Nilimpokea mtoto yule, alikuwa wa kiume, mkubwa, 4.4kgs lakini alikuwa amefariki. Nikamfunga vizuri, na kubandika karatasi kwenye kanga ile, "mtoto wa __"
Mama yake alikuwa nusu kaputi, kizazi kimechanika, daktari akifanya juu chini kuokoa maisha yake. #UZI
#MaamuziYakoKeshoYako
Alikuwa ni mtoto wake wa tano. Alikuwa amepoteza damu nyingi mno. Huku dripu ya damu ikishuka, daktari alisema, "leo, siku haijaanza vema"
Huyu ndio mgonjwa wa kwanza wa upasuaji kwa siku hiyo, aliletwa kwa upasuaji wa dharura.
Alipomaliza kushonwa, niliketi pembeni ya daktari
akijaza ripoti ya upasuaji. Kadi yake ya kliniki ilionyesha alihudhuria kliniki mara moja tu.
Daktari akasema, "Nilijua tu, lazima kuna kosa lilifanyika."
Alipomaliza ripoti hiyo, tukaendelea na mama mwingine, huyu aliletwa akiwa hajiwezi.
Mwili mzima umevimba, hawexi kusimama
wala haoni macho yamevimba.
Upasuaji mwingine wa dharura.
Mbio mbio, zikaletwa damu za kutosha kwasababu alikuwa anatokwa damu sana.
Akapigwa nusu kaputi, tukaingia kazini tena. Alikuwa binti mdogo miaka 20-22 tu, presha ya mimba ilikuwa ikimsumbua.
Daktari akasema, "jamani,
tuombeni huyu mtoto atoke salama"
Hali yake haikuwa nzuri hata kidogo. Mtoto alikuwa amefariki naye, hii ilikuwa mimba ya kwanza.
Tukamsafisha na kutoa damu iliyokuwa imetoka sana ndani, akashonwa vizuri.
Kila mtu kwenye chumba cha upasuaji alishusha pumzi.
#MaamuziYakoKeshoYako
Ripoti ikaandikwa, naye alionekana kuwa na presha ya mimba, lakini hakutumia dawa.
Daktari alipomaliza, aliketi akaongea na sisi, "hakuna kitu muhimu kama kuhudhuria kliniki na kupata vipimo vyote muhimu."
Akatueleza, kina mama wengi wakishazaa mara 2/3
#MaamuziYakoKeshoYako
Wanajisahau, wanakuwa sio wahudhuriaji wa kliniki kwasababu wanaamini wanafahamu kila kitu kuhusu ujauzito.
Hicho ndicho kilitokea kwa yule mama wa kwanza. Mwisho kumbe amepata mimba ya mtoto mwenye uzito mkubwa, amekaa nyumbani na uchungu, ameshindwa kuzaa
#MaamuziYakoKeshoYako
kwasababu njia ni ndogo tofauti na ukubwa wa mtoto. Mwisho mtoto amefariki na kizazi kimechanika, imebidi kitolewe.
Lakini pia, kwenda kliniki pekee haitoshi. Unaenda je, unahakikisha unapata huduma zote na unafuata hayo maelekezo?
Hicho ndio kimetokea kwa
#MaamuziYakoKeshoYako
yule binti wa pili. Licha ya kuhudhuria kliniki kama ilivyotakiwa, hakuwa akitumia dawa za presha kama maelekezo ya daktari. Naye amepoteza kifungua mimba wake.
Lakini je, kina mama na wenza wao wanafahamu ni huduma gani wanatakiwa kupata wakiwa wajawazito?
#MaamuziYakoKeshoYako
1. Kupima uzito, presha, urefu, kiwango cha damu, ultrasound(kujua maendeleo ya mtoto), UKIMWI, Kaswende, Malaria na mkojo.
Hivi vipimo ni muhimu SANA kwa afya ya mama na mtoto.
2. Kuchoma sindano ya tetenasi
3. Kuonana na daktari, ambapo ataangalia
#MaamuziYakoKeshoYako
ukubwa wa mimba, mapigo ya moyo ya mtoto na afya ya mama kwa ujumla.
4. Kupewa elimu ya dalili hatari za ujauzito. Mf: kuvimba mwili mzima, kifafa, homa kali, mapigo ya moyo kwenda kasi, n.k
Dalili hizi zinatokana na magonjwa yanayohatarisha ujauzito
#MaaamuziYakoKeshoYako
5. Kunywa dawa za kuongeza damu, dawa za malaria, dawa za minyoo na iwapo ana presha, basi dawa za presha, au magonjwa yoyote ambayo anaweza kuwa nayo mama.
NI MUHIMU SANA, mama kuzingatia dozi aliyoelekezwa na kumaliza dozi bila kuacha.
#MaamuziYakoKeshoYako
Katika matumizi ya dawa, mama anatakiwa kuhakikisha hatumii dawa YOYOTE ambayo hajaelekezwa na daktari ANAYEFAHAMU KUWA YEYE NI MJAMZITO. Yani iwapo mama ameenda kumuona daktari, lazima aseme kuwa ni mjamzito kwasababu baadhi ya dawa ni hatari kwa mimba
#MaamuziYakoKeshoYako
6. Elimu kuhusu homa ya ini, kunyonyesha, lishe ya mama, maandalizi ya uzazi na bima ya afya.
Elimu hii ni muhimu sana kwa mama, mtoto na baba hasa katika maandalizi ya kujifungua na kulea mtoto. Lishe ya mama inaamua mtoto akue vipi tumboni.
#MaamuziYakoKeshoYako
7. Usiri, mama anatakiwa kutambua kuwa, anapopimwa na kuonana na daktari ana haki ya kuwa na usiri. Yani, vipimo hivyo viwe kati yake na mwenza na daktari na nesi lakini taarifa zake ia zisiwekwe wazi kwa watu wengine zaidi ya wanaohusika.
#MaamuziYakoKeshoYako
Mwisho kabisa, ambacho ni muhimu zaidi. Ni mama kutambua kuwa ana haki juu ya yule kiumbe aliyembeba. Kwamba ushauri wa daktari unakuja kwanza kabla ya mengine yote. Kueleweshwa maana ya vipimo alivyofanyiwa na majibu yake. Na sababu za vipimo hivyo.
#MaamuziYakoKeshoYako
Afya ya mama mjamzito ni jukumu la jamii kiujumla, na NAKUMBUSHIA: Ewe BABA, kwenda KLINIKI na MAMA MJAMZITO sio OMBI, ni JUKUMU LAKO kufahamu hali ya mtoto na mama na kuwa sehemu ya MALEZI ya huyo mtoto tangu akiwa tumboni.
#MaamuziYakoKeshoYako
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
