Oooh Mama Afrika! Tunakusifu kwa kuijaza Afrika. Kwa kutupa matunda bora ya mbegu zilizopandwa kwako.
Tumeona kilio chako kutoka nyikani. Kilio chako kwa matunda yako yaliyopotea kabla hayajaiva.
Mama Afrika, kilio chako tumekisikia. Futa machozi.
Kwani #MaamuziYakoKeshoYako #UZI
Ni siku nyingine tulivu, baada ya purukushani za daladala kuwahi hospitali, nilimsalimu nesi wa zamu huku nikivaa koti langu tayari kuandaa meza kwa ajili ya kliniki ya kina mama wajawazito.
Mlipuko wa homa ya virusi vya Korona ulikuwa umeanza, na siku ile #MaamuziYakoKeshoYako
Tulikuwa na mengi ya kuongea na kina mama wajawazito.
Nesi alitupa kila mmoja jukumu la kuelezea kitu kimoja.
Kabla ya kliniki, kabla ya kugawa namba kwa ajili ya kumuona daktari, ni lazima tutoe MASOMO mbalimbali kwa faida ya kina mama wajawazito.
#MaamuziYakoKeshoYako
Leo tulikuwa na masomo manne:
1. COVID19
2. Homa ya ini
3. Dalili za hatari kwa mama mjamzito
4. Umuhimu wa bima na maandalizi ya uzazi
Masomo yalifundishwa lkn somo la tatu lilitakiwa kuwa la majadiliano.
Nesi alichagua mama kila benchi ataje dalili hizo #MaamuziYakoKeshoYako
Kina mama wengi ambao waliweza kujibu walikuwa na mimba ya pili au zaidi, wale wa mimba ya kwanza wengi walikosea.
Nesi akawaita wale kina baba wote walioandamana na wake zao wajawazito, akawaambia, "kila mmoja ataje dalili moja ya hatari kwa mama mjamzito"
#MaamuziYakoKeshoYako
Kila mmoja alikuwa kimya.
Nesi akasema, "nyie kina baba ndio wasimamizi wa wake zenu wajawazito, nyie ndio mnalala na kuamka nao, haya hamjui dalili za hatari, unamsaidiaje huyo mkeo sasa? Unajuaje kwamba anacholalamika sasa hivi ni hatari au kawaida?"
#MaamuziYakoKeshoYako
Kimya kikatawala. "Kakaeni", akawaambia sura yake ikionyesha wazi kukwazwa na kilichotokea.
Huku akipanga kadi za kliniki aanze kuita majina alinong'ona, "watu wanadhani kuja kliniki ni ili tu wahudumiwe mapema basi"
Zoezi likaendelea, tukipima uzito, presha #MaamuziYakoKeshoYako
Na kuwaelekeza kuingia kwa daktari.
Nikiwa najaza taarifa zao, alikuja mama mmoja wa makamo, ilikuwa mimba yake ya tano lakini zote nne zilikuwa zimeharibika. Alikuwa amekuja na mumewe, mtoto hachezi tumboni. Akaruhusiwa kuingia kwa daktari akiwa na mumewe. #MaamuziYakoKeshoYako
Nilipoingia kwa daktari kukabidhi kadi zao, walikuwa wanampa majibu ya ultrasound. Kwa bahati mbaya mtoto alikuwa amefariki.
Mama yule aliinama, mume wake akamshikilia, akamkumbatia. Wote wakalia. Huyu ni mtoto wa TANO wamempoteza. Ilisikitisha.
#MaamuziYakoKeshoYako
Baada ya kushauriwa na daktari walitoka akaingia dada mmoja wa miaka 20 hivi, yeye alikuwa peke yake
Alianza, "Daktari, mimi hii ni mimba yangu ya kwanza, nina presha na nimekuwa natumia dawa lakini tangu majuzi mtoto hachezi, nikaambiwa ni kawaida inatokea"
#MaamuziYakoKeshoYako
Daktari akampandisha kitandani akapima tumbo kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto. Hakuyasikia.
Akamuuliza, "ni mtoto hachezi tu, au kuna hali yoyote ya tofauti umeisikia hapo kabla ya kuona mtoto hachezi?"
Akasema, "Wiki ilopita nilitokwa na damu kidogo, wifi
#MaamuziYakoKeshoYako
alisema inatokeaga kwenye ujauzito wa kwanza, kwahiyo sikutilia maanani. Lakini kutokea hapo mtoto alipunguza kucheza. Pia nimekuwa naumwa sana kichwa, wakati mwingine uso unavimba yani mwili mzima. Nakunywa dawa zangu za presha basi"
Akaelekezwa kupima
#MaamuziYakoKeshoYako
Ultrasound. Baada ya muda akarudi, ultrasound ikionyesha mtoto amefariki, amekuwa mummified. Daktari akamueleza kinachoonekana. Yule dada alilia sana, akagalagala pale chini, tukambeba tukamuingiza kwenye chumba cha ushauri akaongea na daktari kutulizwa
#MaamuziYakoKeshoYako
Hawa wawili ni mifano ya wanawake wengi wanaopoteza watoto kwasababu ya kutofahamu dalili za hatari, na wanaowazunguka kutofahamu pia.
Je, unafahamu ni dalili gani hizo?
-Homa kali, Degedege, kutokwa na damu ukeni, mwili kuvimba, maumivu makali ya kichwa
#MaamuziYakoKeshoYako
Lakini zaidi ya zile za wakati wa ujauzito, kuna dalili za hatari wakati wa kujifungua, ambazo zinaweza kusababisha kifo cha mama, mtoto au wote.
Dalili hizi ni kama zinavyoonekana hapo chini.
Ni muhimu kwa wanaomjali mama mjamzito kuzifahamu hizi.
#MaamuziYakoKeshoYako
Lakini haya yote yanawezekana tu iwapo wanaomjali mama mjamzito haswa kina baba watahudhuria kliniki pamoja na wenza wao, na kujifunza yanayofundishwa huko.
Pia kuwahi kuanza kliniki na kwenda pale unapoona mabadiliko yoyote katika mwili.
#MaamuziYakoKeshoYako
Muhimu zaidi ni kuhakikisha kama mama mjamzito ana magonjwa ya muda mrefu kama presha, kisukari, magonjwa ya moyo n.k anaendelea na dawa hizo kama anavyoelekezwa na daktari.
Na kuhakikisha anachoma chanjo na kunywa dawa zote anazotakiwa wakati wa ujauzito
#MaamuziYakoKeshoYako
Iwapo ataumwa ugonjwa wowote, ni lazima amfahamishe daktari kuwa yeye ni mjamzito ili kuepuka dawa zinazoweza kumdhuru mtoto tumboni.
Kuepuka matumizi ya mitishamba, na dawa zisizothibitishwa na wataalamu ambayo yanaweza kusababisha mimba kuharibika
#MaamuziYakoKeshoYako
Kina baba kuja kliniki na mwenzi wako ni JUKUMU lako, sio OMBI.
Ni JUKUMU lako kufahamu dalili za hatari.
Ni JUKUMU lako kutoa sapoti ya kihisia kwa mama mjamzito wakati wote hasa wakati anapopitia hali ngumu kama mimba kuharibika, kuumwa n.k
#MaamuziYakoKeshoYako
Ooh Mama Afrika. Nimefikisha ujumbe kwa matunda ya tumbo lako. Nimefikisha ujumbe kwa wapanda mbegu. Nimefikisha ujumbe kwa mataifa.
Nitakulinda Mama Afrika hadi uijaze dunia.
Nchi ipambwe na matunda ya tumbo lako.
Tuponye maumivu ya wale uliowapoteza.
#MaamuziYakoKeshoYako
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
