Habiba Mtanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Profile picture
Tanzanian Adventurer | Story Teller & Digital Campaigner | True Story: My Journey to the Roof of Africa #Kilimanjaro | Tutor | Mummy
MKAZI FEKI πŸ‘£ Profile picture 1 subscribed
Apr 17, 2021 β€’ 10 tweets β€’ 4 min read
Naendelea tulipoishia..

HOROMBO

Katika vituo vyote, sehemu niliyoipenda zaidi kukaa ni Horombo. Ilituchukua masaa karibu 9/10 kufika.

Ni sehemu iliyochangamka, kama kijiji fulani hivi.

Katika safari yetu kuna vituo vya kupumzika na sehemu huko barabarani kwa ajili ya Lunch.. Kuna upepo na baridi sana, yaani kuliko kukaa nje mtu unaenda chooni upepo usikupige. Vyoo ni safi na vimejengwa vizuri.

Nakumbuka nikiwa nakaribia kibao cha Horombo I was excited kwamba nimefika after a long walk, nikaanza kutembea haraka huku nashangilia na kupiga mayowe πŸ˜…
Apr 14, 2021 β€’ 13 tweets β€’ 3 min read
MANDARA

Hii ndio ilikuwa point yangu ya kwanza baada ya kutoka getini. Nilikuwa na personal porter anaitwa Fredy. Mwenyewe alinipokea bag (back pack) na kujitambulisha kwangu.

Ukiwa na personal guide ina maana yeye atakua na wewe bega kwa bega, achana na wale guide wa group.. Tulianza kwa story akanielezea safari zake milimani. Yeye keshapanda mara 6 hadi Uhuru Peak. I was excited!

Mwanzo story zilikolea baadae zikakata ule uchovu.

Tunavyopanda tulikuwa tunakutana na makundi ya watu wanarudi na wengi walikua wanatuambia β€œpole pole”..
Apr 13, 2021 β€’ 7 tweets β€’ 2 min read
SAFARI YA MOSHI

Tunaingia Moshi usiku saa 2 na kupokelewa na wenyeji wetu wakarimu kishenzi. Wale ma-guide sijui walidhani tumetoka nchi gani hatujui Kiswahili, kumbe ni wabongo tuπŸ˜…πŸ˜…

Nadhani walishazoea wanaoenda kupanda Mlima ni foreigners tu. Hii kidogo ilinisikitisha.. Hoteli tuliyofikia kulikuwa na wazungu kibao. Wengi wametoka mlimani wakipongezana kwa dinner, wines na kupeana vyeti..

Nikawa nawatizama kwamba can I do this? Unaona watu wanachechemea miguu, sura hazitamaniki wamebabuka, wengi wako hoi.

Nikaguna, mambo yenyewe ndio hivi!!!
Apr 12, 2021 β€’ 9 tweets β€’ 5 min read
Leo tunaendelea na experience yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro ambapo machozi, jasho na damu ni sehemu ya safari hii inayohitaji ujasiri na moyo wa chuma kweli kweli..

Mfululizo wa matukio niliyopitia unaweza kukufundisha na kukuandaa vyema ewe Mtalii mtarajiwa πŸ˜…πŸ˜…

UZI πŸ‘‡πŸΎ Kituo 1: MLIMA URUGURU

Urefu wa Mlima Uluguru ni kama 8600ft. Na huu ulikuwa ni moja ya mlima wa majaribio kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Kiukweli hili lilikuwa ndio jaribio rahisi kuliko yote hadi tukaona kumbe mambo ni mepesi hivi! Tungejua πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Apr 10, 2021 β€’ 8 tweets β€’ 2 min read
Miaka kadhaa iliyopita nilipata mzuka wa kwenda kutimiza moja ya ndoto zangu kubwa - kupanda Mlima Kilimanjaro.

Siku zote nilitamani kufika juu kabisa ya "Paa la Afrika". Nikasema ipo siku tu!

Hatimaye siku zikawadia za kuitimiza ndoto yangu hii kongwe.

Ilikuwaje?

THREADπŸ‘‡πŸΎ Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails. Sikusafiri peke yangu, kundi letu tulikua 21. Njia tuliyotumia ni Marangu.

Gharama ilikuwa ni USD 560 kwa kila mmoja na hii ilihusisha kila kitu kuanzia usafiri Dar-Moshi, chakula, hoteli, vifaa, ada za getini, personal guides n.k.