Post Tender Negotiations: Majadiliano baada ya kuwasilisha Zabuni.
Haya ni majadiliano yanayolenga kuboresha uelewa wa pande mbili za zabuni yaani MNUNUZI NA MUUZAJI (buyer/procuring entity and Seller/Supplier)
Majadiliano haya hufanyika baada ya wasilisho rasmi la zabuni na kabla ya kutolewa hati ya mahindi 'award notice'. Ni lazima yafanyike kwa uwazi na kwa kushirikisha wadau wote muhimu, taarifa zitunzwe kama ukaguzi utahitajika.
Majadiliano haya hulenga maeneo muhimu kama
-gharama ya zabuni, mradi
-taratibu za malipo
-garantii na waranti
-gharama za 'Maintenance na Msaada' mwingine
-nk
Wazabuni wote wanaofika hatua hii wanatakiwa wapate nafasi sawa na kwa uwazi mkubwa.
Hii no hatua muhimu na wazabuni wanatakiwa wajiandae na waje wakiwa na taarifa muhimu
Makampuni mengi ya Kitanzania wamekua na changamoto za kujiandaa na hatua hii na wamekuwa wakionekana kutomudu pale ambapo hatua hii inahusisha makampuni ya nje.
Wakati makampuni mengi ya nje huleta uwakilishi mkubwa kwa kampuni za Kitanzania ni kinyume.
Ni muhimu kwenye majadiliano haya 'supplier' kuja na timu yake hasa watu wa ufundi, fedha na hata mtendaji mkuu kutegemeana na thamani na ukubwa wa zabuni. Hapa hata wale watakaowauzia malighafi unaweza waalika ili uweze kutoa majibu kwa wakati. Hawa ni pamoja na OEMs.
Ukiacha uwezo kampuni na ubora wa zabuni, namna unavyoonesha na kujibu wakati wa majadiliano baada ya zabuni yatatoa uelekeo wa kupata au kukosa zabuni husika.
Ni mujibu kujiandaa kwa nafasi na kwa taarifa sahihi.
#procurement #negotiations #localcontent
Majadiliano haya hufanyika baada ya wasilisho rasmi la zabuni na kabla ya kutolewa hati ya mshindi 'award notice'. Ni lazima yafanyike kwa uwazi na kwa kushirikisha wadau wote muhimu, taarifa zitunzwe kama ukaguzi utahitajika.
*mahindi = Mshindi
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
