▶️WAFAHAMU WATU MASHUHURI WALIOUWAWA KWA KUPIGWA RISASI. #uzi #vitukuntu
01. ABRAHAM LINCOLN
👉Alikuwa raisi wa 16 wa marekani na ndiye raisi wa kwanza wa marekani kuuawa akiwa madarakani. Aliuwawa mwaka 1865 na John Wilkes Booth aliyeudhiwa na maamuzi ya Lincoln ya kutambua....
....haki za watu weusi. Lincoln alipigwa risasi na John Wilkes Booth alipohudhuria kwenye maonyesho ya muziki. Booth nae aliuawa siku mbili baadae baada ya jaribio la kutoroka kushindikana.
(📸👇 John Wilkes Booth)
02. BENAZIR BHUTTO
👉Alikuwa waziri mkuu wa 11 wa Pakistani na kiongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa cha PPP. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la kiarabu akichagizwa na siasa zake safi za kidemokrasia. Aliuwawa disemba 27 mwaka 2007 akiwa kwenye gari yake aina ya....
....land cruiser akitoka kwenye mkutano wa kampeni. Gari hilo lililokuwa wazi juu lilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi lakini Bi. Bhutto alisimama ili kuwaunga mkono wafuasi wake ndipo alipopigwa risasi na baadae mlipuko ulitokea na kusababisha vifo vya watu.....
📸👇
.....wengine 2o katika eneo la tukio.
03. JOHN F KENNEDY (JFK)
👉Alikuwa raisi wa 35 wa marekani aliuwa November 22 mwaka 1963 akiwa raisi wa nne kuuawa kwa kupigwa risasi katika historia ya marekani. Akiwa na mkewe, kwenye gari la wazi akitoka kwenye hotuba alipigwa risasi tatu. Mpaka leo hakuna jibu la.....
📸👇
.....moja kwa moja juu ya nani aliyehusika kumuua John Kennedy japokuwa "Lee Hervey Oswald" ndiye aliehusishwa na mauaji hayo. Lee nae aliuwawa na raia mmoja (Jack Ruby) siku mbili tuu baadae alipokuwa akipelekwa rumande.
(📸👇 Lee Harvey Oswald)
👉Cha ajabu ni kwamba, John kennedy, Lee Oswald, na raia aliyemuua Oswald, wote walipoteza uhai wao katika hospitali ya Parkland Memorial kwa nyakati tofauti. Mdogo wa John aliyeitwa Robert F Kennedy nae aliuawa mwaka 1968 (alikuwa anawania uraisi wa marekani)
(📸👇 Jack Ruby)
04. MARTIN LUTHER KING JR
👉Anafahamika kwa harakati zake za kutetea usawa miongoni mwa waamerika weusi. Martin Luther king Jr ambaye alitumia dini yake ya kikristo kukemea ukandamizwaji wa watu weusi, aliuawa miaka mitatu baada ya mwanaharakati mwingine......
📸👇
....Malcom X kuuwawa mwaka 1965, wote wawili waliuwawa wakiwa na miaka 39.
👉Robert F. Kennedy aliyekuwa Mdogo wa raisi wa marekani (John F. kennedy), na Mgombea wa uraisi wa Marekani kwa kipindi hiko, alitoa hotuba ya kukemea vikali mauaji ya Martin Luther King Jr, cha kushangaza nae aliuwawa miezi kadhaa baadae!!
(📸👇 Robert F. Kennedy)
05. TUPAC SHAKUR
👉Hili si jina geni kwa mtu yeyote mpenzi wa muziki hasa miondoko ya hiphop. Alipigwa risasi Septemba 7, 1996 akitoka Las vegas Nevada alikokwenda kuhudhuria pambano la Mike Tyson, akiwa na Meneja wake Suge Knight (ambae pia anahusishwa na kifo hicho).
📸👇
👉2pac aliuwawa kwa kupigwa risasi kadhaa kifuani zilizotoka kwenye gari moja nyeupe iliyowazuia kwa pembeni. 2pac alifariki siku chache baadae katika hospitali ya University Medical Center of Southern Nevada. Wengi walihusishwa na kifo chake huku idadi kubwa ikimuelekea....
.....Christopher Wales (B.I.G) kuwa ndiye aliyehusika moja kwa moja na kifo cha Shakur. B.I.G na yeye aliuwawa miezi sita baadae na watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa 2pac kwa lengo la kulipa kisasi.
📸👇
06. MAHATMA GANDHI
👉Pia anafahamiaka kwa jina la "Mohandas Karamchand Gandhi". Gandhi ni maarufu kwa hotuba na kauli zake zinazotumiwa mpaka leo. Huyu ni kiongozi maarufu zaidi wa India iliyokuwa ikitawaliwa na Waingereza. Mahatma gandhi alikuwa kiongozi wa kiroho....
📸👇
....na kisiasa, aliuwawa tarehe 30 Januari mwaka 1948 na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu(Nathuram Godse) alipokuwa akielekea kufanya ibada.
(📸👇 Nathuram Godse)
07. JOHN LENNON
👉Nani halijui Kundi la vijana watanashati la The bittles? (kibongo-bongo “bitozi”) lilotamba miaka ya 1970 na 1980. John Lenon alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo lililotamba sana na alifariki tarehe 8 disemba mwaka 1980.
📸👇
👉Akiwa anaingia hotelini, Lenon alisikia sauti ikimuita na alipogeuka, alipigwa risasi nne na kupoteza maisha papo hapo. Baada ya mauaji hayo, muuwaji Mark David Chapman aliiachia silaha na kukaa barabarani akisubiri akamatwe. Alikuhukumiwa kifungo cha maisha, na yupo jela...
....mpaka sasa.
08. MALCOM X
👉Kama ilivyo kwa luther King Jr, Malcom X nae alikuwa mwanaharakati aliyepigania haki za watu weusi . Alikuwa waziri kwa wakati huo na aliuawa mwaka 1965 baada ya kuamua kuwa Muislam wa kisuni na kuondoa uanachama wake katika chama cha National Islam. Wauwaji wote
....watatu walikuwa wanachama wa chama cha National Islam.
09. JUVENAL HABYARIMANA
👉Aliuwawa baada ya ndege yake kushambuliwa na watu wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo kuuwawa akiwemo raisi wa wakati huo wa Burundi. Mauaji haya ndiyo yaliyoamsha hasira za wanyarwanda hasa wahutu na kuanzisha vita shidi ya watutsi na baadae mauaji ya...
.....kimbari. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ufaransa, mauwaji haya yalifanywa na chama cha Patriotic front (RPC)na kumhusisha raisi wa sasa wa Rwanda Paul Kagame ambaye alikemea na kukana vikali tuhuma hizi na kusema kwamba wafaransa wanajaribuu tu kuficha uovu wao.
▶️Yoshito Matsushige aliyezaliwa tarehe 2 January 1913, alikuwa manusura wa milipuko ya Hiroshima, na mpiga picha pekee ambaye aliweza kunasa picha za kihistoria zinazoonyesha uharibifu wa bomu la atomiki lililopigwa kwenye mji huo.
👉Mnamo mwaka 1941...... 👇👇 #uzi
.....Yoshito alijiunga na shirika la kuchapisha magazeti la Geibinichinichi, ambalo baadaye liliungana na Kampuni ya Chugoku Shimbun. Alipewa idara ya upigaji picha na baada ya 1944, pia alifanya kazi kama mshiriki wa ripoti ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Jeshi ...
..la mkoa wa Chugoku nchini Japan.
👉Mnamo Agosti 6,1945 (kipindi mlipuko unatokea), Yoshito Matsushige alikuwa na umri wa miaka 32, akiishi nyumbani kwake kwenye mji wa Midori-cho, Hiroshima. Nyumba yake ilikuwa maili 1.7 (Sawa na Kilometer 2.7), kutoka sehemu ambayo mlipuko..
▶️Josephine Myrtle Corbin alikuwa mtu wa kwanza kuzaliwa na sehemu za siri mbili na miguu minne, huko Tennessee mnamo 1868.
👉Josephine ilikuwa azaliwe akiwa na pacha wake, lakini waliungana kutoka kiunoni kwenda chini. Ugonjwa huu ambao unaitwa Dipygus, unatokana na...
....hali isiyo ya kawaida ya mapacha kuungana. Alikuwa ameongezeka maradufu umbo lake kutoka kiunoni kwenda chini kwa sababu ya hali hiyo isiyo ya kawaida, lakini kuanzia kiunoni kwenda juu alikuwa wa kawaida (kama anavyoonekana pichani) 📸👇
👉Miguu miwili (ambayo ndio ilikuwa ya pacha wake) kati ya minne ilikuwa midogo kuliko miguu yake halisi, lakini ilikuwa imeungana pamoja hivyo haikuwa ikimsumbua sana.
Josephine aliolewa na Clinton Bicknell akiwa na umri wa miaka 19, na walifanikiwa kupata watoto watano.....
▶️ Kifahamu Kivuko cha kwanza kabisa kuwahi kutumika Ulimwenguni..!! #vitukuntu #uzi
👉Je! Unajua kwamba kivuko cha kwanza ulimwenguni kilijengwa na Waturuki wakati wa Dola ya Ottoman..??
👇👇 U S I O N D O K E 👇👇
▶️Katika miaka ya 1800, usafirishaji uliofanyika katika pande zote za Bosphorus ulifanywa kwa kutumia boti. Katika miaka ya 1840, vivuko vidogo pia vilianza kutoa huduma za usafirishaji kwenye eneo hilo la Bosphorus lilopo nchini Uturuki.
📸👇(Bosphorus)
👉Mnamo mwaka1850, kivuko cha "kirket-i Hayriyye" kilianzishwa na huduma ya usafirishaji baharini ilianzishwa kwa watu wa Istanbul kupitia kivuko hiki. Hüseyin Haki Efendi, mmoja wa mameneja wa kivuko hicho, alikuwa mtu mbunifu na alikuwa akifikiria kwa miaka mingi juu ya...
▶️FAHAMU BAADHI YA REKODI ZA KUSHANGAZA ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI ZA DUNIA CHA GUINESS. #uzi #vitukuntu
01. Msichana mwenye miguu mirefu zaidi duniani.
👉Naam huyu ni "Maci Currin", binti wa miaka 17 tu akitokea kwenye nchini Marekani. Maci ameweka rekodi hii....
📸👇
....mwaka huu huu wa 2021. Maci ana urefu wa futi sita na inchi kumi, lakini miguu yake tuu imechukua karibu asilimia 60 ya urefu wake wote.
(Unaweza ukaangalia picha zake zaidi Instagram kwenye account yake ya @ _maci.currin_)
📸👇
02. Familia yenye nywele nyingi.
👉Familia ya Ramos Gomez iliweka rekodi ya ulimwengu kuwa familia kubwa zaidi yenye nywele nyingi za mwilini mnamo mwaka 2000. Ndugu wanne wa familia ya watu 19 kutoka Mexico walioitwa Victor Larry Gomez, Gabriel Danny Ramos Gomez,......
▶️LEO NIMEKULETEA HAPA BAADHI YA PICHA ZA "BEHIND THE SCENES" ZA FILAMU MAARUFU YA "APOCALYPTO" 🎥 #uzi #vitukuntu
📸👇🏾
▶️Filamu hii maarufu kutoka kiwanda cha kutengeneza filamu cha nchini Marekani (Hollywood) inayokwenda kwa jina la "Apocalypto" imekuwa ni mojawapo ya filamu nyingi zenye mafanikio na pia mvuto mkubwa kwa watamazaji.
👉🏾Filamu hii iliachiwa mnamo mwaka 2006.
Tuendelee..
👇🏾 👇🏾
▶️Filamu hii ilikuwa na lengo la dhati la kuelezea maisha ya kale ya wanadamu waliokuwa wakipatikana kwenye maeneo ya Amerika ya Kusini hususani wakazi waliokuwa wakiishi kwenye msitu mkubwa wa Amazon.
👉🏾Muongozaji mkuu wa filamu hii anajulikana kwa jina la "Mel Gibson"