Dr Roman Profile picture
Father, Registered Medical Doctor 👨‍⚕️ | BusnessTycoon #Crypto | #Defi, Public Health Advocate | Human Right Activist l
Apr 25, 2020 6 tweets 1 min read
FAHAMU KUHUSU PUMZI MVUKE /kujikufikiza (steam inhalation)
Kujifukiza ni kuchukua hewa au mvuke kuingia kwenye mapafu kupitia mdomo au pua. mvuke unaweza kuwa na dawa za kitamaduni au hospitali. Kuna aina mbili za pumzi mvuke 1.kufukiza pumzi kavu ; hii ni pumzi ya mafusho kutoka kwa dawa tetea (fumes from volitile drugs) (Mf: Esta, Chloroform, menthol/amonia
2.kufukiza pumzi nyevu; Hii ni pumzi yenye joto la unyevu husaidia kupunguza msongamano puani/sekretion kifuani.
Apr 19, 2020 6 tweets 2 min read
UFAFANUZI KUHUSU BARAKOA NA MATUMIZI YAKE* Na @DocFaustine

1. Barakoa za N95 zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Covid-19. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini. 2. Barakoa za upasuaji (surgical masks) hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawana direct contact na wagonjwa. Barakoa hizi pia zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6. hizi hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi
Oct 16, 2019 7 tweets 2 min read
Fahamu Kuhusu Vidonda Vya Tumbo(Peptic Ulcers)
1.Hivi ni vidonda vinavyotokea kwenye ukuta wa tumbo au sehem ya kwanza ya utumbo mdogo Vidonda hivi vya tumbo ni matokeo ya muingiliano wa muda mrefu wa tindikali ya tumboni na kuta za tumbo. Dalili vidonda vya tumbo ni
1. Maumivu ya tumbo kabla au baada ya Kula
2.Tumbo kujaaa gesi (bloating)
3.kutokusikia njaa/hamu ya kula kupotea
4.kichefuchefu/ kutapika
5.kuhis kushiba haraka
6. Mara nyingne vikizidi husababisha mtu KUTAPIKA DAMU& KUTOBOKA TUMBO (perforation)