NANI MMILIKI WA ZOOM PRODUCTION?
Ikiwa imetimia miezi kadhaa tangu Harmonize kuondoka WCB
kumekuwa na maswali mengi juu ya umiliki wa zoom production hasa baada ya jina la kampuni kubadilishwa kutoka zoom production na kuwa zoom extra huku mtayarishaji wa video
Akibaki yule yule Director Kenny?
Nikukumbushe tu kuwa upo kwenye page ya #Sanukanachapo hivyo upo sehemu salama kabisa utakwenda kupata majibu ya maswali yako yote bila ukakasi.
Awali ya yote kabla ya kujua mmiliki halali ni vyema kujua zoom production iilikuwaje ikaanzishwa.
WAZO
Zoom production ni idea ya Harmonize ambayo ililetwa kwa mara ya kwanza na Jose wa mipango rafiki mkubwa wa Harmonize sababu ni kutokana na wimbi la wasanii kwenda kufanya video South Africa.
Harmonize alilichukua wazo hilo kama changamoto na kuamua kumshirikisha
Mtayarishaji maharufu wa video Tanzania director “khalfani” ama “khalimandro” amabae hakulichukulia hilo swala serious na kukubali kishingo upande.
Harmonize alikuwa anaenda kushoot video yake nchini Afrika kusini alimchukua Director Khalifani ili aende kupata uzoefu
Ili akirudi Tanzania kampuni yao iwe na video za quality sawasawa na South Africa. bahati mbaya wakiwa airport kurudi Tanzania Director Khalfani alipoteza camera wakati wa kufanya ukaguzi ambayo ni mali ya kampuni ya zoom.
Ikabidi Director Khalfani amweleze Harmonize ukweli
Kuwa camera imepoteza jambo ambalo lilimuuzi Harmonize na kuchukulia kama uzembe na kumuamulu Khalfani aifate camera alipoiacha.
Bahati mbaya au nzuri baada ya Khalfani kuitafuta camera bila mafanikio pale airport akaja kukuta camera anayo askari wa
Uhamiaji wa South Africa, ambaye aligoma kutoa hiyo camera na kutaka kupata uthibitisho kutoka kwa Khalfani kwa kueleze kwenye camera kuna nini kama kithibitisho kuwa ile camera ni yake .
Khalfani alifanikiwa kuelezea vizuri na kweli baada ya askari kukagua materials
Akakuta kuwa maelezo yanafanana na kilichomo. ila baada ya kumkabidhi camera askari alidai rushwa ya zaidi ya landi 2000 ili ampe camera lakini Khalfani alisisitiza kuwa hana pesa na ni camera ya boss ambae anamsubiri chumba wasafiri cha kusubiri ndege.
Katika mvutano wa takribani dakika 20 mwisho askari akatoa camera kwa Khalfani ila bahati mbaya zaidi ndege ilikuwa imewaacha hivyo ilizidisha hasira kwa Harmonize kutokana na uzembe huo wa Khalfani
Ila sababu camera ilipatikana kidogo ilipunguza hasira kwa Konde boy.
Baada ya kurudi Tanzania wakawa na project ya kwanza kama zoom production ambapo ilibidi Harmonize asafiri na Khalfani mpaka Zimbabwe wakaenda kufanya kichupa cha ‘Ndonda’ pamoja na Jay Prayzah msanii maarufu Zimbabwe.
Kichupa kikafanyika na kumalizika fresh na kurudii zao Bongo
Project ya pili ikawa video ya Harmonize ‘Sina’ ambayo kwenye video muhusika mkuu alikuwa Mr. Nice ambaye ilikuwa shida kumshawishi afanye kichupa hicho kutokana story ya video ilimzungumzia maisha yake kwa asilimia 90.
Kipindi chote hicho Khalfani alikuwa anafanya kazi kwa kujilazimisha na alikuwa ahamini kwenye kufungua kampuni ya pamoja ‘zoom production’. Badala yake waliendelea kufanya kwa makubaliano tu ndio maana video zote hizo zilikuwa na jina la Khalfani.
KUKUTANA NA KENNY
Harmonize alizidi kuumizwa na hali ya Khalfani kutoamini kwenye kufungua zoom pamoja na kusababisha baada ya kutoka zimbwambwe kuanza kusaka director mwengine atakaye amini kwenye ndoto zake.
Wakati huo Harmonize alikuwa amefanya video ya ‘Happy birthday’ kwa
Hanscana ikafika wakati wa kuchukua video yake, Harmonize akamcheki Hanscana ili akachukue video hiyo ila Kwa bahati mbaya Hanscana alikuwa na hudhuru hivyo akamjulisha Harmonize apitie ofisini tu atamkuta Director Kenny
Ambae alikuwa kama msaidizi wa Hanscana kwa wakati huo.
Basi Harmonize kufika ofisi hizo akamkuta director Kenny ambae...
ITAENDELEA PART2 ... USIKOSE
#sanukanachapo
Tafadhari like,retweet na follow ili familia iongezeke na kuwafikia watu wengi zaidi.
🙏🙏🙏🙏
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.