Dolphin flow Profile picture
Animation for the soul😊🥀

Jun 14, 2021, 6 tweets

#UZII

Kuna vitu ukivifanya vinapelekea mtu mwingine apoteze HISIA na wewe kabisa.

Mara nyingi tumepoteza watu bila kujua kwa sababu ya kufanya vitu ambavyo vimepelekea kuwafukuza kwenye maisha yetu.

Cha Kwanza ni KULAUMU:
Hakuna anayependa kulaumiwa kila wakati.

Ukiwa mtu ambaye unalaumu sana, tena wakati mwingine bila hata kumsikiliza mwingine ama kumpa nafasi ya kujieleza, utapoteza watu wengi sana.

Kuna watu wakipiga simu tu wanaanza na kulaumu, wakiandika meseji wanaanza na kulaumu n.k

Ukiwa mtu wa hivi watu wataanza kukukwepa na watapoteza hisia na wewe.

Kingine ni tabia ya KUMTUMIA mtu:
Hii hutokea pale ambapo THAMANI ya mtu kwako haipo kwenye mahusiano mliyonayo bali kwa sababu unataka kumtumia tu uhapomuhitaji.

Yaani, wakati pekee unapoonyesha KUMPENDA au KUMTHAMINI ni pale unapotaka kumtumia tu!.

Baada ya hapo hauna habari naye tena.

Kuna watu ukiona wanakutafuta au wanakuambia maneno mazuri ujue wanataka kukutumia.

Ukiwa mtu wa hivi utapoteza watu wengi wa thamani.

Je, umeshawahi kukutana na mtu wa kulaumu tu au anayependa kukutumia tu?

RT Please wengine wajifunze🙏

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling