Keen observer of the interplay between Finance, International Economics, Taxation and Development. Passionate about learning, reading and running.
Nov 23, 2019 • 13 tweets • 2 min read
Weekend hii nimesoma kitabu kuhusu kesi iliyomkabili Nyerere ya mwaka 1958. Huenda historia ya Tanzania ingekuwa tofauti kama kesi hii ingeamuliwa vinginevyo.
Kuna vitu vingine vizuri nimejifunza kuhusu wakati huo vyenye mafunzo kwetu leo - THREAD
Julius Nyerere alishtakiwa kwa makosa matatu ya kukashfu ma-DC wakikoloni.
Kwenye gazeti la Sauti ya TANU la Tar. 7 Mei 1958, Nyerere alitumia maneno kama 'washenzi', 'maharamia' na 'magava wa mistuni' kuwaelezea ma-DC wakikoloni, DC Weeks wa Geita na DC Scott wa Songea.