M.D (πŸ…¨) Profile picture
M.D & Life Coach 🌳 ✊🏿GOD FIRST | TIME WILL TELL | TUISHI✊🏽 πŸ“ž 0716006808
May 29, 2023 β€’ 23 tweets β€’ 4 min read
Skia nikupe story yangu moja kuhusu jambo lile lile πŸ˜„.

Nilikutana na Binti mmoja hivi, nikawa na ukaribu nae akawa rafiki yangu sana ila siku akanieleza kuwa ananipenda. Mimi nilikuwa namtamani sana sema nilikuwa namuona kuwa sio Level yangu. So sikupenda kuathirishwa..πŸ‘‡ So nilikuwa nameza mate mchezo unaisha. Sasa yeye alivyokuja kuniambia ananipenda nikashtuka kwanza nikahisi anatania so nikaenda nae kwa utani utani. Bwana wee kumbe mwenzangu alikuwa serious tena kazama kweli kweli. Akawa ananipenda kiasi sasa tunakuwa na ugomvi kila wakati..πŸ‘‡
Mar 12, 2023 β€’ 16 tweets β€’ 3 min read
....INAENDELEA. 🧡

Jesca aliposhushwa pale nyumbani alishushwa kama Mzigo tu hakukuwa na mzungumzo mengi, Vilishuswa vitu vyake kisha yeye akashukuka na mtoto wake. Kwenye ile gari kulikuwa na Wanaume wawili, Yule mmoja ambae sio dereva akamfuata na kumwambia Jesca samahani..πŸ‘‡ Sana sisi tunatekeleza wajibu wetu ila pole sana kwa hili, Nakuhurumia sana sababu ni wengi wamefanyiwa kama wewe na nakushauri usije ukaendelea kuntafuta huyo bwana maana tunawajua waliokaidi wakamtafuta kilichowapata.
Jamaa akaingia kwenye mfuko wake akatoa Sh. milioni 1 ...πŸ‘‡
Mar 11, 2023 β€’ 23 tweets β€’ 4 min read
Ben alimuoa Binti Jesca alimpenda sana na waliishi kwa furaha sana siku za Mwanzo wa ndoa yao.
Ben alikuwa ni Mtumishi wa Umma wakati Jesca hakuwa amepata kazi. Alikuwa akiendelea kutafuta kazi kabla ya Ben kumuona na kumuoa basi siku zikaenda, Ben na Jesca wakajaaliwa...🧡 Mtoto mmoja wa kiume. Ben akamwambia Jesca kuwa inabidi waandae mazingira ya biashara ili angalau imsaidie kuleta backup kwenye mshahara wake pia akaeleza kuwa atatakiwa Jesca ndio awe msimizi wa biashara hiyo.
Wakati wakiendelea kujipanga Jesca alibadilika akaona kama..πŸ‘‡
Mar 1, 2023 β€’ 6 tweets β€’ 1 min read
Kuna dada mmoja hivi jina mwaka fulani alienda kuomba kazi ya kujitolea sehemu wakati amefika akaambiwa hakukuwa na nafasi, Akashukuru akaondoka wakati anatoka pale ofisini kuna mtu akajisemea kama utani tu kuwa labda kazi ya kufanya usafi. Aliesema vile hakujua kama yule dadaπŸ‘‡ Atatilia maanani kauli yake, Basi yule dada akarudi akasema naombeni tu hata hiyo ya kufanya usafi hamna shida.
Akaulizwa utaweza kweli? Akasema nitaweza, Basi Boss akapewa tarifa kuwa yupo dada wa usafi amekuja (Inaonekana walikuwa na uhitaji kweli) Boss akamuita..πŸ‘‡
Dec 17, 2022 β€’ 20 tweets β€’ 4 min read
Baada ya kupitia maoni ya watu wengi juu ya mtazamo wangu kuhusu Mwanaume kuoa Mwanamke asieajiriwa, nimegundua mambo kadha wa kadha na ili kuliweka sawa hili naomba soma UZI huu ili tuendelee kujifunza.

I can see wengi wamechangia kwa mihemko, experience na wengine ..πŸ‘‡ Ni wale fuata Mkumbo (Hawajui ila nao wanataka kuonekana wanajua). Anyway ni sehemu ya kujifunza pia.

Ok! Nitaanza na kwanini naamini familia itakuwa bora zaidi Kama Mama akiwa hajaajiriwa.

Lakini kabla ya yote nimeona maoni ya wengi yakibase kwenye maeneo tofauti..πŸ‘‡
Oct 22, 2022 β€’ 16 tweets β€’ 3 min read
Nikimuona mtu anapitia nyakati ngumu maishani huwa najiskia vibaya sana, Najaribu kuvaa viatu vyake nayabeba machungu aliyo nayo moyoni mwake, Lakini siishii hapo na kwa nia njema kabisa napendelea kumtafakari! Like Kwanini anapitia haya? Labda ni Mapenzi ya Mungu? Au Labda..πŸ‘‡ Kuna sehemu aliteleza? Au tatizo lake nini haswa? Unajua ni ngumu kumfuata mtu kumuuliza labda kwanini unapitia haya? Kibinadamu sio sawa kwani unaweza usimsaidie au anaweza jukufikiria vibaya hata kama nia yako ni njema. So najaribu tu kutumia akili yangu kujipatia πŸ‘‡
Oct 20, 2022 β€’ 6 tweets β€’ 1 min read
Nilimuuliza Baba yangu, kwanini niliitwa Regan? Akaniambia "Nilikuita hvyo sababu kuna bwana Mmarekani aliitwa Ronald Reagan, nilivutiwa na siasa na harakati zake, nikatamani mwanangu awe na spirit kama yake"
Nikamuuliza so na mimi niwe Mwanasiasa? Akanijibu "Sio lazima". 😌...πŸ‘‡ Nikamwambia Ronald Reagan alikuwa mtu maarufu hata kuwa Rais wa Taifa kubwa la Marekani, kuishi nje ya siasa ni ngumu kuishi kama alivyoishi yeye.
Mzee akaniambia "Fuatilia vizuri utagundua licha ya siasa zake alikuwa na mengi zaidi na makubwa aliyoyafanikisha kwa uwezo wake..πŸ‘‡
Oct 18, 2022 β€’ 15 tweets β€’ 3 min read
Ilikuwa hivi, Nilikuwa nilitafuta kazi sehemu na nikapata. Alieniajiri alikuwa mtu anaefahamiana na Baba yangu, hawakuwa marafiki ila walikuwa wanafahamiana kiasi. Baba yangu akaniambia nenda kafanye kazi, sahau kuwa mimi namfahamu Boss wako, fahamu mimi ni Baba yako tu ila...πŸ‘‡ Fahamu mimi sihusiki vyovyote na kazi yako, so hilo liweke akilini, ila pia akaniambia ikitokea kuna tatizo nisimueleze yeye kwanza bali nianze na Boss wangu na ikitokea ameshindwa kunisaidia ndipo nilifikishe kwake. Nikaenda kazini, nikafanya kazi mwenzi 1, 2, 3 nikaomba....πŸ‘‡
May 30, 2021 β€’ 17 tweets β€’ 3 min read
SAFARI YANGU YA KUTAFUTA MKE.
Mungu ajidhihirisha katika matokeo ya hitimisho la safari hiyo- UZI

TUENDELEE.....

Baada ya story yangu iliyopita kuelezea misukosuko niliyokutana nayo, na namna Mungu alivyonivusha sasa tuone namna Mungu alivyonitua mzigo mzito... Tukijikumbusha kidogo baada ya kuingia kwenye mahusiano na watu tofauti,
-Binti Wa Kilokole (Aliebadilika tabia)
-Binti Mfanyabiashara (Alietoa kiumbe chetu kisicho na hatia)
-Binti wa Kijijini (Niliegundua alikuwa mjamzito wakati nikitaka kumposa)

Sasa tuendelee,....