🇹🇿l Africa-China Matters| Chinese Soft Power | @UniversityofDaresSalaam | Reggae | Hip Hop | Afrobeat | I tweet in Kiswahili and English|
Jan 9, 2020 • 10 tweets • 2 min read
UZI WA MJADALA WA KIMOMBO NA KISWAHILI: SOMO KUTOKA CHINA
1. Imekuwa ni mazoea kuona China ikitajwa kwenye mjadala wa lugha hapa kwetu Tz. Mara nyingi China hutajwa ktk muktadha wa kuonesha kwamba si lazima sana kujua kimombo. Mbona Wachina hawakijui na wameendelea? Wanahoji.
2. Nataka nianze kwa kusisitiza, tuna ulazima wa kukijua kimombo. Tena tukijue vizuri kabisa. Tukiwa UDSM kama wanafunzi, Mwalimu Lwaitama aliwahi kutuonya kwamba tusijifiche kwenye uzalendo wa Kiswahili ikawa ndiyo kisingizio chetu cha kutojua na kuzungumza vizuri kimombo.