Ayubu Madenge Profile picture
Dad|Friend|Citizen|Humble servant of the people
Aug 23, 2020 6 tweets 3 min read
Akiwa na miaka 27 alifanya mapinduzi akawa rais.Akainua uchumi wa nchi yake kupitia biashara ya mafuta,akaandika kitabu ambacho ilikuwa ni lazima wanafunzi wakisome “Green Book”.Miaka 42 ya kuitawala Libya Gaddafi akajiita Mfalme wa wafalme,kiongozi wa mapinduzi.Mwisho akauawa. Muammar al-Gaddafi Gaddafi alipiga marufuku biashara ya pombe na lugha ya kiingereza kutumika nchini kwake.Pia akafunga kumbi za starehe na bar.Vile vile alifanikiwa kuweka makubaliano na Makumpuni ya mafuta yaliyoiwezesha Libya kupata Pesa nyingi.Akajenga shule,hospitali na miundombinu yakutosha.