Mobam🐦 Profile picture
~ Entrepreneur •Digital marketing enthusiast & Sales Expert •Let's unlock potential together •#Tech #DigitalMarketing #Lifeskills #Arsenal.

Jun 7, 2021, 20 tweets

#Simulizi_Uzi

SAFARI YANGU YA KUTO KUMWANI MWANAMKE KTK MAHUSIANO ILIPOANZIA.

Baada ya mahusiano ya miaka minne ya uaminifu na upendo kwa binti mmoja hivi jina kapuni, ndipo safari yangu ya kuto mwamini tena mwanamke katika mahusiano ilipoanzia kutokana na kile alichonifanyia.

Katika maisha yangu ya mahusino na huyo binti, nilikuwa mwaminifu sana pia nilimwamini kupita kiasi, siwezi sema labda sikuwa na uzoefu katika mapenzi laahasha,

nilikuwa na uzoefu kuliko hata binti mwenyewe yaani..🙌🏾

Kutokana na mazingira aliyokuwa ameyajenga kwangu ndio kilikuwa kichocheo kikubwa kilicho changia kumwamini kupita kiasi,

Kwa uaminifu niliokuwa nao hata kama ungempiga picha akiwa nyumba ya kulala wageni(guest)..

ukaniletea ningekupinga kwa nguvu zote na kukuambia ni photo shop hiyo, unaweza kujiuliza labda alikuwa ananipa nini laahasha utajiumiza kichwa kwa kujiuliza maswali,

mana kama mapenzi nilikuwa mkongwe kabla yake na nilikutana na wanaoyajua na kuyamudu hayo mambo ya kiutu uzima

Katika mapenzi binti alikuwa ni mgeni sana vitu vingi nilimpatia mafunzo kwa vitendo.😊

Kilicho kuja kubadilisha mtazamo wangu katika swala la uaminifu ilikuwa ni siku moja alipokuja kwangu,🤒

basi wakati nimekaa nae yapata mida ya saa nane mchana kuna mtu alikuwa anapiga simu yake,...

yule binti akawa hataki kupokea baada ya jamaa kukazana kupiga kama mara tatu nne hivi huku simu haipokelewi,

ikanibidi nimuulize binti swali kwanini hapokei na ni nani ane mpigia, hapa nikapewa jibu jepesi,.👇🏾👇🏾

kwamba kuna jamaa anamtaka hivyo huwa anamsumbua kwa kumpigia simu, nikamuuliza swali la pili,

je ulisha wahi kumwambia uko katika mahusiano, nikajibiwa ndiyo,haikupita muda akapiga tena nikapokea jamaa hakuongea baada ya kusikia sauti ya kiume,...

nikaamua kuishia hapo maswali yaliyo baki nikawa najiuliza mwenyewe na kujijibu.

Njia ya Muongo ni fupi sanaa....😁 unajua kuruka ruka koote kule yule binti aisee...🙌🏾

Ebu Tuvute Pumzi then wait muendelezo uta kuja soon weka...

Notification On tu Yaani usi kosee.....🤳

#RETWEET
Follow @iam_mobam

#Simulizi_Part_2

Unajua Njia ya muongo ni fupi sana😅 na siku zote ukiwa muongo usiwe msahaulifu, ilikuwa ya pata saa moja jioni kile kigiza cha usoni,...

nikaamua kwenda kuoga nikamuacha akiwa amejilaza kitandani, baada ya kufika bafuni nikagundua nimesahau sabuni chumbani,

nilipofika mlangoni nikasikia kama binti anaongea na simu basi nikafungua mlango taratibu kwa kunyata .....

kwa vile chumbani nilikuwa sijawasha taa kulikuwa na giza hivyo hakuweza kuniona..

Baada ya kuingia chumbani nikagundua alikuwa anaongea na yule jamaa aliekuwa akimpigia ile mida ya saa nane mchana,...

huku akimuuliza mbona ulikuwa haupokei simu na ninani aliepokea simu yako,

binti alijitetea sana huku akimwambia ni binamu yangu(Ma Causin hawaa)🤒, ulipopiga simu nilikuwa nae hivyo akasema ngoja leo akuzengue.

Akamalizia na neno moja kwamba naomba uniamini.

Nilivuta pumzi nikapiga konde moyo nikingojea wamalize maongezi yao,.sema inauma aisee usiombe ikukute kwa ulie mpenda😓..basi bana..

baada tu ya kumaliza maongezi nikamuuliza binamu umemaliza kuongea,..

alishikuta sana alipogundua kwamba nilikuwa chumbani na nilisikia kila alichokiongea, alilia na kuniomba msahama,..

sikumsamehe kwa siku hiyo baada ya majuma mawili ya kujitafakari nikaamua kutoa msamaha,...

tukaendeleza safari yetu ya mahusiano iliyokatika behewa moja la uaminifu, likawa limesalia moja tu la upendo.

Kiukweli Kuamini Amini Watu Muangalie wengine ni vijukuu vya shetani😂😂

Sasaa ww kaza fuvu tuu..mimi yame nikuta🤒🤒

So Baada ya wiki 3 Kupita Nikaja Gundua ana wasiliana na yule Causin..

Nilicho fanya nika mueka chini na kusema....

Ninge kua wa kwanza kwako ningesema nime kufanya uwe na tamaa ya wanaume ila sijawa wa kwanza kwako

Kuanzia sasaa Fuata mambo yako niache na mambo yangu ukiendelea kuni zoea nita kuchapa makofi ni bora uondoke kwa wema kama tulivyo kutana..

Alionesha kulia ila Mwisho wa reli ni kwakina Mpambazii..kigoma..ukweli ili niuma sana koz.

Nili amini yule binti anafaa kutengenezeka na kuja kua mama bora wa familia tulio iwaza kila uchwao kumbe ni bint hatar.

Basi hapo ndiyo mwanzo wangu kuto amini awa watu....kama yupo wa kuniaminisha tofaut na ninacho amini aniaminishe.🤳

#SHUKRANI_SANA_WANANGU

Huu Ni mwanzo wa Ziles Nyuzi Zetu...Nadhan Mna Kumbuka Baadhi Tulikua Tuna Ruka na Nyuz Ming sana Humu🤓🤓and mostly hua true tings🤳

#RETWEET
#LIKE
#comment

follow @iam_mobam

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling