▶️WAFAHAMU WATU MASHUHURI WALIOUWAWA KWA KUPIGWA RISASI.
#uzi
#vitukuntu
01. ABRAHAM LINCOLN
👉Alikuwa raisi wa 16 wa marekani na ndiye raisi wa kwanza wa marekani kuuawa akiwa madarakani. Aliuwawa mwaka 1865 na John Wilkes Booth aliyeudhiwa na maamuzi ya Lincoln ya kutambua....
....haki za watu weusi. Lincoln alipigwa risasi na John Wilkes Booth alipohudhuria kwenye maonyesho ya muziki. Booth nae aliuawa siku mbili baadae baada ya jaribio la kutoroka kushindikana.
(📸👇 John Wilkes Booth)
02. BENAZIR BHUTTO
👉Alikuwa waziri mkuu wa 11 wa Pakistani na kiongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa cha PPP. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la kiarabu akichagizwa na siasa zake safi za kidemokrasia. Aliuwawa disemba 27 mwaka 2007 akiwa kwenye gari yake aina ya....
....land cruiser akitoka kwenye mkutano wa kampeni. Gari hilo lililokuwa wazi juu lilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi lakini Bi. Bhutto alisimama ili kuwaunga mkono wafuasi wake ndipo alipopigwa risasi na baadae mlipuko ulitokea na kusababisha vifo vya watu.....
📸👇
.....wengine 2o katika eneo la tukio.
03. JOHN F KENNEDY (JFK)
👉Alikuwa raisi wa 35 wa marekani aliuwa November 22 mwaka 1963 akiwa raisi wa nne kuuawa kwa kupigwa risasi katika historia ya marekani. Akiwa na mkewe, kwenye gari la wazi akitoka kwenye hotuba alipigwa risasi tatu. Mpaka leo hakuna jibu la.....
📸👇
.....moja kwa moja juu ya nani aliyehusika kumuua John Kennedy japokuwa "Lee Hervey Oswald" ndiye aliehusishwa na mauaji hayo. Lee nae aliuwawa na raia mmoja (Jack Ruby) siku mbili tuu baadae alipokuwa akipelekwa rumande.
(📸👇 Lee Harvey Oswald)
👉Cha ajabu ni kwamba, John kennedy, Lee Oswald, na raia aliyemuua Oswald, wote walipoteza uhai wao katika hospitali ya Parkland Memorial kwa nyakati tofauti. Mdogo wa John aliyeitwa Robert F Kennedy nae aliuawa mwaka 1968 (alikuwa anawania uraisi wa marekani)
(📸👇 Jack Ruby)
04. MARTIN LUTHER KING JR
👉Anafahamika kwa harakati zake za kutetea usawa miongoni mwa waamerika weusi. Martin Luther king Jr ambaye alitumia dini yake ya kikristo kukemea ukandamizwaji wa watu weusi, aliuawa miaka mitatu baada ya mwanaharakati mwingine......
📸👇
....Malcom X kuuwawa mwaka 1965, wote wawili waliuwawa wakiwa na miaka 39.
👉Robert F. Kennedy aliyekuwa Mdogo wa raisi wa marekani (John F. kennedy), na Mgombea wa uraisi wa Marekani kwa kipindi hiko, alitoa hotuba ya kukemea vikali mauaji ya Martin Luther King Jr, cha kushangaza nae aliuwawa miezi kadhaa baadae!!
(📸👇 Robert F. Kennedy)
05. TUPAC SHAKUR
👉Hili si jina geni kwa mtu yeyote mpenzi wa muziki hasa miondoko ya hiphop. Alipigwa risasi Septemba 7, 1996 akitoka Las vegas Nevada alikokwenda kuhudhuria pambano la Mike Tyson, akiwa na Meneja wake Suge Knight (ambae pia anahusishwa na kifo hicho).
📸👇
👉2pac aliuwawa kwa kupigwa risasi kadhaa kifuani zilizotoka kwenye gari moja nyeupe iliyowazuia kwa pembeni. 2pac alifariki siku chache baadae katika hospitali ya University Medical Center of Southern Nevada. Wengi walihusishwa na kifo chake huku idadi kubwa ikimuelekea....
.....Christopher Wales (B.I.G) kuwa ndiye aliyehusika moja kwa moja na kifo cha Shakur. B.I.G na yeye aliuwawa miezi sita baadae na watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa 2pac kwa lengo la kulipa kisasi.
📸👇
06. MAHATMA GANDHI
👉Pia anafahamiaka kwa jina la "Mohandas Karamchand Gandhi". Gandhi ni maarufu kwa hotuba na kauli zake zinazotumiwa mpaka leo. Huyu ni kiongozi maarufu zaidi wa India iliyokuwa ikitawaliwa na Waingereza. Mahatma gandhi alikuwa kiongozi wa kiroho....
📸👇
....na kisiasa, aliuwawa tarehe 30 Januari mwaka 1948 na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu(Nathuram Godse) alipokuwa akielekea kufanya ibada.
(📸👇 Nathuram Godse)
07. JOHN LENNON
👉Nani halijui Kundi la vijana watanashati la The bittles? (kibongo-bongo “bitozi”) lilotamba miaka ya 1970 na 1980. John Lenon alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo lililotamba sana na alifariki tarehe 8 disemba mwaka 1980.
📸👇
👉Akiwa anaingia hotelini, Lenon alisikia sauti ikimuita na alipogeuka, alipigwa risasi nne na kupoteza maisha papo hapo. Baada ya mauaji hayo, muuwaji Mark David Chapman aliiachia silaha na kukaa barabarani akisubiri akamatwe. Alikuhukumiwa kifungo cha maisha, na yupo jela...
....mpaka sasa.
08. MALCOM X
👉Kama ilivyo kwa luther King Jr, Malcom X nae alikuwa mwanaharakati aliyepigania haki za watu weusi . Alikuwa waziri kwa wakati huo na aliuawa mwaka 1965 baada ya kuamua kuwa Muislam wa kisuni na kuondoa uanachama wake katika chama cha National Islam. Wauwaji wote
....watatu walikuwa wanachama wa chama cha National Islam.
09. JUVENAL HABYARIMANA
👉Aliuwawa baada ya ndege yake kushambuliwa na watu wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo kuuwawa akiwemo raisi wa wakati huo wa Burundi. Mauaji haya ndiyo yaliyoamsha hasira za wanyarwanda hasa wahutu na kuanzisha vita shidi ya watutsi na baadae mauaji ya...
.....kimbari. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ufaransa, mauwaji haya yalifanywa na chama cha Patriotic front (RPC)na kumhusisha raisi wa sasa wa Rwanda Paul Kagame ambaye alikemea na kukana vikali tuhuma hizi na kusema kwamba wafaransa wanajaribuu tu kuficha uovu wao.
📸👇
#mwisho
#vitukuntu ♨️🔥
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.