𝗣 𝗔 𝗕 𝗟 𝗢 🦁 Profile picture
Content Creator | Top Story Curator | Social Media Influencer | Open to Collaborations | 📩 kingpablotz@gmail.com
May 12 18 tweets 8 min read
Hebu fikiria.

Unasafiri peke yako katikati ya Jangwa la Sahara, Morocco.

Gari lako linagonga jiwe kubwa, linaharibika vibaya.
Uko umbali wa zaidi ya kilomita 30 mpaka 50 kutoka mji wa karibu.

Hiii ilikuwa ni mwaka 1993 — hakuna simu ya mkononi, hakuna GPS, hakuna msaada unaokuja.

Hivi ndivyo Emile Leray alivyopambana na kifo.

Thread 🧵Image Safari ya Emile ilianza katika mji wa Tan Tan kusini mwa Morocco.

Akiwa na gari lake aina ya Citroën 2CV, alitaka kupenya ndani kabisa ya Jangwa la Sahara — sehemu ambayo wachache waliwahi kuthubutu kuifikia.

Lakini mambo yalibadilika alipokutana na kizuizi cha kijeshi.

Wanajeshi walimwambia kwamba kwa sababu ya mgogoro uliokuwa unaendelea kati ya Morocco na Western Sahara, hapakuwa ruhusa ya kuendelea zaidi.

Emile pia alielezwa kwamba kama alitaka kuendelea na safari, lazima amchukue abiria mmoja wa kijeshi pamoja naye.Image
Mar 24 13 tweets 11 min read
“Mke wangu mpendwa Pauline,” kalamu ya Patrice Lumumba ilianza kuandika kwa haraka kwenye karatasi iliyokuwa imelowa kwenye gereza la Thysville.

Wakati huo mikono yake ikitetemeka kwa baridi na uchungu wa kupigwa na askari wa Mobutu.

“Usiwe na wasiwasi kuhusu maisha yangu, kwa maana najua niko kwenye njia ya haki"

"Wanaweza kunichukua kutoka kwako na kutoka kwa Roland wangu, lakini hawawezi kuua roho ya Kongo inayopigana ndani yangu.”

“Ni heri nife nikiwa huru, kuliko kuishi kama mtumwa.”

Alisimamisha kalamu, akitazama nje kupitia dirisha dogo lililokuwa na baa za chuma, ambapo mvua ya Novemba ilikuwa ikinyesha kama machozi ya ardhi yake iliyovunjika moyo.

Historia ya kafara, Kijana aliyeamua kupenda taifa lake hadi tone la mwisho.

Patrice Lumumba, shujaa wa Uhuru wa Kongo, mwanasiasa mkali, na mfuasi wa haki, alipoteza uhai wake kwa njia ya kikatili mno mwaka 1961.

Thread 🧵Image Katika kijiji kidogo cha Onalua, kilichopo katika mkoa wa Kasai wa Kongo ya Kibelgiji, tarehe 2 Julai 1925, mtoto wa kiume alizaliwa ambaye alikuja kubadilisha historia ya Afrika

Historia ambayo vizazi na vizazi vya Kongo na afrika kamwe haitosahaulika

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Élias Okit’Asombo, lakini dunia ilimtambua kama Patrice Émery Lumumba.

Alizaliwa katika familia ya Kikristo ya kabila la Watetela, wazazi wake wakiwa François Tolenga Otetshima na Julienne Wamato Lomendja, wafugaji wa kawaida waliokuwa wakijipambana na maisha chini ya ukoloni wa Wabelgiji.

Ardhi yao ilikuwa yenye rutuba, lakini utajiri wake ulikuwa unanyakuliwa na wakoloni, na watu wake waliishi kama watumwa katika nchi yao wenyewe.

Patrice alikulia katika mazingira magumu sana kama raia wengi nchini Kongo, lakini akili yake ilikuwa kama taa inayowaka katikati ya giza.

Alisoma katika shule za wamishonari Wakatoliki na Waprotestanti, ambapo alionyesha uwezo mkubwa wa kujifunza na kuwaza zaidi ya wengine. Alikuwa mtu makini na mdadisi wa kila jambo na mwenye kujiamini wakati wote

Alikuwa mtoto ambaye hakukubali tu mambo kama yalivyo—alichunguza, alihoji, na alianza kuhisi uchungu wa watu wake.

Alipokuwa kijana, alianza kufanya kazi kama karani wa posta huko Stanleyville (sasa Kisangani), na baadaye kama muuzaji wa bia huko Léopoldville (sasa Kinshasa).

Lakini moyo wake haukuwa kwenye kazi za kawaida alizokuwa akifanya, badala yake ulikuwa umejaa ndoto za uhuru wa raia na taifa lake.Image
Mar 16 10 tweets 9 min read
Hakika, maisha yana fumbo kubwa, hivi karibuni tumeshuhudia habari kadhaa kuhusu watu mbalimbali wakikamatwa kwa makosa ya madawa ya kulevya

Mambo ndio yamemkuta mwanadada huyu katika safari yake, Safari ya Ndoto Iliyogeuka Jinamizi la Kifo

Leo ni siku ya mwisho kwa Margaret Nduta.

Mwanamke kijana kutoka Murang’a, Kenya, ambaye alikuwa na ndoto kubwa za kubadili maisha yake. Alitaka maisha mazuri, alitaka kutoka kwenye shida za kifedha, alitaka kusaidia familia yake.

Lakini badala yake, alijikuta akihukumiwa kifo nchini Vietnam.

Leo, Machi 16, 2025, atanyongwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya—kosa ambalo anasema hakujua kama alikuwa amelifanya.

Lakini hii si hadithi tu ya mtu mmoja. Hii ni hadithi ya maelfu ya vijana wa Kiafrika wanaotafuta maisha bora nje ya nchi na kuishia kwenye mikono ya mitandao ya usafirishaji wa mihadarati.

Hii ni safari ya Nduta. Safari ya matumaini, ndoto, na mwisho wa kusikitisha.

Thread 🧵 👇🏾Image Nduta alikuwa kama vijana wengi wa Kenya na Afrika Mashariki. Margaret Nduta Macharia alizaliwa huko Karikwe, kijiji kidogo cha Kiharu katika Kaunti ya Murang’a.

Alikulia katika familia ya watu wa kawaida – mama yake, Purity Wangari, alikuwa mama wa nyumbani na mfanyabiashara mdogo wa mboga sokoni, na baba yake alikuwa mkulima wa kahawa na mahindi.

Margaret alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto wanne, na tangu mdogo alionyesha tabia ya utulivu na bidii
Alikuwa akifanya kazi za kuuza nguo za mitumba na kumsaidia mama yake sokoni, lakini pesa hazikuwa za kutosha.

Alikuwa na ndoto za maisha bora – akiangalia watu wakiendesha magari ya kifahari mjini na kusema, “Siku moja nitakuwa kama hao.” Lakini maisha ya kijijini yalikuwa ya changamoto, na ndoto zake zikaanza kufifia polepole

Alitaka maisha mazuri. Alitaka kusaidia familia yake, Alijua njia moja kuu ya kuyapata hayo: kazi nje ya nchi.

Uarabuni na Ulaya hizi ndizo zilikuwa ndoto zake.

Miji yenye mishahara mizuri, nafasi za kazi nyingi, na matarajio ya kubadili maisha haraka.

Na kama ilivyo kwa wengi, alianza kutafuta mawakala wa ajira.

Aliwaona watu wakiondoka kwenda kufanya kazi Uarabuni na kurudi na pesa.

Hakutaka kubaki nyuma.

Kwa hiyo, alijiingiza kwenye mtandao wa mawakala wanaosafirisha watu kwenda kufanya kazi nje.

Nduta hakuwa na pesa za kutosha kulipia ada ya mawakala hawa, lakini alipoambiwa kuwa kuna nafasi ya kazi na angeweza kulipa baadaye, aliona huo ndio mwanya wake wa kutoka kwenye umasikini.Image
Feb 15 13 tweets 7 min read
Haisemwi sana,

Pengine leo ndio unasikia, sababu wale jamaa huwa wanataka vyao ndio vizungumzwe.

Unapozungumzia majanga ya meli, Titanic huwa jina la kwanza linalokuja akilini kwa watu wengi.

Lakini kuna ajali moja ya baharini ambayo ni MBAYA zaidi kuliko Titanic, lakini haijulikani sana nje ya Afrika.

Hii ni simulizi ya MV Le Joola, meli ya abiria kutoka Senegal, ambayo ilizama mnamo 26 Septemba 2002, na kuua takriban 1,863 kati ya watu 2,000 waliokuwepo ndani yake.

Hii inamaanisha kuwa watu wachache sana walinusurika—ni watu 64 pekee!

Moja ya janga baya kutokea katika historia ya baharini..

The Africa's Titanic

Thread 🧵 👇🏾Image Le Joola ilikuwa meli ya abiria inayomilikiwa na serikali ya Senegal. Ilizinduliwa mwaka 1990 na ilikusudiwa kusafirisha watu kati ya mji wa Dakar, mji mkuu wa Senegal, na Casamance, eneo lililoko kusini mwa nchi.

Kwa sababu Casamance ilikuwa na mgogoro wa kisiasa na waasi wa kujitenga, usafiri wa barabara ulikuwa hatari.

Hivyo, serikali ilitumia Le Joola kusafirisha abiria na mizigo kwa usalama kupitia bahari.

Meli hii ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 583 pekee, lakini siku ya tukio, ilikuwa na zaidi ya watu 2,000, ikiwa ni zaidi ya mara tatu ya kiwango chake cha kawaida.Image
Jan 22 9 tweets 6 min read
Ameuliza swali la experience "Umewahi kupanda gari ya magazeti? Ilikuwaje safari yako?" na hizi ndio replies zenye vihoja kama ulikuwa hujui..

Check the thread 💔👇🏾 Image 😂💔 Image
Image
Image
Image
Jan 22 10 tweets 7 min read
Huyu jamaa ameuliza " nimechoka ku pretend nyie huwa mna unganisha vipi bao la kwanza na lipi?" na hizi replies za watu zitakushangaza 💔 🔞

Check the thread 🙆🏽‍♂️👇🏾😂 Image Kuna ukweli hapa? 😂 Image
Image
Image
Image
Oct 25, 2024 12 tweets 5 min read
Celebrities houses before and after fame,

Thread 🧵

1. Cristiano Ronaldo Image
Image
2. Lionel Messi Image
Image