wenzake waliokuwa na mtumbwi mdogo, walipiga kasia hadi kwenye ndege. Majaliwa anasema alipofika kwenye ndege, alikuta watu wakijadili jinsi ya kuingia ndani kutoa msaada, lakini mlango umejifunga (locked). Majaliwa akatumia kasia yake, akapiga, mlango ukafunguka, watu wakaanza kuokolewa kupitia mlango huo. Majaliwa akahamia upande wa rubani.
Oct 10, 2022 61 tweets 10 min read
“Letter to the president of the United Republic of Tanzania”

Dear madam president, HE. @SuluhuSamia

How are you doing? Image These are my quarterly (4th quarter, 1 October–31 December (92 days) greetings to U & yours as well. We prayed 2022 to be a better year for all of us, the year in which we (would) refined ourselves, because it was another year of struggle for existence as always. Let’s talk now!
Oct 9, 2022 25 tweets 5 min read
"MAKUBALIANO YA FEDHEHA"

Julai 2019 Barrick Gold corporation ilinunua kampuni ya ACACIA Mining Plc kwa $428M. Hii ni baada ya mjadala wa muda mrefu kati ya BARRICK na ACACIA takribani miezi 5 ya mazungumzo BARRICK na ACACIA wakakubaliana thamani ya kampuni ya ACACIA ni $951M Awali majadiliano kati ya serikali na BARRICK yaliyofanyika Tanzania yaligomewa na ACACIA na wanahisa wengine wa ACACIA ambao wanamiliki karibu 36% ya hisa zote za ACACIA. Serikali iligoma kwenda mezani na ACACIA, wakaamua kukaa na BARRICK Gold Corporation
Oct 7, 2022 66 tweets 9 min read
Jaji anaingia mahakamani saa 9:30 asubuhi...

Watu wote mahakamani wanasimama....

Kesi namba 36/2022, Halima James Mdee na wenzake V/s CHADEMA inasomwa leo Ijumaa October 4, 2022 hapa Mahakama kuu Mbele ya Jaji Cyprian Mkeha..

Mh Jaji: karibuni... Anasimama Wakili wa Serikali...

WS: Mh Jaji Naitwa Kipilinga Panya nipo pamoja mawakili wasomi..
Aliko Mwamanenge
Emanuel Ukashu
Edson Kilatu
Matinde Wankashu

Kwa pamoja tuwawakilisha waleta maombi Halima James Mdee na wenzake kumi nane..
Sep 7, 2022 6 tweets 2 min read
. @JMakamba Tatizo ni kanuni za EWURA, Sheria ya mafuta, EWURA au Wizara?

Kituo cha Mafuta Mvumi Mission, Chamwino, Dodoma, leo asubuhi bei ya Mafuta ni Sh.3,475 kwa lita ya petroli.

@EwuraTanzania wametoa bei kikomo lita ya Petroli ni Sh.3,023 Chamwino, Dodoma kuanzia 7/9/2022 Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zinapangwa na soko lenyewe. EWURA Jukumu lao litakuwa ni kuhahamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta kwa kampuni za mafuta ambazo zipo 39.
Sep 5, 2022 4 tweets 1 min read
Bashungwa anasema vituo vya afya 234 vimejengwa kwa tozo. April 4,2019 walitueleza Magufuli amejenga 352. Hotuba ya Magufuli bungeni 2020 walisema wamejenga vituo 487. Sept 2021 wakasema Samia wamejenga vituo 220 kwa tozo. Mkopo IMF kwa ajili ya COVID-19 $567.25M mlipeleka wapi? Ukiacha kwamba kukopa ili kutengeneza madawati ni jambo la hovyo. Fedha za IMF mlizipeleka kwenye jukumu ambalo siyo lake. Madawati na Madarasa sio kazi ya mikopo ya IMF. Hizo ni kazi kimaendeleo chini ya WB. Tanzania iliomba fedha IMF kukabiliana na dharura ya COVID-19.
Sep 1, 2022 15 tweets 3 min read
February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa jimbo la Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao 'nyumba ilikosa umeme'. Zilitengwa $5M. Umeme ulikatika kati ya saa 3-20. Huku kwetu, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks etc hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara yao?
Aug 17, 2022 10 tweets 2 min read
Zambia walichagua bilionea wao kuwa Rais. Hakainde Hichilema, HH - “Bally”, Wanamuita “cattle boy” anatajwa kuwa bilionea mkubwa Zambia. Anamiliki ranchi nambari mbili kwa ukubwa nchini Zambia. HH ana utajiri wa zaidi ya US$389M. Wengine tukomae na “watoza ushuru” wenye vilemba. Hakainde Hichilema ni MFUGAJI mkubwa,pia anafanya shughuli za kilimo cha mahindi. Hichilema anashika nambari mbili nchini Zambia kwa kusafirisha nyama baada ya ZAMBEEF. Anasema alianza na ng’ombe 6 na sasa anao ng’ombe zaidi ya milioni 5.
Jun 14, 2022 7 tweets 2 min read
Mzee @MsigwaPeter anasema Maasai siyo wazawa. Tukubaliane naye. Msigwa ni mhehe wa Iringa, Je wahehe ni wazawa wa Iringa au tumpe darasa mchungaji? Hawa ni wabantu. Shina la Wahehe linaanzia kwa mtu aliyeitwa Mufwimi (yaani Mwindaji), simulizi zinaeleza alitokea Ethiopia. Mufwimi alipita akiwinda kutoka Ethiopia, Kenya kabla ya kuingia Tanganyika na kujikuta yupo Usagara na hatimaye eneo la Nguluhe-Dabaga akipitia Ikombagulu, himaya ya Chifu Mwamududa ambaye alikuwa akitawala kabila la Wakombagulu, lililokuwa na watu wachache.
Jun 5, 2022 5 tweets 1 min read
Siku nilikamatwa na polisi mahakama ya mwanzo Tarime. Nikapelekwa mahabusu. Nikatunzwa siku 12. Nikasafirishwa DSM nilipotunzwa siku 11. Tarime mahakamani siku nakamatwa, hakuna aliyejitikisa kunipambania. Moyoni nikajisemea “ni kiherehere changu kujifanya Ernesto ‘Che’ Guevara” Baada ya kupewa dhamana nikatakiwa kufika kituo cha polisi mara 2 kwa kila siku 7 miezi 3 mfululizo. Mara zote nikiwa njiani naona watu wapo bizee na biashara zao. Nikawa najisemea “kujifanya Stokely Carmichael kunaniponza, walimwengu hawana habari wanaendelea na shughuli zao tu”
Jun 1, 2022 17 tweets 3 min read
JPM pamoja na uharibifu na ukatili wake alikuwa ni fursa. Wakati wote nasema, JPM alichelewa kutawala ardhi yetu. Nimeeleza. Alitusaidia mambo mengi kwa kutumia udikteta wake. Tulishughulikiwa na kuimarika sana. Tukashikamana na kuwa imara. Tuliwafahamu hadi matapeli ndani yetu. Ni ukweli dhahiri. Ni tabia za binadamu wote. Kadiri anapoumizwa ndivyo anavyochukizwa. Ni kama alivyo mnyama Paka. Ni kiumbe mpole sana. Huwezi kumuona akigombana na wenzake hovyo. Lakini ukimfungia chumbani, ukampiga, utaona upande wake wa pili. Wataalam wanaita “Apathy spirit”
Jun 1, 2022 7 tweets 1 min read
Nimekumbuka makala ya “Collective Imbecilization” Profesa Chachage imeandikwa na Jenerali Twaha Ulimwengu….

Neno “Imbecilization” usilitafute katika kamusi ya kiingereza kwa kuwa hilo ni neno alilotengeneza Profesa Seithy Chachage mwenyewe. Alikuwa binadamu akili nyingi. Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile ingewezekana kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo, ukafunga madirisha na milango, kisha ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea sawasawa,
May 31, 2022 10 tweets 7 min read
Mwaka 2013 Club Billicanas ilifunguliwa baada ya ukarabati wa gharama kufanyika. Ilikuwa ni uwezo wako wa kunywa/kula siku hiyo. Freeman Mbowe alilipa bili zote. 2015 anaingia mwendazake madarakani, anaanza vibweka, 2017 BILLZ inavunjwa kwa unyama. Mwendazake alikuwa katili sana. Picha ya kwanza Club BILLZ ikiwa na uhai wake. Show kubwa za wasanii wa ‘bongo fleva’ zilifanyika hapo. Frame ya pili ni baada ya Club Billicanas kubomolewa kwa hila tu, sababu nyingi zikiwa za kisiasa. Watu wengi wakakosa ajira. Eneo hilo sasa ni parking tu ya magari. Roho mbaya
May 23, 2022 10 tweets 2 min read
SINOHYDRO Corporation LTD wamepewa zabuni kujenga mradi wa mwendokadi BRT-3 Gongo la Mboto-Kariakoo (23.6km) kwa $148.1M na wamepewa zabuni hiyo bila ushindani (single source), wakati ujenzi wa BRT 2 (Gerezani -Mbagala) 20.3km wamejenga chini ya kiwango. Hawa wachina wameturoga? Zingatia, huo ni mkopo kutoka benki ya Dunia (WB). Na serikali ya Tanzania imekopeshwa $246.7 million kwa ajili ya ujenzi wa BRT-3 ($148.1 million) na BRT-4 ($99.9 million). Wanazo. Wakati huo DART wametumia $2.46 million to 77 kulipa wakazi kupisha ujenzi wa 23.6km kwa BRT-3
May 21, 2022 16 tweets 3 min read
ROSA MISTIKA!

Riwaya iliandikwa na Euphrase Kezilahabi na kuchapishwa January 1, 1971, ni kitabu SERIKALI ya Nyerere ilikipiga marufuku sababu zikitajwa maudhui yake yalikuwa ni yenye kudhalilisha (haikuthibitishwa) ukatoliki. Dhehebu ambalo Mwalimu Nyerere alikuwa muumini huko Watu wanajiuliza, endapo katika riwaya hiyo lingetumika jina la "MwanaAsha" kubeba taswira ya binti Rosa, wakatoliki akiwepo Mwalimu Nyerere wangelikasirika na kuzuia uchapishwaji wa riwaya hiyo ya Euphrase Kezilahabi? Maswali tu, tunajiuliza!
May 21, 2022 14 tweets 3 min read
Katiba yetu hakuna cheo cha “baba wa taifa”. Hakuna kanuni/sheria yeyote imetungwa wananchi kutambua cheo hicho. Sifikirii kama mtakuwa sahihi mkitaka Mwl. Julius Nyerere atambuliwe na wote kwa jina la ‘baba wa Taifa’. Ni Rais wa 1 wa TZ. Historia ya taifa letu ipo kabla yake! Ni kizazi dhalimu tu ndiyo kinaweza kupewa kila kitu na kukubali bila kuhoji. Neno “kwanini” linaonyesha ustawi wa ubongo. Hili siyo dola la kijeshi, kifalme au kisultani. Hatupokei kila neno na kumeza. Ndiyo, hakuna sheria inayotutaka tumtambue kwa cheo cha “baba wa taifa”. Ipo?
May 21, 2022 11 tweets 2 min read
Ukumbi wa Msekwa imefanyika semina, wabunge wamelipwa Shs. 440,000 (Shs. 172.9M). Kuipitisha bajeti ya miundombinu (ujenzi wa lot Na. 6 ya Tabora - Kigoma (411km). Na gharama za ujenzi ni (Sh.11.1bn) kwa kila 1km. 411km mkandarasi atatumia Shs. 4.6T. Kapewa tender bila ushindani. Mnakumbuka niliwapa simulizi, wizara ya fedha wameingia makubaliano na China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (tenda bila ushindani) thamani ya Shs. 6.7 trilioni kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani?