Kingo Magazine Profile picture
Jarida la katuni na hadithi zinazoelimisha na kuburudisha.
6 Apr
#porojo DARASA LA MAMA SAMIA

Tangu kuapishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, hotuba zake zimekuwa zikiwakuna wengi—zinakuna panapowasha!

1/
Kwanza alianza kwa kuwaagiza Takukuru na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufuta kesi zisizo na msingi na uhalali wa kupelekwa mahakamani. Halafu majuzi akawaagiza Waziri wa Fedha kukomesha ukamuaji, ubabe na maguvu unaotumika kuwakamua walipa kodi maana watahama nchi

2/
Hotuba za Mama Samia zina maneno rahisi rahisi lakini ukijaribu kuzitafakari vyema zinaweza kukukosesha usingizi. Kwa mfano, unaweza kujiuliza, je, mahakama zetu zimekuwa zikishikilia watu bila misingi ya ushahidi?

3/
Read 7 tweets