Urs Truly ✍🏾 Profile picture
I Dont Want It In Half Measures👌I Want It All🤲 #ARSENAL COYG || #SIMBA🦁 ||Never lied,True teller|| #fanani✍️
Mar 26, 2021 25 tweets 10 min read
"PIGA PICHA..☁️🙄"

Piga picha uko bar na machizi wako wawili mnakula stori za hapa na pale..ni kama saa tatu,tatu na nusu hivi..bar haijajaa vizuri ila ugiza flani na mziki wa kueleweka ndo unakufanya uendelee kuagiza moja moja... Piga picha kwamba Ghafla unaona kwa mbali kiwiliwili cha mtu kinakuja uelekeo wa bar..kila kinaposogea ndo unazidi kukiona vizuri..unaanza kuona nywele zilizofungwa kwa style yao inaitwa ponytail ya juu..unywele uliomwagika mpaka matakoni kwa jinsi unavyojitokeza pembeni ya mwili
Mar 19, 2021 20 tweets 3 min read
"ZINGATIA..☝️"
Retweet kwanza

Ni saa nne za usiku na mvua inanyesha tofauti na ilivyozoeleka ila naanza kuona mataa ya mji wa Dodoma..safari bado na njaa inauma..naona nikifika centre nisimame kidgo..stop ya kula ni Chako ni Chako kuna kuku wa kuchoma..nakula na kubeba nyingne.. Huwezi jua njian kuna mengi chakula muhimu..nakiwasha tena..napoanza kuitafuta Moro njiani malori mengi na ni usiku hvyo naenda kwa mwendo wa kawaida..nsije nkapunguza miaka ya kuishi..kamziki kwa mbali huku nasikia wiper zikifanya kazi kwa bidii ili tu nione uelekeo.
Nov 20, 2020 18 tweets 4 min read
"SIRI YANGU🤫"

Napiga pafu moja kutoka kwenye glass...mkono unanipiga begani,tuji bia tunanimwagikia kidogo kwa tshirt,,naangalia nyuma kuangalia ni nani huyu fa**..
Nakutana na cheko moja la kihuni..kumbe Jose,
"Mjinga umemwaga bia yangu" Ananicheki kwa dharau..anaita muhudumu ananiongezea mbili...
Inabidi nimuulize "hii jeuri imeanza lini kapuku wewe..😅

Anantizama af sura inabadilika.."kuna hela nilikua nadunduliza nimtoe mtoto wa mtu ila acha tuinywee tu bia..atleast siku niseme na mimi nshawahi kukutoa"
Oct 23, 2020 17 tweets 4 min read
"NILILAMBA JOKERI🃏.."

Nipo kwenye gari nna hasira flani..nafungua whatsapp natafuta convo yetu mwanzoni kabsa..naandika "mnazingua"
Huyu ni rafiki angu wa kike,Ney, tumepanga kwenda premier ya movie flani ilikua inatoka af tuna ka dk 10 ianze,ameomba aje na rafiki zake wawili Mi nipo na mchizi,ye ndo kamaindi mbaya. Kanimaindi mimi pamoja na huyo rafiki angu.."kubabeki,tunaenda kuanza movie nusu..si bora tukanywe bia tujue moja" 🤔nkawaza sio wazo baya ujue..
Mara nasikia milango inafunguliwa siangalii hata nyuma nawasha gari..
Aug 15, 2020 26 tweets 10 min read
"THUBUTUU...🤧"

Sijui ilikuwaje hadi nkasahau kuandika kuhusu hiki kisa..🤭
Nadhani kwasababu mchizi hakua mtu wangu wa karibu sana..ilikua ni kuonana kwenye vigenge vya stori na kitaa.

Ila siku tulijikuta wawili tu kwenye kota za tanesco anapokaa,chobingo moja yetu pendwa.. Mchizi aliitwa Saleh..
Tulisalimiana kiwana tukiulizana mishe zinaendaje na vijistori vya hapa na pale vya kupoteza muda.
Mchizi alitoa sigara mbili huku akiniuliza kama natumia..nilimjibu situmii hvyo aliiwasha yake akavuta pafu mbili kubwa..alitoa moshi nje af akabaki kaduwaa
Jun 27, 2020 18 tweets 6 min read
"KARMA..🎭"

🌡Kama huna kifua basi usisome uzi huu haukufai maana mi natoa visa vya ukweli kama ifuatavyo...👇

Nipo na mwana ananionesha picha af ananiuliza "unaikumbuka hii"..naichek af nacheka ni picha ya kitambo kidgo,tukiwepo sisi na wasichana watatu..mmoja wao akiwa VERO Vero mi nilimjua kipindi anatoka na mchizi wangu huyo..baada ya kukutana nae viwanja..tulikula sana bata za hapa na pale na huyu manzi,kipindi hicho anakaa mitaa ya sabasaba na wenzake.. walikua wamoto..kila weekend lazima niulizwe "shem leo wap!!nna rafki yangu nataka nikususie"
May 7, 2020 22 tweets 5 min read
"LAANA...."🧞‍♂️

Wiki moja baada ya kuanza darasa la kwanza kutokana na umbo langu kua dogo kidgo kuliko wengne ilinipa ugumu maana nilishindiliwa uonevu wa kila namna..ila siku,mmoja wa wanafunzi alinikingia kifua..na si mwingine bali ni "MUDI" kama wengi tufupishavyo, jembe langu Sikuwah kuonewa kuanzia siku hiyo na ndipo nilipojifunza ubabe..sikuwah kumwambiaga ila alikua kama kaka angu japo tulikua umri sawa ila kwa mwili wake na udogo wangu tofauti ilikua kubwa,alikua ndo rafiki wangu wa kwanza kishule shule. Alinifunza kujihami,kujilinda na ni yeye