Zitto MwamiRuyagwa Kabwe Profile picture
Member and former Party Leader @ACTWazalendo, Tegadalay ተጋዳላይ #HifadhiJamii #Ajira #MaishaNafuu #TheFutureIsPurple #Tanzania #TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Jul 20 7 tweets 8 min read
A Nation at a Crossroads

Tanzania is a land of immense potential—lush farmlands, vast mineral wealth, and natural gas reserves that could power a brighter future. Yet, under the Chama Cha Mapinduzi (CCM), which has ruled for 60 years, millions are trapped in poverty, farmers are exploited, and our resources benefit the few

THREADImage
Image
Image
Image
Operation Maji Maji is about changing that. Over two weeks, I’ve met farmers, families, and youth, hearing their struggles and amplifying their voices as we prepare for the October 2025 elections. Image
Image
Image
Image
Jul 17 7 tweets 4 min read
Leo inazinduliwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Shabaha ya Dira ni kuwa na Pato la Taifa la USD 1 trillion ambapo pato la mtu mmoja liwe wastani wa USD 7,000 kwa mwaka kutoka USD 1,200 za sasa.

Hii maana yake ni kuwa Uchumi wetu (GDP) inapaswa kukua mara 13. Inawezekana, lakini katika Taifa lililo na mshikamano, lisilo na ubaguzi na lenye demokrasia. Msingi wa hayo ni HAKI.

Kazi kubwa inapaswa kufanywa kwa NIDHAMU ya hali ya juu sana kufikia shabaha hiyo. Taifa lenye jamii ya uchawa uchawa haiwezi kuwa na nidhamu ya kufikia malengo tajwa.

THREADImage Nidhamu ya kazi inahitajika kwa kila sekta

KILIMO: Kasi ya ukuaji wa Uchumi itapaswa kuongozwa na sekta ya Kilimo, kikue kwa kasi ya 8-10% kwa mwaka. Tunapaswa kuweka nguvu kubwa katika TIJA kwenye Kilimo, angalau tuongeze mavuno mara mbili (doubling) ya sasa katika kila Ekari ya mazao ya Kilimo. Nina mfano napenda kuutoa, wa zao la Pamba, ambapo ilhali mkulima wa Tanzania anapata kilo 250 - 300 kwa kila ekari ya Pamba, mkulima wa Benin anapata kilo 800 na mkulima wa Burkinafaso anapata kilo 1500. Hali ni mbaya zaidi kwenye Mahindi na Mpunga ambapo wakulima wetu wanapata gunia chache zaidi kutoka kila ekari 1!

Dira ya 2050 itafikiwa iwapo tutakuwa na nidhamu kwenye TIJA!
Oct 21, 2021 8 tweets 2 min read
1/8 Dar imeendelea kuwa Mkoa unaochangia sehemu kubwa ya Pato la Taifa (GDP) Tanzania (maana:thamani ya bidhaa na Huduma zote zinazozalishwa nchini ndani ya Mwaka). Kwa mujibu wa Taarifa ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa Mwaka 2020, Dar es Salaam ilichangia 17.1% ya GDP ya Tanzania 2/8 Mikoa 9 inayofuatia Dar es Salaam Kwa kuchangia Pato la Taifa ni;
1.Mwanza - 7.4%
2.Mbeya - 5.6%
3.Shinyanga ( ikijumuisha Mkoa wa Simiyu) - 5.1%
4.Morogoro - 4.8%
5.Arusha - 4.7%
6.Tanga - 4.7%
7.Kilimanjaro - 4.5%
8.Geita - 4.4%
9.Ruvuma - 3.8%