Tanzania: Uhuru hatarini kuelekea Uchaguzi hrw.org/sw/news/2020/0…
Hii hapa Kiswahili:
Mamlaka nchini #Tanzania zimeongeza ukandamizaji dhidi ya vyama vya upinzani, taasisi zisizokuwa za kiserikali na vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo
@hrw wapanue wigo!
"Tangu .. mwezi Juni, serikali imekamata takribani wanachama 17 wa vyama vya upinzani na wakosoaji wa serikali, kusimamisha kazi za kikundi cha watetezi wa haki za binadamu na kufuta leseni na kuzuia vikundi vingine vikubwa vya utetezi wa haki za binadamu kuwa waangalizi" @hrw
"Mamlaka pia zimeweka vikwazo vipya kwa vyombo vya habari, kufuta leseni ya gazeti lenye uhusiano na mwanachama wa upinzani na kuzuia vyombo vingine vya habari kutokana na kutoa taarifa juu ya Covid-19, ambayo Rais John Magufuli anasema haipo tena nchini" @hrw #Tanzania
“Badala ya kuzingatia haki ya kujieleza katika wakati huu muhimu, mamlaka zimeamua kuchukua hatua ambazo zinaleta mashaka juu ya uchaguzi kuwa wa huru na haki.” @oryembley @hrw
Washajua mpk kimataifa kinachoendelea #Tanzania
#TutaelewanaTu mbona?
"Mwezi Julai, polisi walimkamata na kumshikilia Sheikh Issa Ponda, @PondaIssa kiongozi wa Kiislam, kwa siku tisa baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari kutaka uchaguzi huru na wa haki"
#Tanzania
This is on the record! Mahodari wote majina tuyaweke kapuni!
"Serikali pia imeweka vizuizi vipya kwa vyombo vya habari na katika uhuru wa kujieleza mitandaoni. Imepitisha kanuni zinazopiga marufuku watangazaji wa Kitanzania kufanya kazi na watangazaji wa kigeni bila mtumishi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano #Tanzania "
@hrw #TutaelewanaTu
"Mnamo Juni 10, bunge limepunguza uwezo wa vikundi kupinga kisheria sheria au sera ambayo inadaiwa kukiuka muswada wa haki za katiba. Hatua hii inaonyesha kuwa imelenga kuzuia vikundi kufungua kesi yenye maslahi ya umma kwa niaba ya wahanga wa dhuluma za serikali" @hrw #Tanzania
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
