LUSAJO Profile picture
Grow your Company/Business Sales with Me | Increase your Market Outreach with Me | I'm the Founder & MD at @ebdigitaltec | JESUS IS MY LORD
Feb 17 18 tweets 3 min read
Ulishawahi kusikia neno FRANCHISING katika ulimwengu wa kibishara?

Naamini wengi wameshawahi kusikia lakini hawajawahi kufuatilia kwa undani kuhusu FRANCHISE BUSINESS.

Uzi huu usiochosha umeonesha FRICHISE BUSINESS inavyoendeshwa na kuleta mafanikio, bila kusahau changamoto zakeImage Kufranchise ni nini?

Franchise ni mfumo wa biashara ambapo mwenye BRAND ya biashara (Franchisor) anampa mjasiriamali mwingine (Franchisee) haki ya kutumia jina la biashara, Brand, mifumo ya uendeshaji, na bidhaa au huduma kwa MASHARTI na MAKUBALIANO maalum.
Apr 3, 2024 23 tweets 4 min read
Siku Moja katika mwezi wa 9 mwaka jana, nilipigiwa simu na kampuni fulani maeneo ya Mikocheni.

Waliniomba nikafanye training ya team yao kwa Sababu MAUZO YAMEDUMAA na yanaelekea kufa kabisa.

Niligundua UGONJWA ambao unatesa kampuni nyingi hapa TZ.

Shuka na 🧵 tujifunze Nilipofika, kama ilivyo kawaida yangu, siwezi kuanza session mpaka nikae na viongozi waniambie tatizo, ndipo ning'amue tatizo. Na baada ya hapo ndio najua angle ya kuishighulikia kama ni Uongozi au ni Team au wote kwa pamoja.

Na hapa siku yangu ilikuwa ndefu. Stori Iko hivi;
Feb 10, 2024 20 tweets 4 min read
Nasaha za Mzee wangu siku Moja kabla ya Harusi. Soma mpaka mwisho itakusaidia

Mwanangu Lusajo, unapoenda kuishi na mwenza wako, sio kila kitu cha kumfanyia surprise mke wako.

Surprise ni catalyst ya Mapenzi lakini pia shetani anaweza kutumia njia ya surprise kuua ndoa yako.

👇🏾 Image Sikiliza mwanangu, Surprise sio utamaduni wetu, bali ni utamaduni wa kizungu.

Nilipoenda kusoma St. Catherine Brock University, Ontario Canada mwaka 1976, ndio niliyakuta mambo hayo. Na jamii ya kizungu ndio waliokuwa wakifanya mambo hayo sana.

Nilishangaa sana kuona hayo mambo Image
Jul 26, 2023 8 tweets 2 min read
UJASUSI KATKA BIASHARA

Ili biashara yako IFANIKIWE SOKONI Kuna haja kubwa sana ya kuwa JASUSI. Na hii ndio jambo kubwa ambalo litakusaidia kukaa kwenye soko.

Kwa dakika chache tushuke na uzi mfipi kuona ujasusi huu ukoje, unafanyikaje na una faida gani. 🧵👇🏾 Image UJASUSI WA KIBIASHARA ni moja ya mbinu inayotumika katika kufanya Tafiti za Masoko (Marketing Research).

Hii itakupa picha ya namna Bora ya kuanzisha bishara au kuingiza bidhaa.

Hakuna Kampuni kubwa isiyofanya hayo mambo kwa mshindani wake.

Hufanya hivyo kwa SIRI kubwa sana Image
Jul 8, 2023 4 tweets 3 min read
Leo asubuhi nilipoamka, na kuingia Twitter, nilikutana na tweet ya @iamKaga ambayo alielezea issue ya vyombo.

Na Mimi nikasema wacha niende nikashuhudie. Na nikivutiwa, nanunua kabisa.

Nilifika pale godown, na kweli nilivutiwa na vyombo vya pale. Kisha nikachukua vyombo vya 9kg Ambayo vina thamani ya Tsh 40,500/- baada ya kutoka hapo, nikavipeleka home na kupiga picha na kushare kwenye status.

Na sijawahi kuweka status ya kuuza vyombo. Niliamua kuuza kwa set.

Ghafla nikatafutwa na jamaa mmoja, mmiliki wa Pub moja maarufu pale Mbeya.





Jun 23, 2023 13 tweets 2 min read
Wiki hii, nimefanikiwa kufika katika ofisi za kampuni tatu kwa ajili ya kufanya consultation za kibiashara.

Kuna mambo ambayo nimebaini na ni changamoto ambazo nimezikuta almost kwenye kampuni zote tatu.

Wacha niwasogezee, kisha nawe ufaidike kwa kujua haya maana yatasaidia 1. Watu wengi hufungua kampuni kwa sababu wana fedha za kufungulia lkn wamekosa kufanya mambo ya msingi kwa ajili ukuaji wa kampuni husika.

Mambo hayo ni:-
◾Hawana DHUMUNI maaalum la kampuni.
◾Hawajafanya RESEARCH juu ya Kampuni.
◾Hawajafanya chaguzi sahihi za JINA
Jun 12, 2023 9 tweets 2 min read
Maswali yamekuwa mengi sana juu ya watu kuona biashara ya mitumba ngumu, hii ni kutokana na factor zifuatazo.

FACTOR AFFECTING BIASHARA ZA MITUMBA.

Nimecompile na nazileta hapa ili kupunguza foleni kidogo.

Tunaenda kishule Shule kidogo 😂😂

UZI 👇🏾 1. LACK OF KNOWLEDGE
Watu wengi wanaanza biashara za mitumba kwa mikumbo. Hawapati nafasi ya kujifunza kwanza.

Hili ni tatizo linalopelekea kushindwa biashara na kuichukia.

Unatakiwa upate elimu kwa mzoefu + research zako ili uweze kuijua vizuri na kufanikiwa.
Jun 12, 2023 10 tweets 3 min read
Stori ya Mitumba sehemu ya pili inaendelea hapa!

Baada ya kupata hiyo simu, tukanunua na balo la nguo. Tulianza tena na balo la blouse za shifon kwa sababu ya mzunguko.

Tulipoteza sana wateja. Waliitikia wachache sana. Ule mzigo tuliuzungusha kwa almost wiki nzima Image Ndipo alianza kusafiri na kupeleka huko Rufiji, Bagamoyo na Morogoro lkn haikwenda kiviile. Maana ukienda kule lazima utauza bei ya chini.

Nami siku ambazo nilikuwa off nilikuwa nachukua nguo na kwenda kuuza maofisini. Ila inahitaji kunikana sana sio kazi rahisi 😂 Image
Jun 12, 2023 26 tweets 8 min read
Biashara ya wife ni kuuza mitumba. Na mimi huwa nashiriki katika hatua mbalimbali za kumsupport

Mpaka ikanifanya niijue vizuri biashara hii. nimejua chimbo zote muhimu za kununua, nimejua chimbo nzuri za kuuzia

Na hii ni stori ya kuwatia moyo wanaotaka kuwekeza ktk biashara hii ImageImageImage Miezi kadhaa nilishawahi kuleta Uzi flani kuhusu mimi. Na wengi mliusoma na nilielezea ktk hustle zetu me na wife, tushawahi kufanya mishe za kuuza mitumba.

Tulianzaje, tuliendeleaje na ikawaje? Twende pamoja. Leo nitawapa hatua tulizopitia na mwisho mtaona hii biashara
May 31, 2023 12 tweets 2 min read
Kabla hujaanzisha kampuni/biashara lazima ufikirie kwa kina kuhusu soko la bidhaa yako. Mambo yafuatayo ni muhimu kufanya:-

1. MARKETING RESEARCH (UTAFITI WA SOKO) wa bidhaa yako. Kabla hujaanzisha
◾Unatakiwa ujue kwa undani kuhusu bidhaa zako zina faida gani kwa wanunuaji. ◾Unatakiwa uwajue wanunuaji wako ni wa aina gani.
◾Unatakiwa ujue wateja wako wanapatikana wapi.
◾Unatakiwa uwajue washindani wako katika biashara/huduma
◾Unatakiwa ujue namna wanavyo faulu kuuza bidhaa hizo kwa wateja.
◾Unatakiwa ujue mbinu ambazo wanafikia wateja.
May 30, 2023 4 tweets 2 min read
Mbali na ushabiki wa mpira, Kuna binafsi ninamuadmire sana. Anaitwa Eng. Hersi Said.

He's so smart upstairs. Nimefuatilia interview zake kadhaa, Hana papara ya kujibu maswali. Anajibu kwa utulivu mkubwa sana.

Na hajibu kwa hisia/mihemko. Anajibu in realistic thoughts. Image Nikimsikiliza, nikimuangalia na kumuona evaluation zinazokuja kichwani mwangu ni:-

1. Msomi mzuri.
2. Kiongozi Bora
3. Msikivu
4. Hana majivuno
5. Mtanashati
6. Tajiri
7. Stands on logical things
8. Hakurupuki
9. Ana busara sana
10. Ni action maker.

Hayo mambo nayaona kwake Image
May 30, 2023 7 tweets 3 min read
Moja ya kitu tunachokifanya ni kuwameneji vijana na talanta zao. Tangu mwaka Jana mwezi wa 12 tunamanage vijana 5. Ambao career zao ni tofauti.

Leo wacha nimzungumzie mmoja wao. The best lady her self @immaculatepet14

I hope wengi wenu mnamuona sana humu Twitter. Image Huyu dada, tulikutana mtandaoni tukachat sana juu ya shughuli zake.

Akaniambia maeneo ambayo anakwama. Nikamwita aje tuonane.

Nilitaka nipime kiwango Cha utandaji wake, uaminifu na commitment. Nikampa kazi ya kuipaka ofisi yangu mpya.

Ila sikumwambia kwamba nampima and soever Image
May 30, 2023 8 tweets 2 min read
Vijana Kuna mambo Mnaweza kufanya kwa pamoja na mkajikuta mmetoka.

Mnajitafuta vijana wanne au watano wenye career tofauti ila kwa combination. Mfno;-

1. Graphics Designer
2. Photo & Videographer
3. Motions Designer
4. Social Media Manager

Mnajiorganise na kufungua ofisi yenu. Hii sio kampuni, Bali ni shared ofisi. Kwa maana kila mmoja anakuwa na meza yake aliyonunua yeye na kila mtu anakuwa na mashine yake.

Ila Kuna vitu mnashare. Mfano; Kodi ya pango, umeme, Internet, decoration ya ofisi.

Ofisi hii Mnaweza kumpa mtu mmoja dhamana ya kutumia TIN
May 29, 2023 21 tweets 4 min read
Jamaa yangu kanipigia simu analalamika KAIBIWA pesa na mkewe. Kakasirika kweli daaahhh!!

Baada ya muda kidogo mke wake kanipigia simu kuniambia Mme wake akipata mshahara anafanya matumizi yake personal afu hahufumii familia.

So akawa analalamika sana, kwamba niongee na mmewe Kwa sababu hajali familia. Makochi yamechoka, nguo za mtoto zimkwisha, Hajui mkewe anavaaje. Kiasi cha mwanamke kuishiwa nguo.

Na Jamaa anamkataza kabisa mke wake kujiriwa/kujishughulisha na Biashara za hapa na pale.

Sasa Kumbe mwanamke anapiga mishe za mtandaoni 😂😂
May 29, 2023 11 tweets 2 min read
Mambo haya ukiwa nayo katika lifestyle yako, ni rahisi kutengeneza circle kubwa za CONNECTION.

Na hii sio kuifanya kama event, inatakiwa iwe ni LIFESTYLE ambayo inaishi ndani yako.

Sasa twende sambamba katika Uzi huu mfupi.

Kisha ufanyie kazi, utanishukuru baadae. 1. UKARIMU.
Ukiwa na ukarimu katika maisha yako, unaongeza nafasi kubwa sana ya kuconnect na watu.

Mambo yanayo unda ukarimu ni:-

1. Heshima
2. Upendo
3. Kujali
4. Hekima

Ukizungumzia ukarimu, unazungumzia hayo mambo makuu.

Hivyo vitu hutengeneza HISIA
May 10, 2023 6 tweets 1 min read
Simu inaitaaa... Then napokea!!

Mimi: Hello bro, niaje Mzee wangu?
Jamaa: Fresh kaka! Mambo yanaendaje?
Mimi: Mungu anajaalia.
Jamaa: Poa poa, Sasa mwanangu niazime laki Kuna dogo kazidiwa yaani. Ntakupa next Ijumaa.
Mimi: Poa ndugu yangu nikutumie kwa no ipi?
Jamaa: hii hii Mimi: Poa mkuu. Jitahidi urudishe basi siku mkuu, nimechukua kwenye pesa ya ofc.
Jamaa: Bro usihofu, SIJAWAHI kukuangusha bro!
Mimi: Poa poa

Muala from CRDB App shwaaaaa...

Ikawa Asubuhi ikawa Usiku, siku ya Ijumaa hii hapa!

Saa 1 kimya
Saa 2 kimya
Saa 4 kimya
Saa 8 kimya
May 10, 2023 4 tweets 1 min read
Wiki ijayo, siku za Jumanne, Jumatano na Alhamis tutatoa huduma zifuatazo kwenye maofisi. Kwa ajili ya consultations. Kama kampuni yako Ina tatizo hapa:-

1. Mauzo (Sales)
2. Masoko (Marketing Plan, strategies & Branding)
3. Huduma kwa Wateja

Kindly DM for reservations. Image 1. SALES
Most of people katika hizi kampuni wanaweza kujua namna ya kufanya Selling lakini wanashindwa kwenye CLOSING OF DEAL.

Huo ndio ugonjwa ambao nataka tuukomeshe kwenye kampuni yako.

Wakati mwingine team zenu hamuwapi mafunzo.

Tuchek then tuwanoe vijana wenu 😂😂
May 9, 2023 8 tweets 2 min read
Una ndoto ya Kumiliki HARDWARE? anzaa hivi:-

Kwanza naomba nikukumbushe kwamba ukitaka ufanikiwe, Anza na ulichonacho mkononi. Usisubiri kiongezeke au kiaje au mpaka upewe! UTACHELEWA.

Twende sawa...

Fanya scouting ya eneo zuri lenye miradi ya ujenzi.

Tafuta frame yako hapo. 2. Lipia kwa uwezo utakaokuwa nao. Mieiz 3, 6 au 12 ni wewe tu.

Baada ya hapo, tungeneza shelf za kuanzia. Kisha punguza papara ndugu yangu, mambo mazuri yanakuja kwa upole.

3. Nenda Kariakoo kwenye mitaa ya Hardware za jumla. Kabla hujafanya manunuzi, tenga hata siku mbili
May 9, 2023 13 tweets 2 min read
Tunaendelea na Mganga wetu...

Sasa jamaa alifanya kama alivyoagizwa. Aliuza mzigo, Kisha akapata pesa ya kurudisha. Jamaa akaenda Dar na kurudisha pesa.

Yule mwenye mzigo akamlazimisha amkopeshe Tena mzigo mwingine. Jamaa akakubali.

Akakopeshwa mzigo mara 2 ya ukubwa wa kwanza. Jamaa akapata akili mpya ya kuuza. Na yeye alienda kuwakopesha wateja wake ili mzigo utembee sana.

Kweli alifanikiwa. Jamaa aliuza na akapata faida. Kweli akawa TAJIRI.

Alirudi kwa mganga na mueleza alivyo jiongeza. Mganga, akampongeza sana.

Unajua kilichotokea 😂😂
May 9, 2023 26 tweets 4 min read
Nikiwa Form 4 pale Iyunga Tech, kuna wikiendi nilienda kumtembelea Babu yangu mmoja aliyenilea lkn sio ndugu.

Ni maeneo ya Meta, Kuna mtaa unaitwa Chunya Street, jirani na bar maarufu ya zamani sana iliitwa Summer Night.

Huyu Mzee aliitwa Mzee Mahenge (Akili Nyingi) RIP 😔 Alifurahi sana kuniona. Na nilimpenda sana tangu nikiwa mdogo kwa sababu alitupenda sana watoto wa mtaani pale.

Alikuwa anatukusanya na kutusimulia hadithi. Ilifika mahali Kila wikiendi tulienda kwake tusimuliwe hadithi tu.

Yule Mzee alikuwa na HEKIMA sana, kiasi cha vikao
Mar 27, 2023 25 tweets 12 min read
NILIANZISHA OFISI YA KWANZA 2015 kupitia hustle za mtaani, mwaka 2016 Ofisi ILIVAMIWA NA MAJAMBAZI usiku na kuiba PC 7, mashine zngine na fedha taslim na ku7bisha kuwa na deni la almost 8Mil za wateja. Sikukata tamaa, niliendelea kukomaa na gigs ili kulipa madeni 👇🏾👇🏾 ImageImage Nilibahatika kuwa na timu nzuri ya kufanya kazi, na kwa kipindi kifupi tuliweza kutengeneza faida nzuri.

Ofisi hii ilipatikana maeneo ya Sae, Jijini Mbeya.

Ndipo nilipoamua kuhamia Dar ili kujitafuta na kuanza life jipya. Nikafikia kwa rafiki yangu wa damu @marck_nguta Image