hamza Lule Profile picture
Advocate of The High Court and Subordinate Court thereto*
Sep 23, 2021 7 tweets 2 min read
INTERNATIONAL TRANSFER CERTIFICATE (ITC)
Mara ngap umesikia story kuhusu ITC ? Unajua kwa nn khalid Aucho, Mayele, Djuma Shabani hawagusi gozi la ngombe?
Yes mchawi haswaa ni ITC yaan kwa kilugha cha shule za kidumu na fagio cheti cha kimataifa cha uhamisho. ITC ni cheti ambazo kinatumika kuidhinisha uhamisho wa kimataifa wa mchezaji kutoka shirikisho moja kwenda lingine kwa lugha rahisi ni kuwa mchezaji huyu anahama kutoka nchi moja kwenda nyingine. Mfano usajili wa Prince Dube kutua matajiri wa Chamazi ulikamilika baaada ya ITC .
Apr 16, 2020 13 tweets 7 min read
KESI MAARUFU
SISTI MARISHAY (N/F OF EMMANUEL DIDAS V THE BOARD OF TRUSTEE (MOI),
PARMANENT SECRETARY MINISTRY OF HEALTHY AND SOCIAL WELFARE AND ATTORNEY GENERAL

Hii ni kesi ya madai ambayo msingi wake ni uzembe wa kitaalamu uliyopelekea kupotea kwa uwezo wa kiakili na kimwili wa Ndugu Emmanuel Didas.Majira ya 26/10/2007 Didas(mhanga) alipata ajali mbaya ya pikikiki maeneo ya Morocco jijini Dar es Salaam.Mhanga alikua ni fundi an dereva pikipiki,baada ya ajali mhanga alikimbizwa hospitalini na kupokelewa MOI ambapo alilazwa.Madaktari wakaingia kazini
Jan 7, 2020 7 tweets 3 min read
KESI MAARUFU
"PINGAMIZI LA AWALI"
POINT OF PRELIMINARY OBJECTION
MUKISA BISCUITS MANUFACTURING CO V WEST END DISTRIBUTORS LTD(1969)EA 696

Kama umekua mfuatiliaji wa masuala ya kesi Mahakamani pasi na shaka utakua umekutana na msamiati au neno maarufu la "PINGAMIZI LA AWALI" PINGAMIZI LA AWALI ni hoja za kisheria ambazo zinawasilishwa na upande mmoja wa kesi mahakamani ambazo zikisikilizwa au kuendeshwa zinamaliza kesi husika. PINGAMIZI LA AWALI AU POINT OF PRELIMINARY OBJECTION al maarufu PO huwasilishwa mahakaman na upande wowote katika kesi