MASKINI & TAJIRI:-
1.Maskini hudhani utajiri ni bahati,tajiri hudhani umaskini hutokana na uvivu na uzembe. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake,tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.
2.Tajiri bila masikini ni maskini lakini maskini bila tajiri ni tajiri.Umaskini ni matokeo ya fursa zote ambazo hazikutumika kwa usahihi,utajiri ni jumla ya fursa zote zilizotumika kwa usahihi
3.Maskini huwaza kulima mchicha,tajiri huwaza kulima miti ya mbao.Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa,tajiri huamini atapata pesa kupitia pesa za wengine.Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa,tajiri hudhani maskini ana tabia ya kuombaomba.
4.Maskini hupata pesa kwa kufanya kazi hasizozipenda,tajiri hupata pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.Maskini hufundisha watoto wake kupambana na maisha,tajiri hufundisha watoto wake kuwa matajiri.
NB:BILA MASKINI UTAJIRI HAUNA MAANA.
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
